Walawi 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 23:1-44

Sikukuu Zilizoamriwa

1Bwana akamwambia Mose, 223:2 Hes 29:39; Eze 44:24; Kol 2:16; Isa 6:3; Mt 6:9; Yn 12:28; Kut 32:5; Hes 10:2-3; 2Nya 30:5“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamriwa, sikukuu zilizoamriwa za Bwana, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu.

Sabato

323:3 Kut 20:9-10; Ebr 4:9-10; Kum 5:13; Hes 28:26; Lk 13:14; Neh 13:22; Isa 56:2; 58:13“ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwa Bwana.

Pasaka Na Mikate Isiyotiwa Chachu

(Hesabu 28:16-25)

423:4 Nah 1:15; Kut 23:14“ ‘Hizi ni sikukuu za Bwana zilizoamriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamriwa: 523:5 Kut 12:6-11; Hes 28:16-17; Kum 16:1-8; Yos 5:10Pasaka ya Bwana huanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. 623:6 Kut 12:17-19Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa kwanza, Sikukuu ya Bwana ya Mikate Isiyotiwa Chachu huanza; kwa siku saba, mtakula mikate isiyotiwa chachu. 7Katika siku ya kwanza, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. 8Kwa siku saba mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku hiyo ya saba mtafanya kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida.’ ”

Malimbuko

9Bwana akamwambia Mose, 1023:10 Hes 15:2; Law 19:9; Kut 22:29; 34:22; Rum 11:16; Kum 16:9; Yos 3:15; Mit 3:9; 1Kor 15:20; Yak 1:18“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa nafaka ya kwanza mtakayovuna. 1123:11 Kut 29:24; 28:38; Law 9:21; 10:14Naye atauinua huo mganda mbele za Bwana ili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato. 1223:12 Law 12:6; Kut 12:5Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwa Bwana dhabihu ya kuteketezwa kwa moto ya mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, 1323:13 Law 2:14-16; 6:20; 10:9; 24:5; Hes 15:6; 28:9; Mwa 35:14pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa23:13 Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo mbili. za unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hini23:13 Robo ya hini ni sawa na lita moja. ya divai. 1423:14 Yos 5:11; Rut 2:14; 1Sam 17:17; 25:18; 2Sam 17:28; Kut 34:26; Law 3:17; Hes 10:8; 15:21; Yer 2:3Kamwe msile mkate wowote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wenu sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.

Sikukuu Ya Majuma

(Hesabu 28:26-31)

15“ ‘Tangu siku ile iliyofuata Sabato, siku mliyotoa sadaka ya mganda wa kuinuliwa, hesabuni majuma saba kamili. 1623:16 Mdo 20:16; 2:1; Hes 28:26Mtahesabu siku hamsini mpaka siku inayofuata Sabato ya saba, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwa Bwana. 1723:17 Kut 34:22; 23:16; Hes 15:17-19Kutoka popote mnapoishi, mtaleta mikate miwili ya unga laini, sehemu mbili za kumi za efa, uliookwa kwa chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwa Bwana. 1823:18 Kut 29:41; 30:9; 37:16; Yer 19:13; 44:18Toeni pamoja na hiyo mikate wana-kondoo saba, kila mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, na fahali mchanga, na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa Bwana, pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, sadaka iliyotolewa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 1923:19 Hes 28:30; Law 4:23Kisha toeni dhabihu ya mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili, kila mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya amani. 2023:20 Kut 29:24Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwa Bwana kwa ajili ya kuhani. 2123:21 Kut 32:5Siku iyo hiyo mtatangaza kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.

2223:22 Law 19:9-10; Kum 24:19-21; Rut 2:2, 15; Kut 23:11; Kum 15:1-18; Ay 20:19; Za 112:9; Mit 14:31; Isa 58:7-8; Yak 2:1“ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

Sikukuu Ya Tarumbeta

(Hesabu 29:1-6)

23Bwana akamwambia Mose, 2423:24 Ezr 3:1; Hes 10:9-10; 29:1; 31:6; 2Fal 11:14; 2Nya 13:12; Za 98:6“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu la ukumbusho litakaloadhimishwa kwa kupiga tarumbeta. 25Msifanye kazi zenu zozote za kawaida, lakini toeni sadaka kwa Bwana iliyoteketezwa kwa moto.’ ”

Siku Ya Upatanisho

(Hesabu 29:7-11)

26Bwana akamwambia Mose, 2723:27 Law 16:29; Kut 30:10; Hes 29:7; Isa 58:3-5; Dan 10:3, 12“Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. 28Msifanye kazi siku hiyo, kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ambapo upatanisho unafanyika kwa ajili yenu mbele za Bwana Mungu wenu. 2923:29 Mwa 17:14; Law 7:20; Hes 5:2Mtu yeyote ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. 3023:30 Law 20:3Mtu yeyote atakayefanya kazi siku hiyo nitamwangamiza kutoka miongoni mwa watu wake. 3123:31 Law 3:17Hamtafanya kazi kamwe. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo popote mnapoishi. 3223:32 Law 16:31; Neh 13:19Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”

Sikukuu Ya Vibanda

(Hesabu 29:12-40)

33Bwana akamwambia Mose, 3423:34 1Fal 8:2; Hag 2:1; Kut 23:16; Yn 7:2, 37; Kut 34:22; Ezr 3:4; Neh 8:14; Zek 14:16“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya Bwana ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba. 35Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida. 3623:36 1Fal 8:2; 2Nya 7:9; Neh 8:18; Yn 7:37; Law 1:9Kwa siku saba toeni sadaka kwa Bwana za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.

37(“ ‘Hizi ni sikukuu za Bwana zilizoamriwa, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu kwa kuleta sadaka kwa Bwana za kuteketeza kwa moto: sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, dhabihu na sadaka za vinywaji zitahitajika kila siku. 3823:38 Kut 20:10; 2Nya 2:4; Eze 45:17; Law 7:16Sadaka hizi ni nyongeza ya zile mnazozitoa katika Sabato za Bwana, na pia ni nyongeza ya matoleo yenu ya chochote mlichoweka nadhiri, na sadaka zenu zote za hiari mnazozitoa kwa Bwana.)

3923:39 Isa 62:9; Kut 23:16; Kum 16:13; Mt 21:8“ ‘Basi kuanzia siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, baada ya kuvuna mazao yote ya nchi, mtaadhimisha sikukuu kwa Bwana kwa siku saba; siku ya kwanza ni mapumziko, pia siku ya nane ni mapumziko. 4023:40 Za 9:2; 66:6; 105:43; 118:27; 137:2; Neh 8:10, 14-17; Isa 44:4; Kum 12:7; 14:26; 28:47; Yoe 2:26Siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za Bwana Mungu wenu kwa siku saba. 41Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa Bwana kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni mwezi wa saba. 4223:42 Kut 23:16; Neh 8:14-16Mtaishi katika vibanda kwa siku saba: Wazawa wote wa Waisraeli wataishi katika vibanda, 4323:43 Kum 31:13; Za 78:5ili wazao wenu wajue kuwa niliwafanya Waisraeli waishi kwenye vibanda nilipowatoa Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

44Kwa hiyo Mose akawatangazia Waisraeli sikukuu zilizoamriwa na Bwana.