Yakobo 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Yakobo 2:1-26

Onyo Kuhusu Upendeleo

12:1 Mdo 7:2; 1Kor 2:8; Mit 24:23; Mdo 10:34Ndugu zangu, kama waaminio katika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe na upendeleo kwa watu. 22:2 Ebr 10:25Kwa maana kama akija mtu katika kusanyiko lenu akiwa amevaa pete ya dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia mtu maskini mwenye mavazi yaliyochakaa, 3nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,” 42:4 Yn 7:24je, hamjawabagua na kuwa mahakimu mioyoni mwenu mkihukumu kwa mawazo yenu maovu?

52:5 Yak 1:16, 19; Ay 34:19; 1Kor 1:26-28; Lk 12:21; Ufu 2:9; Yos 1:12Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao? 62:6 1Kor 11:22; Mdo 8:3; 16:19Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani? 7Je, si wao wanaolikufuru Jina lile lililo bora sana mliloitiwa?

82:8 Law 19:18; Mt 5:43Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema. 92:9 Kum 1:17; Yak 2:1Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 102:10 Mt 5:19; Gal 5:3Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. 112:11 Kut 20:14; Kum 5:18; 5:17; Kut 20:13Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria.

122:12 Yak 1:25; Mt 16:27Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru. 132:13 Mt 9:13; Lk 6:37Kwa kuwa hukumu bila huruma itatolewa kwa mtu yeyote asiyekuwa na huruma. Huruma huishinda hukumu.

Imani Na Matendo

142:14 Mt 7:26; Yak 1:22-25Ndugu zangu, yafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa anayo imani lakini hana matendo? Je, imani kama hiyo yaweza kumwokoa? 152:15 Mt 25:35, 36; Ay 31:19; Lk 3:11Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, 162:16 Lk 3:11; 1Yn 3:17, 18mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? 172:17 Yak 2:20, 26; Gal 5:6Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa.

182:18 Rum 3:28; Mt 7:16, 17; Yak 3:13Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.”

Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo. 192:19 Kum 6:4; Mt 12:29; 8:29; Lk 4:34Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.

202:20 Yak 2:17, 26Ewe mpumbavu! Je, wataka kujua kwamba imani bila matendo haifai kitu? 212:21 Mwa 22:9, 12Je, Abrahamu baba yetu hakuhesabiwa haki kwa kile alichotenda, alipomtoa mwanawe Isaki madhabahuni? 222:22 Ebr 11:17; 1The 1:3Unaona jinsi ambavyo imani yake na matendo yake vilikuwa vinatenda kazi pamoja, nayo imani yake ikakamilishwa na kile alichotenda. 232:23 Mwa 15:6; Rum 4:3; 2Nya 20:7; Isa 41:8Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu. 24Mnaona ya kwamba mtu huhesabiwa haki kwa yale anayotenda wala si kwa imani peke yake.

252:25 Ebr 11:31Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? 26Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.