Walawi 21 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 21:1-24

Sheria Kwa Ajili Ya Makuhani

121:1 Kut 28:1; Law 5:3; 13:3; Hes 5:2; 6:6; 19:11; 31:19; Eze 44:25Bwana akamwambia Mose, “Sema na makuhani, wana wa Aroni, uwaambie: ‘Kamwe kuhani asijitie unajisi kwa utaratibu wa kiibada kwa ajili ya mtu wake yeyote anayekufa, 2isipokuwa jamaa wake wa karibu, kama vile mama yake au baba yake, mwanawe au binti yake, ndugu yake, 321:3 Hes 6:6; 21:5; Law 13:40; 19:28; Yer 7:29; 16:6; Eze 5:1; 44:20au dada yake asiyeolewa ambaye anamtegemea kwa kuwa hana mume, kwa ajili ya hao aweza kujitia unajisi. 4Kamwe asijitie unajisi mwenyewe kutokana na wale watu ambao anahusiana nao kwa kuoana, na hivyo kujitia unajisi.

5“ ‘Kamwe makuhani wasinyoe nywele za vichwa vyao wala wasinyoe pembeni mwa ndevu zao, au kuweka chale kwenye miili yao. 621:6 Ezr 8:28; Law 18:21; 3:11; 22:25; 10:3; Kut 19:22; Law 20:7; Za 15:4; Mt 5:33-37; Yak 5:12Lazima wawe watakatifu kwa Mungu wao, na kamwe wasilinajisi jina la Mungu wao. Kwa sababu ndio wanaotoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Bwana, chakula cha Mungu wao, hivyo lazima wawe watakatifu.

721:7 Eze 44:22; 21:8; Law 3:11; Kut 31:13; 21:9; Mwa 38:24; Law 19:29; Kut 29:29; Hes 35:25; Kut 28:2“ ‘Kamwe wasioe wanawake waliojinajisi kwa ukahaba, au waliopewa talaka na waume wao, kwa sababu makuhani ni watakatifu kwa Mungu wao. 8Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu Mimi Bwana ni mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi kuwa watakatifu.

9“ ‘Ikiwa binti wa kuhani anajitia unajisi kwa kufanya ukahaba, anamwaibisha baba yake; lazima achomwe kwa moto.

1021:10 Kut 29:7; Law 8:7-13; 16:4; 10:6“ ‘Kuhani mkuu, yule miongoni mwa ndugu zake ambaye amekwisha kutiwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake, na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa, wala asirarue nguo zake. 1121:11 Hes 5:2; 6:6; 9:6; 19:11-14; 31:19; Law 19:28Kamwe asiingie mahali palipo maiti ndani. Kamwe asijitie unajisi, hata kwa ajili ya baba yake au mama yake, 1221:12 Kut 25:8; 28:41; Law 10:7wala asiondoke mahali patakatifu pa Mungu wake au kupanajisi, kwa sababu amewekwa wakfu kwa mafuta ya Mungu wake. Mimi ndimi Bwana.

1321:13 Eze 44:22“ ‘Mwanamke kuhani atakayemwoa lazima awe bikira. 14Kamwe asimwoe mjane, au mwanamke aliyepewa talaka, wala mwanamke aliyejinajisi kwa ukahaba, bali atamwoa tu bikira kutoka miongoni mwa watu wake, 1521:15 Rum 12:1; 1Kor 3:16; Efe 5:17; 1The 4:1-8na hivyo hatawatia unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. Mimi ndimi Bwana, nimfanyaye mtakatifu.’ ”

16Bwana akamwambia Mose, 1721:17 Hes 16:5; Za 64:4“Mwambie Aroni: ‘Kwa vizazi vijavyo, hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake. 1821:18 Law 22:19-25; 19:14; 2Sam 4:4; 9:3; 19:26Hakuna mtu mwenye dosari yoyote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili, 19hakuna mtu mwenye mguu au mkono uliolemaa, 2021:20 Law 22:24; Kum 23:1; Isa 56:3au mwenye kibiongo au aliyedumaa, au aliye na tatizo la macho, au aliye na uvimbe wenye usaha au majipu, au aliyehasiwa. 2121:21 Law 3:11; 22:19Hakuna mzao wa kuhani Aroni mwenye kilema chochote atakayekaribia kutoa sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Kama ana kilema, kamwe asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake. 2221:22 1Kor 9:13Anaweza kula chakula kitakatifu sana cha Mungu wake, pia hata chakula kitakatifu. 2321:23 Kut 25:8; Law 20:8; Hes 18:19Lakini kwa sababu ya kilema chake, kamwe asikaribie karibu na pazia wala kukaribia madhabahu, asije akanajisi mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Bwana, niwafanyaye watakatifu.’ ”

24Basi Mose akamwambia Aroni jambo hili na wanawe, pamoja na Waisraeli wote.

New International Version

Leviticus 21:1-24

Rules for Priests

1The Lord said to Moses, “Speak to the priests, the sons of Aaron, and say to them: ‘A priest must not make himself ceremonially unclean for any of his people who die, 2except for a close relative, such as his mother or father, his son or daughter, his brother, 3or an unmarried sister who is dependent on him since she has no husband—for her he may make himself unclean. 4He must not make himself unclean for people related to him by marriage,21:4 Or unclean as a leader among his people and so defile himself.

5“ ‘Priests must not shave their heads or shave off the edges of their beards or cut their bodies. 6They must be holy to their God and must not profane the name of their God. Because they present the food offerings to the Lord, the food of their God, they are to be holy.

7“ ‘They must not marry women defiled by prostitution or divorced from their husbands, because priests are holy to their God. 8Regard them as holy, because they offer up the food of your God. Consider them holy, because I the Lord am holy—I who make you holy.

9“ ‘If a priest’s daughter defiles herself by becoming a prostitute, she disgraces her father; she must be burned in the fire.

10“ ‘The high priest, the one among his brothers who has had the anointing oil poured on his head and who has been ordained to wear the priestly garments, must not let his hair become unkempt21:10 Or not uncover his head or tear his clothes. 11He must not enter a place where there is a dead body. He must not make himself unclean, even for his father or mother, 12nor leave the sanctuary of his God or desecrate it, because he has been dedicated by the anointing oil of his God. I am the Lord.

13“ ‘The woman he marries must be a virgin. 14He must not marry a widow, a divorced woman, or a woman defiled by prostitution, but only a virgin from his own people, 15so that he will not defile his offspring among his people. I am the Lord, who makes him holy.’ ”

16The Lord said to Moses, 17“Say to Aaron: ‘For the generations to come none of your descendants who has a defect may come near to offer the food of his God. 18No man who has any defect may come near: no man who is blind or lame, disfigured or deformed; 19no man with a crippled foot or hand, 20or who is a hunchback or a dwarf, or who has any eye defect, or who has festering or running sores or damaged testicles. 21No descendant of Aaron the priest who has any defect is to come near to present the food offerings to the Lord. He has a defect; he must not come near to offer the food of his God. 22He may eat the most holy food of his God, as well as the holy food; 23yet because of his defect, he must not go near the curtain or approach the altar, and so desecrate my sanctuary. I am the Lord, who makes them holy.’ ”

24So Moses told this to Aaron and his sons and to all the Israelites.