Wimbo 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wimbo 2:1-17

Mpendwa

12:1 1Nya 27:29; Hos 14:5; Wim 5:13; Isa 55:1Mimi ni ua la Sharoni,

yungiyungi ya bondeni.

Mpenzi

2Kama yungiyungi katikati ya miiba

ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya wanawali.

Mpendwa

32:3 Mwa 3:6; Wim 1:4, 14; 4:16Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni

ndivyo alivyo mpenzi wangu

miongoni mwa wanaume vijana.

Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu,

na tunda lake ni tamu kwangu.

42:4 Es 1:11; Hes 1:52Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu,

na bendera ya huyu mwanaume

juu yangu ni upendo.

52:5 Wim 7:8; 5:8Nitie nguvu kwa zabibu kavu,

niburudishe kwa matofaa,

kwa maana ninazimia kwa mapenzi.

62:6 Wim 8:3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,

na mkono wake wa kuume unanikumbatia.

72:7 Wim 5:8; 3:5; 8:4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza

kwa paa na kwa ayala wa shambani:

Msichochee wala kuamsha mapenzi

hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Pili

Mpendwa

82:8 Wim 8:14Sikiliza! Mpenzi wangu!

Tazama! Huyu hapa anakuja,

akirukaruka juu milimani

akizunguka juu ya vilima.

92:9 2Sam 2:18; Wim 8:14Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana.

Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu,

akitazama kupitia madirishani,

akichungulia kimiani.

10Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia,

“Inuka, mpenzi wangu,

mrembo wangu, tufuatane.

11Tazama! Wakati wa masika umepita,

mvua imekwisha na ikapita.

12Maua yanatokea juu ya nchi;

majira ya kuimba yamewadia,

sauti za njiwa zinasikika

katika nchi yetu.

132:13 Nah 3:12; Wim 7:122:13 Mik 7:1; Isa 28:4; Yer 24:2; Hos 9:10Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni,

zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri.

Inuka, njoo mpenzi wangu.

Mrembo wangu, tufuatane.”

Mpenzi

142:14 Wim 8:13; Mwa 8:8; Wim 1:15Hua wangu penye nyufa za majabali,

mafichoni pembezoni mwa mlima,

nionyeshe uso wako,

na niisikie sauti yako,

kwa maana sauti yako ni tamu,

na uso wako unapendeza.

152:15 Amu 15:4; Wim 7:12; Eze 13:4; Za 80:13Tukamatie mbweha,

mbweha wale wadogo

wanaoharibu mashamba ya mizabibu,

mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua.

Mpendwa

162:16 Wim 7:10; 4:5; 6:3Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake,

yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

172:17 Wim 4:6; 1:14; Rum 13:12Mpaka jua linapochomoza,

na vivuli vikimbie,

rudi, mpenzi wangu,

na uwe kama paa,

au kama ayala kijana

juu ya vilima vya Betheri.