Warumi 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Warumi 2:1-29

Hukumu Ya Mungu

12:1 Rum 1:20; 2Sam 12:5-7; Mt 7:12Kwa hiyo huna udhuru wowote, wewe utoaye hukumu kwa mwingine, kwa maana katika jambo lolote unalowahukumu wengine, unajihukumu wewe mwenyewe kwa sababu wewe unayehukumu unafanya mambo hayo hayo. 22:2 2Sam 12:5-7; Mt 7:12Basi tunajua kwamba hukumu ya Mungu dhidi ya wale wafanyao mambo kama hayo ni ya kweli. 3Hivyo wewe mwanadamu, utoapo hukumu juu yao na bado unafanya mambo yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? 42:4 Efe 3:8, 16; Kol 2:2; Rum 11:22; 3:25; Kut 34:6Au waudharau wingi wa wema, ustahimili na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu wakuelekeza kwenye toba?

52:5 1Pet 3:20; 2Pet 3:9Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa. 62:6 Za 62:12; Mt 16:27Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. 72:7 1Kor 15:53, 54; 2Tim 1:10Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. 82:8 2The 2:12Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. 92:9 1Pet 4:17; Rum 1:16; 3:9; Za 32:10Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia, 102:10 Rum 1:16; 2:9bali utukufu, heshima na amani kwa ajili ya kila mmoja atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, kisha kwa mtu wa Mataifa. 112:11 Mdo 10:34; 1Pet 1:17Kwa maana Mungu hana upendeleo.

122:12 1Kor 9:20, 21; Gal 4:21Watu wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria, nao wote wale waliotenda dhambi chini ya sheria watahukumiwa kwa sheria. 132:13 Yak 1:22, 23, 25Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki. 142:14 Mdo 10:34(Naam, wakati wa watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria. 152:15 Mhu 12:14; 1Kor 4:5; Mdo 10:42; Rum 16:25; 2Tim 2:8Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.) 162:16 Mhu 12:14; 1Kor 4:5; Mdo 10:42; Rum 16:25; 2Tim 2:8Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.

Wayahudi Na Sheria

172:17 Yer 8:8; Yn 5:45Tazama, wewe ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea sheria na kujisifia uhusiano wako na Mungu, 182:18 Flp 1:10; Kum 4:8; Za 147:19, 20; Flp 1:10kama unajua mapenzi ya Mungu na kukubali lililo bora kwa sababu umefundishwa na hiyo sheria, 192:19 Mt 15:14; Lk 18:9kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu, na mwanga kwa wale walio gizani, 202:20 2Tim 1:13; 3:5mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una maarifa ya kweli katika hiyo sheria, 212:21 Mt 23:3, 4; Za 50:16basi wewe, uwafundishaye wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, wewe mwenyewe waiba? 222:22 Mdo 19:32; Mal 3:8Wewe usemaye mtu asizini, wewe mwenyewe wazini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, wafanya jambo la kumchukiza katika mahekalu? 23Wewe ujivuniaye sheria, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja sheria? 242:24 Isa 52:5; 2Pet 2:2Kama ilivyoandikwa, “Kwa ajili yenu ninyi, Jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa watu wa Mataifa.”

252:25 Gal 5:3; Yer 4:4; 9:25, 26Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. 262:26 Rum 8:4; 1Kor 7:19Hivyo, ikiwa wale wasiotahiriwa wanatimiza mambo ambayo sheria inataka, je, kutokutahiriwa kwao hakutahesabiwa kuwa sawa na kutahiriwa? 272:27 Mt 12:41, 42Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana sheria ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja.

282:28 Mt 3:9; Yn 8:39Kwa maana mtu si Myahudi kwa vile alivyo kwa nje, wala tohara ya kweli si kitu cha nje au cha kimwili. 292:29 Flp 3:3; Kol 2:11; Rum 7:6; 2Kor 3:6; Yn 12:43; Gal 1:10Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.