Wakolosai 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wakolosai 3:1-25

Kanuni Za Kuishi Maisha Matakatifu

13:1 Rum 6:5; Mk 16:19Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo alikoketi mkono wa kuume wa Mungu. 23:2 Flp 3:19, 20Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani. 33:3 Rum 6:2; 2Kor 5:14Kwa maana ninyi mlikufa, nao uhai wenu sasa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 43:4 1Kor 1:7; 1Pet 1:13; 1Yn 3:2; Gal 2:20; 1Kor 1:7; 1Pet 1:13; Yn 3:2Wakati Kristo, aliye uzima wenu, atakapotokea, ndipo nanyi mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.

53:5 Efe 5:3-5; Rum 6:2; Efe 4:22; Gal 5:24; 1Kor 6:18; Efe 5:3; Gal 5:19-21Kwa hiyo, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambayo ndiyo ibada ya sanamu. 63:6 Rum 1:18Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. 73:7 Efe 2:2Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo. 83:8 Efe 4:22-31Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. 93:9 Efe 4:22-25Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, 103:10 Rum 1:22; 2Kor 4:16; Efe 2:10nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake. 113:11 Rum 10:12; 1Kor 7:19; Gal 3:28; Efe 1:23Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote, na ndani ya wote.

123:12 Flp 2:3; 2Kor 6:6; Gal 5:22, 23; Efe 4:2Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 133:13 Efe 4:2, 32; 4:32Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. 143:14 1Kor 13:1-13; Efe 4:3Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.

153:15 Yn 14:27Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. 163:16 Rum 10:17; Kol 1:28; Efe 5:19Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. 173:17 Efe 5:20-22Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.

Kanuni Katika Madaraka Ya Nyumbani

18Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana.

193:19 Efe 5:25, 28, 33; 1Pet 3:7; Efe 4:31Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.

203:20 Efe 6:1; 5:24; Tit 2:9Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.

213:21 Efe 6:4Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

223:22 Efe 6:5; 1Tim 6:1; Tit 2:9; 1Pet 2:18Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana. 233:23 Efe 6:6, 7Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, 243:24 Mdo 20:32kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia. 253:25 Mdo 10:34Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.