Wimbo 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wimbo 5:1-16

Mpenzi

15:1 Yoe 3:18; Wim 4:12; 4:16; Isa 55:1Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu,

bibi arusi wangu;

nimekusanya manemane yangu pamoja

na kikolezo changu.

Nimekula sega langu la asali na asali yangu;

nimekunywa divai yangu na maziwa yangu.

Marafiki

Kuleni, enyi marafiki, mnywe;

kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.

Shairi La Nne

Mpendwa

25:2 Efe 5:275:2 Mit 8:4; Wim 6:9; 4:7; 1:15Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho.

Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha:

“Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu,

hua wangu, asiye na hitilafu.

Kichwa changu kimeloa umande,

na nywele zangu manyunyu ya usiku.”

3Nimevua joho langu:

je, ni lazima nivae tena?

Nimenawa miguu yangu:

je, ni lazima niichafue tena?

4Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo;

moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake.

5Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu,

mikono yangu ikidondosha manemane,

vidole vyangu vikitiririka manemane,

penye vipini vya komeo.

65:6 Wim 6:1-2; 3:15:6 Hos 5:15; Mao 3:8Nilimfungulia mpenzi wangu,

lakini mpenzi wangu alishaondoka;

alikuwa amekwenda zake.

Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake.

Nilimtafuta lakini sikumpata.

Nilimwita lakini hakunijibu.

75:7 Wim 3:3Walinzi walinikuta

walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini.

Walinipiga, wakanijeruhi,

wakaninyangʼanya joho langu,

hao walinzi wa kuta!

85:8 Wim 2:7; 1:14; 2:5Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza:

kama mkimpata mpenzi wangu,

mtamwambia nini?

Mwambieni ninazimia kwa mapenzi.

Marafiki

9Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani,

wewe uliye mzuri kupita wanawake wote?

Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani,

hata unatuagiza hivyo?

Mpendwa

105:10 Za 45:2Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu,

wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu.

11Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote,

nywele zake ni za mawimbi

na ni nyeusi kama kunguru.

125:12 Mwa 49:12; Wim 1:15Macho yake ni kama ya hua

kandokando ya vijito vya maji,

aliyeogeshwa kwenye maziwa,

yaliyopangwa kama vito vya thamani.

13Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo

yakitoa manukato.

Midomo yake ni kama yungiyungi

inayodondosha manemane.

145:14 Ay 28:6Mikono yake ni fimbo za dhahabu

iliyopambwa kwa krisolitho.

Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwa

iliyopambwa na yakuti samawi.

155:15 1Fal 4:33; Wim 7:4Miguu yake ni nguzo za marmar

zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi.

Sura yake ni kama Lebanoni,

bora kama miti yake ya mierezi.

165:16 Wim 4:3; 7:9; Yer 31:3; Rum 8:35Kinywa chake chenyewe ni utamu,

kwa ujumla yeye ni wa kupendeza.

Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu,

ee binti za Yerusalemu.