Warumi 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Warumi 6:1-23

Kufa Na Kufufuka Pamoja Na Kristo

16:1 Rum 3:5, 6Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka? 26:2 Kol 3:5, 8La hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi? 36:3 Mt 28:19Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 46:4 Mdo 2:24; Kol 2:12; 2Kor 5:17; Gal 6:15Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima.

56:5 Efe 2:6; 2Tim 2:11Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. 66:6 Gal 5:24; Kol 3:9; 2Kor 4:10; Gal 2:20; Rum 7:24Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. 76:7 1Pet 4:1; Rum 6:18Kwa maana mtu yeyote aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.

86:8 Rum 6:5; 2Tim 2:11Basi ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. 96:9 Mdo 2:24; Ufu 1:18Kwa maana tunajua kwamba Kristo, kwa sababu alifufuliwa kutoka kwa wafu, hawezi kufa tena; mauti haina tena mamlaka juu yake. 106:10 Rum 6:2; Ebr 7:27; 9:26-28; Gal 2:19; 1Pet 3:18Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu.

116:11 Rum 6:2; 2Kor 5:15; 1Pet 2:24Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. 126:12 Rum 6:16; Mwa 4:7; Za 19:13; 119:133Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. 136:13 Rum 7:5; 2Kor 5:156:13 1Pet 2:24Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki. 146:14 Rum 2:12; Gal 5:18; Rum 3:24Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.

Watumwa Wa Haki

156:15 1Kor 9:21Ni nini basi? Je, tutende dhambi kwa kuwa hatuko chini ya sheria bali chini ya neema? La, hasha! 166:16 Za 51:5; 2Pet 2:19Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu yeyote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii, aidha watumwa wa dhambi, ambayo matokeo yake ni mauti, au watumwa wa utii ambao matokeo yake ni haki? 176:17 Rum 1:18; 2Kor 2:14; 2Tim 1:13Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa. 186:18 Rum 8:2; 1Pet 4:1Nanyi, mkiisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mmekuwa watumwa wa haki.

196:19 Rum 3:5; Gal 3:15Ninasema kwa namna ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wenu wa hali ya asili. Kama vile mlivyokuwa mkivitoa viungo vya miili yenu kama watumwa wa mambo machafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi, hivyo sasa vitoeni viungo vyenu kama watumwa wa haki inayowaelekeza mpate kutakaswa. 206:20 Rum 6:16; Yn 8:34Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 216:21 Rum 6:23; Eze 16:61, 63; Rum 8:6, 13Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni mauti. 226:22 1Pet 2:16Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele. 236:23 Mit 10:16; Yak 1:15; Mt 25:46Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

羅馬書 6:1-23

與基督同死同活

1那麼,我們該怎麼說呢?我們可以繼續犯罪,使恩典更豐富嗎? 2當然不可!我們既然向罪死了,豈可繼續活在罪中? 3難道你們不知道,我們受洗歸屬基督耶穌是和祂一同死嗎? 4所以,我們藉著洗禮和祂同死同埋葬了,為要行事為人有新生命的樣式,正如基督藉著父的榮耀從死裡復活一樣。

5我們如果已經在基督的死亡上與祂聯合,也必在祂的復活上與祂聯合。 6我們知道,我們的舊人已經和祂一同被釘在十字架上,使轄制我們身體的罪失去力量,使我們不再做罪的奴隸。 7因為死去的人已經脫離了罪。

8我們如果已經與基督同死,相信也必與祂同活。 9因為我們知道,基督既然從死裡復活了,就不會再死,死亡也不能再控制祂。 10祂死,是向罪死,只死一次;祂活,卻是向上帝活著。 11同樣,你們在基督耶穌裡應當看自己是向罪死了,向上帝活著。

12所以,不要讓罪轄制你們必死的身體,使你們順從身體的私慾。 13也不要將你們的肢體獻給罪作不義的工具,而是要像一個從死裡復活的人將自己獻給上帝,把你們的肢體獻給上帝作義的工具。 14罪不能再主宰你們,因為你們已經不在律法之下,而是在恩典之中。

做義的奴僕

15那麼,我們在恩典之中,不在律法之下,就可以任意犯罪嗎?當然不可! 16你們難道不明白嗎?你們獻身為奴服從誰,就是誰的奴隸。做罪的奴隸,結局是死亡;作上帝的奴僕,就被稱為義人。 17感謝上帝!你們從前雖然做過罪的奴隸,現在卻衷心服從了所傳給你們的教導, 18從罪中得到釋放,成為義的奴僕。

19因為你們有人性的軟弱,我就用簡單的話向你們解釋。以前你們將肢體獻給骯髒不法的事,任其奴役,助長不法。現在你們要將肢體獻給義,為義效勞,成為聖潔的人。 20你們做罪的奴隸時,不受義的約束, 21做了現在引以為恥的事,得到什麼益處呢?那些事只能導致死亡! 22但現在你們已從罪中得到釋放,作了上帝的奴僕,結果使你們聖潔,最終得到永生。 23因為罪的代價就是死亡,而上帝藉著我們的主基督耶穌賜下的禮物則是永生。