Warumi 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Warumi 15:1-33

Usijipendeze Mwenyewe, Bali Wapendeze Wengine

115:1 Rum 14:1; 1The 5:14Sisi tulio na nguvu, hatuna budi kuchukuliana na kushindwa kwa wale walio dhaifu wala si kujipendeza nafsi zetu wenyewe. 215:2 1Kor 10:33Kila mmoja wetu inampasa kumpendeza jirani yake kwa mambo mema, ili kumjenga katika imani. 315:3 2Kor 8:9; Za 69:9Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe, bali kama ilivyoandikwa: “Matukano yao wale wanaokutukana wewe yalinipata mimi.” 415:4 Rum 4:23, 24; 1Kor 10:11; 9:9, 10; 10:11; 2Tim 3:16, 17Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

515:5 2Kor 13:11; Efe 4:3Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 615:6 Ufu 1; 6; Za 34:3; Mdo 4:24, 32ili kwa moyo mmoja mpate kumtukuza Mungu aliye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Injili Sawa Kwa Wayahudi Na Kwa Watu Wa Mataifa

715:7 Rum 14:1; 5:2Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu. 815:8 Mt 15:24; Mdo 3:25, 26; 2Kor 1:20Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 915:9 Rum 3:29; Mt 9:8; 2Sam 22:50; Za 18:49pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:

“Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu wa Mataifa;

nitaliimbia sifa jina lako.”

1015:10 Kum 32:43Tena yasema,

“Enyi watu wa Mataifa, furahini

pamoja na watu wa Mungu.”

1115:11 Za 117:1Tena,

“Msifuni Bwana, ninyi watu wa Mataifa wote,

na kumwimbia sifa, enyi watu wote.”

1215:12 Ufu 5:5; Isa 11:10; Mt 12:21Tena Isaya anasema,

“Shina la Yese litachipuka,

yeye atakayeinuka ili kutawala juu ya mataifa.

Watu wa Mataifa watamtumaini.”

1315:13 Rum 14:17; 1Kor 4:20Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Paulo Mhudumu Wa Watu Wa Mataifa

1415:14 Efe 5:9; 2Pet 1:12Ndugu zangu, mimi mwenyewe ninasadiki kwamba mmejaa wema na ufahamu wote, tena mnaweza kufundishana ninyi kwa ninyi. 1515:15 Rum 12:3; 1:5; 12:3; Gal 1:15; Efe 3:7, 8Nimewaandikia kwa ujasiri vipengele kadha wa kadha katika waraka huu kama kuwakumbusha tena kwa habari ya ile neema Mungu aliyonipa, 1615:16 Mdo 9:5; Rum 11:13; 1:1; Isa 66:20ili kuwa mhudumu wa Kristo Yesu kwa watu wa Mataifa nikiwa na huduma ya kikuhani ya kutangaza Injili ya Mungu, ili watu wa Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.

1715:17 Flp 3:3; Ebr 2:17Kwa hiyo ninajisifu katika Kristo Yesu, kwenye utumishi wangu kwa Mungu. 1815:18 Mdo 15:12; Rum 1:15; 16:26Kwa maana sitathubutu kusema kitu chochote zaidi ya kile ambacho Kristo amefanya kwa kunitumia mimi katika kuwaongoza watu wa Mataifa wamtii Mungu kwa yale niliyosema na kufanya, 1915:19 Yn 4:48; Mdo 19:11; 22:17-21kwa nguvu za ishara na miujiza, kwa uweza wa Roho wa Mungu, hivyo kuanzia Yerusalemu hadi maeneo yote ya kandokando yake mpaka Iliriko, nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu. 2015:20 2Kor 10:15, 16Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari Njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine. 2115:21 Isa 52:15Lakini kama ilivyoandikwa:

“Wale ambao hawajahubiriwa habari zake wataona,

nao wale ambao hawajazisikia watafahamu.”

2215:22 Rum 1:13Hii ndiyo sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu.

Paulo Apanga Kwenda Rumi

2315:23 Mdo 19:21; 24:17Lakini sasa kwa kuwa hakuna nafasi zaidi kwa ajili yangu katika sehemu hii, ninatamani kuja kwenu kama ambavyo nimekuwa na shauku kwa miaka mingi. 2415:24 Rum 15:28; 1Kor 16:6; Tit 3:1Nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi mpaka huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo. 2515:25 Mdo 19:21; 24:17Sasa, niko njiani kuelekea Yerusalemu kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu huko. 2615:26 Rum 16:9; 2Kor 1:11; Kol 4:12Kwa kuwa imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya maskini walioko miongoni mwa watakatifu huko Yerusalemu. 2715:27 1Kor 9:11; Rum 9:4; 11:17; Gal 6:6Imewapendeza kufanya hivyo, naam, kwani ni wadeni wao. Kwa maana ikiwa watu wa Mataifa wameshiriki baraka za rohoni za Wayahudi, wao ni wadeni wa Wayahudi, ili Wayahudi nao washiriki baraka zao za mambo ya mwilini. 2815:28 Flp 4:17; Rum 15:24Kwa hiyo baada ya kukamilisha kazi hii na kuhakikisha kuwa wamepokea kila kitu kilichokusanywa, nitapitia kwenu nikiwa njiani kwenda Hispania. 2915:29 Rum 1:10; 1:11Ninajua kwamba nitakapokuja kwenu, nitakuja na wingi wa baraka za Kristo.

3015:30 Gal 5:22; 2Kor 1:11; Kol 4:12Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho Mtakatifu, kujiunga nami katika taabu zangu mkiniombea kwa Mungu. 3115:31 2Kor 1:10; 2Tim 3:11Ombeni ili nipate kuokolewa mikononi mwa wale wasioamini walioko Uyahudi, na kwamba utumishi wangu upate kukubaliwa na watakatifu wa huko Yerusalemu, 3215:32 Mdo 18:21; Rum 1:10, 13; 1Kor 16:18ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, nami niburudishwe pamoja nanyi. 3315:33 2The 3:16Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amen.