Wagalatia 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wagalatia 4:1-31

1Lile nisemalo ni kwamba wakati wote mrithi bado ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ndiye mmiliki wa mali yote. 2Yeye huwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 34:3 Gal 4:9; 5:1; Kol 2:8, 20; Ebr 9:10Vivyo hivyo na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa utumwani chini ya taratibu za kawaida za ulimwengu. 44:4 Mk 1:15; Rum 5:6; Efe 1:10; Yn 3:17; 1:14; Lk 2:27Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe, ambaye alizaliwa na mwanamke, akazaliwa chini ya sheria, 54:5 Rum 3:24; Yn 1:12; Rum 8:14kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, ili tupate kupokea zile haki kamili za kufanywa watoto wa Mungu. 64:6 Mdo 16:7; Rum 5:5; 8:15, 16Kwa sababu ninyi ni watoto wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, anayelia, “Abba,4:6 Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba; lingeweza kutumiwa tu na mtoto wa kuzaa. Baba.” 74:7 Rum 8:17; Gal 3:29Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mtoto, kwa kuwa wewe ni mtoto, Mungu amekufanya wewe pia kuwa mrithi kwa kupitia Kristo.

Paulo Awashawishi Wagalatia

84:8 Rum 1:28; 1Kor 1:21; 15:34; 1The 4:5; 2The 1:8; Gal 4:3Zamani, mlipokuwa hammjui Mungu, mlikuwa watumwa wa viumbe ambavyo kwa asili si Mungu. 94:9 1Kor 8:3; Gal 4:3; Kol 2:20Lakini sasa kwa kuwa mmemjua Mungu, au zaidi mmejulikana na Mungu, inakuwaje mnarejea tena katika zile kanuni za kwanza zenye udhaifu na upungufu? Mnataka ziwafanye tena watumwa? 104:10 Rum 14:5; Kol 2:16Mnaadhimisha siku maalum, miezi, nyakati na miaka! 114:11 1The 3:5; Gal 2:2; 5:2, 4Nina hofu juu yenu, kwamba kazi niliyofanya kwa ajili yenu inaweza kuwa nimejitaabisha bure.

124:12 Rum 7:1; Gal 6:18; 2Kor 2:5Ndugu zangu, nawasihi mwe kama mimi, kwa sababu mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea jambo lolote baya. 134:13 1Kor 2:3; 2Kor 11:30; 12:7, 9; Gal 1:6Ninyi mwajua kwamba ni kwa ajili ya udhaifu wangu niliwahubiria Injili. 144:14 Mt 10:40; 2Sam 19:27; Mal 2:7; Zek 12:8; Mt 10:40; Lk 10:16Ingawa hali yangu iliwatia majaribuni, hamkunidharau wala kunidhihaki, bali mlinikaribisha kama malaika wa Mungu, kama vile Kristo Yesu. 15Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imekwenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngengʼoa macho yenu na kunipa mimi. 164:16 Gal 2:5, 14; Amo 5:10Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa kuwaambia kweli?

174:17 Gal 2:4, 12; Rum 10:12; 1Kor 11:2Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku. 184:18 Gal 4:13, 14Ni vizuri wakati wote kuwa na shauku kwa ajili ya kusudi zuri, si wakati nikiwa pamoja nanyi tu. 194:19 1The 2:11; Rum 8:29; Efe 4:13Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara nyingine ninawaonea utungu, ninatamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20Natamani kama ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha sauti yangu. Kwa maana nina wasiwasi kwa ajili yenu.

Mfano Wa Hagari Na Sara

214:21 Rum 2:12Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je, hamjui sheria inavyosema? 22Kwa maana imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wawili, mmoja wa mwanamke mtumwa na wa pili wa mwanamke huru. 234:23 Gal 4:28, 29; Rum 9:7, 8; Mwa 17:16-21; 18:10-14; 4:24Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili, na yule mwingine wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu.

24Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika Mlima Sinai, lizaalo watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hagari. 25Basi Hagari anawakilisha Mlima Sinai ulioko Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 264:26 Flp 2:3; Ebr 12:22; Isa 2:2; Ufu 3:12; 21:2, 10Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. 274:27 Isa 54:1Kwa maana imeandikwa:

“Furahi, ewe mwanamke tasa,

wewe usiyezaa;

paza sauti, na kuimba kwa furaha,

wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa;

kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi

kuliko wa mwanamke mwenye mume.”

284:28 Mdo 3:25; Rum 9:8; Gal 3:29Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 294:29 Mwa 21:9; Gal 5:11; 6:12Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 304:30 Mwa 21:10Lakini Maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.” 314:31 Rum 7:4; Gal 4:22Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali wa yule aliye huru.