Wimbo 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wimbo 3:1-11

13:1 Isa 26:9; Wim 5:6Usiku kucha kwenye kitanda changu

nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye;

nilimtafuta, lakini sikumpata.

2Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,

katika barabara zake na viwanja;

nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.

Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.

33:3 Wim 5:7; Isa 21:6-11Walinzi walinikuta

walipokuwa wakizunguka mji.

Nikawauliza, “Je, mmemwona

yule moyo wangu umpendaye?”

43:4 Wim 8:2; 6:9; 8:5; Rum 8:35-39; Mit 8:17; 4:13Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita

nilimpata yule moyo wangu umpendaye.

Nilimshika na sikumwachia aende

mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu,

katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.

53:5 Wim 2:7; 8:4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza

kwa paa na kwa ayala wa shambani:

Msichochee wala kuamsha mapenzi

hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Tatu

Mpenzi

63:6 Wim 8:6; 4:6, 14; Kut 30:34; Yer 2:2Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani

kama nguzo ya moshi,

anayenukia manemane na uvumba

iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote

vya mfanyabiashara?

73:7 1Sam 8:11Tazama! Ni gari la Solomoni

lisindikizwalo na mashujaa sitini,

walio wakuu sana wa Israeli,

83:8 Ay 15:22; Za 91:5wote wamevaa panga,

wote wazoefu katika vita,

kila mmoja na upanga wake pajani,

wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.

9Mfalme Solomoni alijitengenezea gari;

alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.

103:10 Mt 22:37; Efe 3:19; Rum 5:8Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha,

kitako chake kwa dhahabu.

Kiti chake kilipambwa kwa zambarau,

gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo

na binti za Yerusalemu.

113:11 Isa 3:16; 54:5; 32:9-13; 62:5; Yer 3:14Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni,

mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji,

taji ambalo mama yake alimvika

siku ya arusi yake,

siku ambayo moyo wake ulishangilia.