Walawi 11 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 11:1-47

Vyakula Najisi Na Visivyo Najisi

(Kumbukumbu 14:3-21)

1Bwana akawaambia Mose na Aroni, 211:2 Mdo 10:12-14; Kum 14:4; Eze 4:4; Mt 15:11; Rum 14:2; 1Kor 8:8; Kol 2:16; Ebr 9:10“Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala: 3Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.

4“ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu. 5Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. 611:6 1Tim 4:4-5Sungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. 711:7 Isa 65:4; 66:3, 17Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, hacheui; huyo ni najisi kwenu. 811:8 Isa 52:11; Law 5:2; Ebr 9:10; Mt 15:11, 20; Mdo 10:14-15; 15:29; Rum 14:14-17; 1Kor 8:8Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu.

9“ ‘Kuhusu viumbe wote wanaoishi ndani ya maji ya bahari na vijito, mtakula wale wote wenye mapezi na magamba. 1011:10 Law 7:18; Kum 14:3Lakini viumbe wote ndani ya bahari au vijito wasio na mapezi na magamba, wakiwa miongoni mwa makundi au viumbe wote ndani ya maji, hao ni machukizo kwenu. 1111:11 Law 5:2Nao watakuwa machukizo kwenu. Msile nyama yao, nayo mizoga yao itakuwa machukizo. 12Chochote kinachoishi ndani ya maji ambacho hakina mapezi na magamba kitakuwa chukizo kwenu.

1311:13 Kum 14:12; Rum 14:1-23“ ‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu, 1411:14 Mwa 1:11mwewe mwekundu, aina zote za mwewe mweusi, 1511:15 Mwa 8:7aina zote za kunguru, 16mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za kipanga, 17bundi, mnandi, bundi mkubwa, 1811:18 Isa 13:21; 14:23; 34:11-14; Sef 2:14mumbi, mwari, nderi, 1911:19 Zek 5:9; Mwa 1:11; Isa 2:20korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

2011:20 Mdo 10:14; 11:22; Mt 3:4; Mk 1:6“ ‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu. 21Lakini wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi. 22Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi. 23Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu.

Wanyama Ambao Ni Najisi

2411:24 Law 5:2; 13:3; 14:46; 15:5; 22:6; Hes 19:7, 19; Amu 6:5; Yer 46:23; Nah 3:17“ ‘Mtajinajisi kwa wanyama hawa. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. 2511:25 Kut 19:10; Law 13:6, 34; 14:8; 15:5; 16:26; Hes 8:7; 19:7-8; 31:24Yeyote atakayebeba mizoga ya viumbe hawa ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

26“ ‘Kila mnyama mwenye ukwato ulioachana lakini haukugawanyika kabisa, au yule asiyecheua, huyo ni najisi kwenu; yeyote agusaye mzoga wowote wa hao atakuwa najisi. 27Miongoni mwa wanyama wote watembeao kwa miguu minne, wale watembeao kwa vitanga vyao ni najisi kwenu; yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. 2811:28 Ebr 9:10; 11:29; Isa 66:17; Ebr 9:10; Isa 66:17Yeyote atakayebeba mizoga yao ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Wanyama hawa ni najisi kwenu.

29“ ‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yoyote ya mijusi mikubwa, 3011:30 Za 58:8; Isa 2:20guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga. 31Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. 3211:32 Law 15:12; Hes 19:18; 31:20Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi mpaka jioni, kisha kitakuwa safi tena. 3311:33 Law 6:28; 15:12Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho. 34Chakula chochote ambacho chaweza kuliwa lakini kikawa kimeingia maji kutoka kwenye chungu hicho ni najisi, na kitu chochote cha majimaji ambacho chaweza kunyweka kutoka kwenye chungu hicho ni najisi. 35Chochote ambacho mzoga wa mmojawapo utaangukia kitakuwa najisi. Jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi. 36Lakini chemchemi au kisima, mahali pa kuchota maji, patakuwa safi, lakini yeyote atakayegusa moja ya mizoga hii ni najisi. 37Kama mzoga ukianguka juu ya mbegu zozote ambazo ni za kupanda, zinabaki safi. 38Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu.

3911:39 Law 17:15; 22:4, 8; Kum 14:21; Eze 4:14; 44:31; Hes 19:11“ ‘Kama mnyama ambaye mnaruhusiwa kumla akifa, yeyote atakayeugusa mzoga wake atakuwa najisi mpaka jioni. 4011:40 Law 14:8; 17:15; 22:8; Eze 44:31; Ebr 9:10Yeyote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.

41“ ‘Kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi ni chukizo; kisiliwe. 42Msile kiumbe chochote kitambaacho juu ya ardhi, kiwe kitambaacho kwa tumbo lake, au kitambaacho kwa miguu minne au kwa miguu mingi; ni chukizo. 4311:43 Law 20:5; 22:5Msijitie unajisi kwa chochote katika viumbe hivi. Msijitie unajisi kwa viumbe hivyo au kutiwa unajisi navyo. 4411:44 Kut 6:2, 7; 19:10; 20:2; 22:31; 31:13; Isa 43:3; 51:15; Eze 20:5; Law 19:2; 20:7; Hes 15:40; Yos 3:5; 7:13; 24:19; 1Nya 15:12; 2Nya 29:5; 35:6; Kum 14:2; 1Sam 2:2; Ay 6:10; Za 99:3; Efe 1:4; 1The 4:7; 1Pet 1:15-16Mimi ndimi Bwana Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi. 4511:45 Law 25:38, 55; Mwa 17:7; Kut 6:7; 19:6; 1Pet 1:16; Rum 14:17; 1Kor 6:11Mimi ndimi Bwana niliyewapandisha mtoke Misri ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo kuweni watakatifu kwa sababu Mimi ni mtakatifu.

