Wagalatia 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wagalatia 1:1-24

Salamu

11:1 Mdo 9:15; 20:24; 1Kor 1:1Paulo mtume: si mtume wa wanadamu wala aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu; 21:2 Flp 4:21; Mdo 16:6; 1Kor 16:1na ndugu wote walio pamoja nami:

Kwa makanisa ya Galatia:

31:3 Rum 1:7; 1Kor 1:3; 2Kor 1:2; Efe 1:2; Flp 1:2; Kol 1:2; 1The 1:1Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo, 41:4 Rum 4:25; 1Kor 15:3; Flp 4:20aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu. 51:5 Rum 11:36Utukufu una yeye milele na milele. Amen.

Hakuna Injili Nyingine

61:6 Gal 5:8; 2Kor 11:4Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata Injili nyingine, 71:7 Mdo 15:24; Gal 5:10ambayo kwa kweli si Injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo. 81:8 2Kor 11:4; Rum 9:3Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele! 91:9 Rum 16:17; Kum 4:2; 12:32; Mit 30:6; Ufu 22:18Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!

101:10 1The 2:4; 1Sam 24:7; Mt 28:14; 1Yn 3:9; 1The 2:4Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo.

Paulo Ameitwa Na Mungu

111:11 1Kor 15:1Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu. 121:12 1Kor 15:1, 3; Gal 1:1; Efe 3:3Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.

131:13 Mdo 26:4, 5; 8:3Ninyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kwa nguvu na kujaribu kuliangamiza. 141:14 Mt 15:2Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu. 151:15 Isa 49:1, 5; Mdo 9:15Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake, 161:16 Gal 2:9; Mt 16:17alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote, 171:17 Mdo 9:2, 19-22wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.

181:18 Mdo 9:22, 23; 9:26, 27Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa1:18 Yaani Petro. na nilikaa naye siku kumi na tano. 191:19 Mt 13:55Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 201:20 Rum 9:1; 1:9Nawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo. 211:21 Mdo 6:9; 9:30Baadaye nilikwenda sehemu za Syria1:21 Syria hapa ina maana ya Shamu. na Kilikia. 221:22 1The 2:14; Rum 16:3Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Uyahudi yaliyo katika Kristo. 231:23 Mdo 6:7; 8:3Wao walisikia habari tu kwamba, “Mtu yule ambaye hapo kwanza alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akijaribu kuiangamiza.” 241:24 Mt 9:8Nao wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.