Walawi 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 10:1-20

Kifo Cha Nadabu Na Abihu

110:1 Kut 6:23; 24:1; 28:1; 30:9; Hes 3:2-4; 16:46; 26:61; 16:7, 18; 1Nya 6:3; 1Fal 7:50; Yer 52:19; 2Fal 25:15; 2Nya 4:22; Eze 8:11; Law 16:12; Isa 6:6Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea Bwana moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu. 210:2 Za 2:12; 50:3; 106:18; Hes 11:1; 16:35; Isa 29:6; Mwa 19:24; 38:7; 1Nya 24:2; Ay 1:16Hivyo moto ukaja kutoka kwa uwepo wa Bwana na kuwaramba, nao wakafa mbele za Bwana. 310:3 Kut 14:4; 19:22; 30:29; Law 21:6; 22:32; Hes 16:5; 20:13; Isa 5:16; 44:23; 49:3; 55:5; 60:21; Eze 28:22; 38:16Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonena Bwana wakati aliposema:

“ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia

nitajionyesha kuwa mtakatifu;

machoni pa watu wote

nitaheshimiwa.’ ”

Aroni akanyamaza.

410:4 Kut 6:18-22; 25:8; Mdo 5:6-10Mose akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjomba wake Aroni, akawaambia, “Njooni hapa. Ondoeni miili ya binamu zenu mbele ya mahali patakatifu, mkaipeleke nje ya kambi.” 510:5 Law 8:13; 10:6; Kut 6:23; Law 13:45; 21:10; Hes 1:53; 5:18; 16:22; 20:29; Yer 41:5; Mk 14:63; Yos 7:1; 22:18; Mwa 50:3, 10; 1Sam 25:1Hivyo wakaja na kuwaondoa, wakiwa bado wamevalia makoti yao ya ibada, wakawapeleka nje ya kambi, kama Mose alivyoamuru.

6Ndipo Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe, Eleazari na Ithamari, “Msifunue vichwa vyenu wala msirarue mavazi yenu, la sivyo mtakufa na Bwana ataikasirikia jumuiya nzima. Lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, wanaweza kuwaombolezea wale ambao Bwana amewaangamiza kwa moto. 710:7 Kut 25:8; 28:41; Law 21:12Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta ya Bwana ya upako yako juu yenu.” Hivyo wakafanya kama vile Mose alivyosema.

8Kisha Bwana akamwambia Aroni, 910:9 Mwa 9:21; Kut 12:14; 29:40; Law 23:13; Hes 6:3; 15:5; 28:7; Kum 14:26; 28:39; 29:6; Isa 5:22; 22:13; 28:1, 7; Yer 35:6; Hos 4:11; Hab 2:15-16; Amu 13:4; Mit 21:1; 23:29-35; 31:4-7; Eze 44:21; Mik 2:11; Lk 1:15; Efe 5:18; 1Tim 3:3; Tit 1:7“Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 1010:10 Mwa 7:2; Law 6:27; 14:57; 20:25; Eze 22:26; 10:11; 2Nya 15:3; 17:7; Ezr 7:25; Neh 8:7; Mal 2:7; Kum 17:10-11; 24:8; 25:1; 33:10; Mit 4:27; Hag 2:11Ni lazima mtenganishe kilicho kitakatifu na kile kilicho cha kawaida, kati ya yaliyo najisi na yaliyo safi, 11na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazo Bwana aliwapa kupitia Mose.”

1210:12 Kut 29:41; Law 6:14-18; 10:13; 6:16; Eze 42:13Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe waliosalia, Eleazari na Ithamari, “Chukueni sadaka ya nafaka iliyobaki kutoka sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, muile hapo kando ya madhabahu ikiwa imeandaliwa bila chachu, kwa sababu ni takatifu sana. 13Mtaila katika mahali patakatifu kwa sababu ni fungu lenu na fungu la wana wenu la sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, kwa maana hivyo ndivyo nilivyoamriwa. 1410:14 Hes 5:9; Kut 29:31; Law 4:12Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila mahali safi pa kawaida ya ibada; mmepewa wewe na watoto wako kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli. 1510:15 Law 7:34; Kut 29:28Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele za Bwana kama sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako la kawaida na wanao, kama Bwana alivyoagiza.”

1610:16 Law 9:3Mose alipouliza kuhusu mbuzi atolewaye kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kukuta kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliobaki, akawauliza, 1710:17 Law 6:24-30; Eze 42:13; Kut 28:38“Kwa nini hamkula sadaka ya dhambi katika eneo la mahali patakatifu? Ni takatifu sana. Mlipewa ninyi ili kuondoa hatia ya jumuiya kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho mbele za Bwana. 1810:18 Law 4:18; 6:17, 26, 30Kwa kuwa damu yake haikuletwa ndani ya Mahali Patakatifu, mngemla mbuzi huyo katika sehemu ya mahali patakatifu kama nilivyoagiza.”

1910:19 Law 9:12; Yer 6:20; 14:12; Hos 9:4; Mal 1:10Aroni akamjibu Mose, “Leo wanangu wametoa sadaka zao za dhambi na sadaka zao za kuteketezwa mbele za Bwana, lakini mambo kama haya yamenitokea mimi. Je, Bwana angependezwa kama ningekuwa nimekula sadaka ya dhambi leo?” 20Mose aliposikia haya, akaridhika.