Walawi 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 24:1-23

Mafuta Na Mikate Mbele Za Bwana

1Bwana akamwambia Mose, 224:2 Kut 27:20; 39:37; Hes 8:2-4“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 324:3 Kut 12:14Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 424:4 Kut 25:31; 31:8Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.

524:5 Kut 25:30; Ebr 9:2; Law 23:13; Kut 40:24“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa24:5 Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo mbili. za unga kwa kila mkate. 624:6 Kut 25:23-30; Hes 4:7; 1Fal 7:48; Ebr 9:2; 1Nya 9:32Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. 724:7 Law 2:1-2Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto. 824:8 Kut 25:30; 1Nya 9:32; 2Nya 2:2-4; Mt 12:5Mikate hii itawekwa mbele za Bwana kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu. 924:9 Law 6:16-17; 8:31; Mt 12:4; Mk 2:26; Lk 6:4; 1Sam 9:21; Kut 29:33Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto.”

Mwenye Kukufuru Apigwa Mawe

10Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli. 1124:11 Kut 3:15; 18:22; 20:7; 31:2; 2Fal 6:33; Ay 1:11; Hes 1:4; 7:2; 10:15; 13:2; 17:2; Yos 7:18; 1Fal 7:18Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.) 1224:12 Kut 18:16; Hes 15:34Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao.

13Ndipo Bwana akamwambia Mose: 1424:14 Law 20:2; Kum 13:9; 17:5-7; Mdo 7:58“Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe. 1524:15 Kut 22:28; Law 5:1; Hes 9:13Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake; 1624:16 Kut 22:28; 21:21; 1Fal 21:10-13; Mt 26:66; Mk 14:64; Yn 10:33; Mdo 7:58; Za 74:10, 18yeyote atakayekufuru Jina la Bwana ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la Bwana, ni lazima auawe.

1724:17 Mwa 9:6; Kut 21:12; Kum 27:24; Hes 35:31; Mt 26:52; Ufu 13:10“ ‘Kama mtu yeyote atamuua mtu mwingine, ni lazima auawe. 18Mtu yeyote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai. 19Ikiwa mtu yeyote atamjeruhi jirani yake, chochote alichomtenda naye atatendewa: 2024:20 Kut 21:24; Mt 5:38; Law 19:34; Kum 10:17-19iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa. 2124:21 Kut 21:33Yeyote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini yeyote auaye mtu, lazima auawe. 2224:22 Kut 12:49; 22:21; Eze 47:22; Hes 9:14; 15:16Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

2324:23 Kum 13:9; 17:7Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.