Wimbo 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wimbo 1:1-17

11:1 1Fal 4:32; Za 45Wimbo ulio bora wa Solomoni.

Shairi La Kwanza

Mpendwa

21:2 Wim 8:6; Mwa 14:18; Amu 9:13; Wim 4:10Unibusu kwa busu la kinywa chako,

kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.

31:3 Es 2:12; Za 45:8-14; Mhu 7:1Manukato yako yananukia vizuri,

jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa.

Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!

41:4 Yer 31:3; Flp 3:12; Wim 2:3Nichukue twende nawe, na tufanye haraka!

Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake.

Marafiki

Tunakushangilia na kukufurahia,

tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai.

Mpendwa

Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!

51:5 Wim 2:14; 2:7; 5:16; 4:3; Mwa 25:13Mimi ni mweusi, lakini napendeza,

enyi binti za Yerusalemu,

mweusi kama mahema ya Kedari,

kama mapazia ya hema la Solomoni.

61:6 Za 69:8; Wim 7:12; 8:12; 2:15Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi,

kwa sababu nimefanywa mweusi na jua.

Wana wa mama yangu walinikasirikia

na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu.

Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.

71:7 Wim 3:1-4; Isa 13:20; Mwa 24:65Niambie, wewe ambaye ninakupenda,

unalisha wapi kundi lako la kondoo

na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.

Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela

karibu na makundi ya rafiki zako?

Marafiki

81:8 Wim 5:9; 6:1Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,

fuata nyayo za kondoo,

na kulisha wana-mbuzi wako

karibu na hema za wachungaji.

Mpenzi

91:9 Wim 2:2; 2Nya 1:16-17Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike

aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.

101:10 Eze 16:11; Isa 61:10; Wim 5:13Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,

shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.

11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,

vyenye kupambwa kwa fedha.

Mpendwa

121:12 Wim 4:11-14Wakati mfalme alipokuwa mezani pake,

manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.

131:13 Mwa 37:25Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane

kati ya matiti yangu.

141:14 Wim 4:13; 1Sam 23:291:14 2Nya 20:2; Wim 2:3; 5:8Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina

kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.

Mpenzi

151:15 Wim 4:7; 7:6; Za 74:19; Yer 48:28Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!

Tazama jinsi ulivyo mzuri!

Macho yako ni kama ya hua.

Mpendwa

16Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!

Ee, tazama jinsi unavyopendeza!

Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.

Mpenzi

171:17 1Fal 6:9Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,

na mapao yetu ni miberoshi.