46“ ‘Haya ndiyo masharti kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kiendacho juu ya ardhi. 4711:47 Law 10:10; Yer 15:19; Eze 22:26; 44:23Ni lazima mpambanue kati ya kilicho najisi na kilicho safi, kati ya viumbe hai vinavyoweza kuliwa na vile visivyoweza kuliwa.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

利未記 11:1-47

有關食物的條例

1耶和華對摩西亞倫說: 2「你們把以下條例告訴以色列人。

「地上的動物, 3凡是蹄子分瓣且反芻的,你們都可以吃。 4但你們不可吃只有蹄子分瓣或只反芻的動物。駱駝不潔淨,因為牠雖反芻但蹄子不分瓣; 5獾不潔淨,因為牠雖反芻但蹄子不分瓣; 6野兔不潔淨,因為牠雖反芻但蹄子不分瓣; 7豬不潔淨,因為牠蹄子雖分瓣但不反芻。 8你們不可吃牠們的肉,也不可摸牠們的屍體,因為牠們對你們來說不潔淨。

9「海洋與河流裡的動物,凡有鰭有鱗的,你們都可以吃。 10但海洋與河流裡無鰭無鱗的動物,你們要憎惡。 11牠們都是可憎之物,不可吃牠們的肉,也不可摸牠們的屍體。 12水中任何無鰭無鱗的動物,你們都要視為可憎之物。

13「你們不可吃以下鳥類,要視為可憎之物。牠們是鵰、胡兀鷲、黑禿鷲、 14鳶、隼類、 15烏鴉類、 16駝鳥、夜鷹、海鷗、鷹類、 17小鴞、鸕鷀、大鴞、 18倉鴞、鵜鶘、魚鷹、 19鸛、鷺鳥類、戴鵀和蝙蝠。

20「你們要憎惡會飛會爬的昆蟲, 21但可以吃會飛會跳的昆蟲, 22包括蝗蟲、蟋蟀和蚱蜢。 23所有會飛會爬的昆蟲,你們要視為可憎之物。

24「以下的動物會使你們不潔淨。任何人接觸到牠們的屍體,都不潔淨,要等到傍晚才能潔淨。 25任何人拿牠們的屍體,都必須洗淨所穿的衣服,要等到傍晚才能潔淨。 26蹄子不分瓣或不反芻的動物,你們要視為不潔淨,碰到牠們的人都不潔淨。 27所有以腳掌走路的四足動物,你們要視為不潔淨,碰到牠們屍體的人都不潔淨,要等到傍晚才能潔淨。 28凡拿牠們屍體的人都必須洗淨所穿的衣服,要等到傍晚才能潔淨。你們要視牠們為不潔淨的動物。

29「地上不潔淨的動物有鼬鼠、老鼠、大蜥蜴、 30壁虎、巨蜥、小蜥蜴和變色龍。 31這些爬蟲都是不潔淨的。任何人碰到牠們的屍體,都不潔淨,要等到傍晚才能潔淨。 32如果牠們的屍體掉在什麼東西上,不管是木器、衣物、皮件還是袋子,不管作何用途,都會變得不潔淨。要把那東西放在水中,一直到傍晚才能潔淨。 33如果牠們的屍體掉在陶器裡,陶器裡盛的東西都不潔淨。你們必須打碎那陶器。 34陶器裡的水如果滴到食物上,食物就不潔淨;如果滴到盛飲料的器皿裡,飲料也不潔淨。 35牠們的屍體無論掉在什麼東西上,那東西都不潔淨,無論是爐是鍋都要打碎。 36如果牠們的屍體掉進水泉或儲水池裡,水泉和儲水池仍然是潔淨的,但碰到屍體的人是不潔淨的。 37如果牠們的屍體接觸到將要播撒的種子,種子仍是潔淨的。 38但如果牠們的屍體碰到泡過水的種子,種子就不潔淨。

39「一隻可以食用的動物死後,任何人如果碰到牠的屍體,都不潔淨,要等到傍晚才能潔淨。 40任何人如果吃牠的肉,或拿牠的屍體,都必須洗淨衣服,等到傍晚才能潔淨。

41「所有地上的爬蟲都是可憎的,你們不可吃。 42你們不可吃用肚子、四腳或多腳爬行的動物,這些都是可憎的。 43你們不可讓這些動物玷污自己,使自己不潔淨。 44我是你們的上帝耶和華。你們要分別出來做聖潔的人,因為我是聖潔的。你們不可讓地上的爬蟲玷污自己。 45我是耶和華,我帶你們離開埃及,為要做你們的上帝。你們要聖潔,因為我是聖潔的。

46「以上是有關飛禽走獸、水族和地上一切爬蟲的條例, 47使你們可以分清什麼是潔淨的、什麼是不潔淨的、什麼是可吃的、什麼是不可吃的。」