Wagalatia 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wagalatia 6:1-18

Chukulianeni Mizigo

16:1 1Kor 2:15; Rum 14:1; 15:1; Ebr 12:13; Yak 5:19; 1Kor 2:15; 3:1; 4:21; 2The 3:15; 1Kor 7:5Ndugu zangu, ikiwa mtu ameghafilika akatenda dhambi, basi ninyi mlio wa rohoni, mrejesheni upya mtu huyo kwa roho ya upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa. 26:2 Rum 15:1; 1Kor 9:21; Rum 15:1; Gal 5:13; 1The 5:14; Yn 13:14, 15, 34; 15:12; Yak 2:8Chukulianeni mizigo ninyi kwa ninyi, nanyi kwa njia hii mtatimiza sheria ya Kristo. 36:3 Rum 12:3; 1Kor 8:2; Rum 12:3; 1Kor 8:2; Gal 2:6; 2Kor 3:5; 12:11Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. 46:4 1Kor 11:28; 2Kor 13:5; Lk 18:11Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo aweze kujisifu, bila kujilinganisha na mtu mwingine. 56:5 Rum 2:6; 1Kor 3:8Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe. 66:6 1Kor 9:11, 14; Rum 15:27; 1Kor 9:11, 14Basi, yeye afundishwaye katika neno na amshirikishe mwalimu wake mema yote.

76:7 1Kor 6:9; 2Kor 9:6; 1Kor 15:33; Ay 13:9; Lk 16:25; Rum 2:6Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. 86:8 Hos 8:7; Rum 6:23; Yn 3:18; Ay 4:8; Mit 11:18; 22:8; Hos 8:7; 10:12; Rum 8:13; Yak 3:18Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 96:9 1Kor 15:58; Za 126:5; 2Kor 4:1; Ay 42:12; Ebr 12:3; Ufu 2:10Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa. 10Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waaminio.

Si Kutahiriwa Bali Kuwa Kiumbe Kipya

11Angalieni herufi kubwa nitumiazo ninapowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe!

12Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili wanataka wawalazimishe kutahiriwa. Sababu pekee ya kufanya hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo. 13Hata wale waliotahiriwa wenyewe hawaitii sheria, lakini wanataka ninyi mtahiriwe ili wapate kujivuna kwa habari ya miili yenu. 14Mungu apishie mbali nisije nikajivunia kitu chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu. 15Kwa maana katika Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu, bali kule kuwa kiumbe kipya ni kila kitu! 16Amani na rehema viwe na wote wanaofuata kanuni hii, na juu ya Israeli wa Mungu.

17Hatimaye, tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, kwa maana nachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu.

18Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.