Walawi 20 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 20:1-27

Adhabu Kwa Ajili Ya Dhambi

1Bwana akamwambia Mose, 220:2 Mwa 26:11; Kut 19:21; Law 24:14; Hes 15:35-36; Kum 21:21; Yos 7:25; 2Fal 17:17; 23:10; 2Nya 33:6“Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa yeyote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe. 320:3 Law 23:30; 15:31; 18:21; Za 74:7; 79:1; Yer 7:30; Eze 5:11; Hes 19:20Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu. 420:4 Kum 17:2-5Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho wakati mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, nao wakaacha kumuua, 520:5 Kut 20:5; Law 17:7mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo pamoja na jamaa yake, nami nitawakatilia mbali yeye na watu wote waliofanya ukahaba na Moleki.

620:6 Law 19:31“ ‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayeenda kwa waaguzi na wenye pepo, na hivyo kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake.

720:7 Law 11:44, 45; Kut 29:1; 31:13; Efe 1:4; 1Pet 1:16; Kut 6:2; 20:2“ ‘Jitakaseni basi, nanyi kuweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 820:8 Mwa 26:5; Kut 31:13; Eze 20:12Shikeni amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

920:9 Kut 20:12; 21:17; Yer 35:16; Mal 1:6; 2:10; Kum 21:21; 22:30; 27:16; Eze 18:13; 22:7; 33:4-5; Mt 15:4; Mk 7:10; Yos 2:19; 2Sam 1:16; 3:29; 1Fal 2:37“ ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani baba yake au mama yake, lazima auawe. Amemlaani baba yake au mama yake, nayo damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

1020:10 Kut 20:14; 21:12; Kum 5:18; 22:22; Yn 8:5; Mwa 38:24“ ‘Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe.

1120:11 Law 18:7-8; Kum 27:23“ ‘Kama mtu atakutana kimwili na mke wa baba yake, hakumheshimu baba yake. Mwanaume huyo na mwanamke huyo wote wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

1220:12 Mwa 11:31; 38:16; Law 18:15“ ‘Ikiwa mtu atakutana kimwili na mke wa mwanawe, lazima wote wawili wauawe. Walichokifanya ni upotovu; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

1320:13 Law 18:22“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

1420:14 Law 18:8, 17; 21:9; Hes 16:39; Amu 14:15; 15:6; Kum 27:23“ ‘Ikiwa mwanaume ataoa binti pamoja na mama yake, huo ni uovu. Wote watatu ni lazima wachomwe moto, ili kwamba pasiwepo na uovu katikati yenu.

1520:15 Kut 20:10; 22:19; Law 18:23; 18:9; 5:1; Mwa 17:14; 20:12“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mnyama, ni lazima auawe, na pia ni lazima mnyama huyo auawe.

16“ ‘Kama mwanamke atamsogelea mnyama kukutana naye kimwili, muueni mwanamke huyo pamoja na mnyama pia. Lazima wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

1720:17 Mwa 26:5; Kut 31:13; Eze 20:12; Mwa 26:5; Kut 31:13; Eze 20:12“ ‘Ikiwa mtu anamwoa dada yake, binti aliyezaliwa na baba yake au mama yake, nao wakakutana kimwili, ni aibu. Lazima wakatiliwe mbali machoni pa watu wao. Huyo mwanaume amemwaibisha dada yake, hivyo atawajibika kwa ajili ya uovu huo.

1820:18 Law 15:24; Eze 18:6; 20:19; Law 18:2, 12“ ‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.

19“ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.

2020:20 Law 18:13-14; Mwa 15:2“ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na shangazi yake, amemwaibisha mjomba wake. Nao watawajibika kwa ajili ya uovu huo; watakufa bila kuzaa mtoto.

2120:21 Law 18:16; Mt 14:4; Mk 6:18“ ‘Ikiwa mwanaume ataoa mke wa ndugu yake, hili ni tendo chafu; amemwaibisha ndugu yake. Nao hawatazaa mtoto.

2220:22 Mwa 26:5; Law 18:25-28“ ‘Zishikeni amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike. 2320:23 Law 18:3, 24-25, 27-30Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nami nikachukizwa sana nao. 2420:24 Kut 3:8; 13:5; 33:16; Hes 14:8; 16:14; 1Fal 8:53; Za 135Lakini niliwaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, ambaye amewatenga kutoka mataifa.

2520:25 Law 10:10; Kum 14:3-21; Mdo 10:14; Law 11:47“ ‘Kwa hiyo, ninyi lazima mweze kutofautisha kati ya wanyama walio safi na wasio safi, pia kati ya ndege wasio safi na walio safi. Msijitie unajisi kutokana na mnyama yeyote, au ndege, wala kitu chochote kitambaacho juu ya ardhi, vile ambavyo nimevitenga kuwa najisi kwa ajili yenu. 2620:26 Kum 14:2; Law 19:2; Yos 24:19; 2Fal 19:22Mtakuwa watakatifu kwangu, kwa sababu Mimi, Bwana, ni mtakatifu, nami nimewatenga kutoka mataifa kuwa wangu mwenyewe.

2720:27 Kut 22:18; Law 19:31; 24:14; Kum 18:10; 1Sam 28:7“ ‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’ ”