Warumi 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Warumi 9:1-33

Kuteuliwa Kwa Israeli Na Mungu

19:1 Gal 1:20; 1Tim 2:7; Rum 1:9Ninasema kweli katika Kristo, wala sisemi uongo, dhamiri yangu inanishuhudia katika Roho Mtakatifu. 29:2 Rum 10:1Nina huzuni kuu na uchungu usiokoma moyoni mwangu. 39:3 Kut 32:32; 1Kor 12:3; 16:22; Rum 11:14Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu hasa, wale walio wa kabila langu kwa jinsi ya mwili, 49:4 Kut 6:7; Kum 7:6; 4:13; Flp 1:12; Za 147:19; Ebr 9:1; Mdo 13:32; Gal 3:16yaani, watu wa Israeli, ambao ndio wenye kule kufanywa wana, ule utukufu wa Mungu, yale maagano, kule kupokea sheria, ibada ya kwenye Hekalu na zile ahadi. 59:5 Mt 1:1-16; Yn 1:1; Kol 2:9; Rum 1:3, 25; 2Kor 11:31Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Kristo alikuja kwa jinsi ya mwili kama mwanadamu, yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amen.

69:6 Rum 2:28, 29; Gal 6:16Si kwamba Neno la Mungu limeshindwa. Kwa maana si kila Mwisraeli ambaye ni wa uzao utokanao na Israeli ni Mwisraeli halisi. 79:7 Mwa 21:12; Ebr 11:18Wala hawakuwi wazao wa Abrahamu kwa sababu wao ni watoto wake, lakini: “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki.” 89:8 Rum 8:14; Gal 3:16; 4:23Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Abrahamu. 99:9 Mwa 18:10; 18:14Kwa maana ahadi yenyewe ilisema, “Nitakurudia tena wakati kama huu, naye Sara atapata mtoto wa kiume.”

109:10 Mwa 25:23; 25:21Wala si hivyo tu, bali pia watoto aliowazaa Rebeka walikuwa na baba huyo huyo mmoja, yaani, baba yetu Isaki. 119:11 Rum 8:28; 9:16; 8:28Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kwamba kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama, 129:12 Mwa 25:23si kwa matendo, bali kwa yeye mwenye kuita, Rebeka aliambiwa, “Yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.” 139:13 Mal 1:2-3; Kum 21:15; Mit 13:24; Mt 10:37; Lk 14:26; Yn 12:25Kama vile ilivyoandikwa, “Nimempenda Yakobo, lakini nimemchukia Esau.”

Mungu Hana Upendeleo

149:14 2Nya 19:7; Kum 32:4; Ay 8:3; 34:10; Za 92:15Tuseme nini basi? Je, Mungu ni dhalimu? La, hasha! 159:15 Kut 33:19Kwa maana Mungu alimwambia Mose,

“Nitamrehemu yeye nimrehemuye,

na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.”

169:16 Efe 2:8; Tit 3:5Kwa hiyo haitegemei kutaka kwa mwanadamu au jitihada, bali hutegemea huruma ya Mungu. 179:17 Kut 14:4; Za 76:10Kwa maana Maandiko yamwambia Farao, “Nilikuinua kwa kusudi hili hasa, ili nipate kuonyesha uweza wangu juu yako, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote.”

189:18 Yos 11:20; Rum 11:25Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia yeye atakaye kumhurumia na humfanya mgumu yeye atakaye kumfanya mgumu.

199:19 1Kor 15:35; Yos 2:18; 2Sam 16:10; Dan 4:35Basi mtaniambia, “Kama ni hivyo, kwa nini basi bado Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kupinga mapenzi yake?” 209:20 Isa 64:8; Yer 18:6; Isa 10:15Lakini, ewe mwanadamu, u nani wewe ushindane na Mungu? “Je, kilichoumbwa chaweza kumwambia yeye aliyekiumba, ‘Kwa nini umeniumba hivi?’ ” 219:21 2Tim 2:20Je, mfinyanzi hana haki ya kufinyanga kutoka bonge moja vyombo vya udongo, vingine kwa matumizi ya heshima na vingine kwa matumizi ya kawaida?

229:22 Rum 2:4Iweje basi, kama Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na kufanya uweza wake ujulikane, amevumilia kwa uvumilivu mwingi vile vyombo vya ghadhabu vilivyoandaliwa kwa uharibifu? 239:23 Rum 8:28; 8:30Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake, 249:24 Rum 8:28; 3:29yaani pamoja na sisi, ambao pia alituita, si kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa?

Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko

259:25 Hos 2:23; 1Pet 2:10Kama vile Mungu asemavyo katika Hosea:

“Nitawaita ‘watu wangu’

wale ambao si watu wangu;

nami nitamwita ‘mpenzi wangu’

yeye ambaye si mpenzi wangu,”

269:26 Hos 1:10; Mt 16:16tena,

“Itakuwa hasa mahali pale walipoambiwa,

‘Ninyi si watu wangu,’

wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ ”

279:27 Mwa 22:17; Isa 10:22-23; Hos 1:10; Yoe 2:32; Rum 11:5Isaya anapiga kelele kuhusu Israeli:

“Ingawa idadi ya wana wa Israeli

ni wengi kama mchanga wa pwani,

ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28Kwa kuwa Bwana ataitekeleza

hukumu yake duniani kwa haraka

na kwa ukamilifu.”

299:29 Yak 5:4; Isa 1:9; 13:19; Yer 50; 40Ni kama vile alivyotabiri Isaya akisema:

“Kama Bwana Mwenye Nguvu Zote

asingelituachia uzao,

tungelikuwa kama Sodoma,

tungelifanana na Gomora.”

Kutokuamini Kwa Israeli

309:30 Flp 3:9; Ebr 11:17Kwa hiyo tuseme nini basi? Kwamba watu wa Mataifa ambao hawakutafuta haki, wamepata haki ile iliyo kwa njia ya imani. 319:31 Isa 51:11; Rum 11:7; Gal 5:4Lakini Israeli, ambao walijitahidi kupata haki kwa njia ya sheria, hawakuipata. 329:32 1Pet 2:8Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kwa njia ya matendo. Wakajikwaa kwenye lile “jiwe la kukwaza.” 339:33 Isa 8:14; 1Pet 2:6, 8Kama ilivyoandikwa:

“Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu

na mwamba wa kuwaangusha.

Yeyote atakayemwamini

hataaibika kamwe.”