Warumi 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Warumi 16:1-27

Salamu Kwa Watu Binafsi

116:1 2Kor 3:1; Mdo 18:18Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea. 216:2 Flp 2:29; 3Yn 5, 6; Mdo 9:13Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.

316:3 Mdo 18:2; Gal 5:6; Rum 8:1Wasalimuni Prisila16:3 Prisila kwa Kiyunani ni Priska, hivyo tafsiri nyingine zimemuita Priska. na Akila, watumishi wenzangu katika Kristo Yesu. 4Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu; wala si mimi tu ninayewashukuru bali pia makanisa yote ya watu wa Mataifa.

516:5 Kol 4:15; 1Kor 16:15Lisalimuni pia kanisa linalokutana nyumbani mwao.

Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Kristo huko Asia.

6Msalimuni Maria, aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.

716:7 Gal 1:22Wasalimuni Androniko na Yunia, jamaa zangu ambao wamekuwa gerezani pamoja nami. Wao ni maarufu miongoni mwa mitume, nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.

8Msalimuni Ampliato, yeye nimpendaye katika Bwana.

916:9 Rum 16:3Msalimuni Urbano, mtendakazi mwenzetu katika Kristo, pamoja na rafiki yangu mpendwa Stakisi.

1016:10 Mdo 11:14Msalimuni Apele aliyejaribiwa na akaithibitisha imani yake katika Kristo.

Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Aristobulo.

1116:11 Rum 16:7, 21; Mdo 11:14Msalimuni ndugu yangu Herodioni.

Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Narkisi walio katika Bwana.

12Wasalimuni Trifaina na Trifosa, wale wanawake wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana.

Msalimuni rafiki yangu mpendwa Persisi, mwanamke mwingine aliyefanya kazi kwa bidii katika Bwana.

1316:13 Mk 15:21Msalimuni Rufo, mteule katika Bwana, pamoja na mama yake, ambaye amekuwa mama kwangu pia.

14Wasalimuni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao.

1516:15 Mdo 9:13; 16; 2Wasalimuni Filologo, Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa na watakatifu wote walio pamoja nao.

1616:16 1The 5:26; 1Pet 5:14Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu.

Makanisa yote ya Kristo yanawasalimu.

Maelekezo Ya Mwisho

1716:17 1Tim 1:3; 6:3; Mt 18:15-17; 1Kor 14:20Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza. 1816:18 Flp 3:19; Kol 2:4Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno laini na ya kubembeleza, hupotosha mioyo ya watu wajinga. 1916:19 Rum 1:8; Mt 10:16; 1Kor 14:20Kila mtu amesikia juu ya utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu.

2016:20 Rum 15:33; Mwa 3:15Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi.

Neema ya Bwana wetu Yesu iwe nanyi. Amen.

2116:21 Mdo 16:1; 13:1; 17:6Timotheo, mtendakazi mwenzangu anawasalimu. Vivyo hivyo Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu.

22Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana.

2316:23 Mdo 19:22Gayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kanisa lote, anawasalimu.

Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu pia wanawasalimu.

[ 2416:24 Rum 16:20; 1The 5:28Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amen.]

Maneno Ya Mwisho Ya Kumsifu Mungu

2516:25 Flp 3:20; Rum 2:16; Isa 48:6; 1Tim 3:16Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. 2616:26 Efe 1:9; 2Tim 1:10; Tit 1:2, 3; 1Pet 1:20; Mdo 6:7Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii 2716:27 Rum 11:36; 1Tim 1:17; 6:16; Yud 25Mungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo utukufu ni wake milele na milele! Amen.