Wafilipi 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Wafilipi 2:1-30

Kuiga Unyenyekevu Wa Kristo

12:1 2Kor 13:14; Kol 3:12Kama kukiwa na jambo lolote la kutia moyo katika kuunganishwa na Kristo, kukiwa faraja yoyote katika upendo wake, kukiwa na ushirika wowote na Roho, kukiwa na wema wowote na huruma, 22:2 Yn 3:29; Flp 4:2; Rum 12:16; 15:15basi ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, mkiwa na upendo huo moja, mkiwa wa roho na kusudi moja. 32:3 Gal 5:26; Rum 12:10; 1Pet 5:5Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake. 42:4 1Kor 10:24, 33; 13:5Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.

52:5 Mt 11:29; Yn 13:15; 1Pet 2:21; 1Yn 2:6Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu:

62:6 Yn 1:1; 5:18Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa,

hakuona kule kuwa sawa na Mungu

kuwa kitu cha kushikilia,

72:7 Mt 20:28; Rum 8:3; Ebr 5:8bali alijifanya si kitu,

akachukua hali hasa na mtumwa,

naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

82:8 Rum 5:19; Ebr 5:8Naye akiwa na umbo la mwanadamu,

alijinyenyekeza, akatii hata mauti:

naam, mauti ya msalaba!

92:9 Dan 7:14; Mdo 2:33; Efe 1:20Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana,

na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina,

102:10 Rum 14:11; Efe 1:10ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe,

la vitu vya mbinguni, na vya duniani,

na vya chini ya nchi,

112:11 Yn 13:13; Mdo 2:36; Rum 14:9; 1Kor 8:6; 12:3na kila ulimi ukiri ya kwamba

Yesu Kristo ni Bwana,

kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ngʼaeni Kama Mianga Katika Ulimwengu

122:12 2Kor 7:15; 1Pet 1:17; Za 2:11Kwa hiyo, wapenzi wangu, kama vile ambavyo mmekuwa mkitii siku zote, si tu wakati nikiwa pamoja nanyi, bali sasa zaidi sana nisipokuwepo, utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka, 132:13 Ezr 1:5; Yn 15:5; 2Kor 3:5; 1The 2:11kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi lake jema.

142:14 1Kor 10:10; 1Pet 4:9Fanyeni mambo yote bila kunungʼunika wala kushindana, 152:15 Mt 5:45, 48; Efe 5:1; Mdo 2:40ili msiwe na lawama wala hatia, bali mwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika kizazi chenye ukaidi na kilichopotoka, ambacho ndani yake ninyi mnangʼaa kama mianga ulimwenguni. 162:16 1The 2:19Mkilishika neno la uzima, ili nipate kuona fahari siku ya Kristo kwamba sikupiga mbio wala kujitaabisha bure. 172:17 2Tim 4:6; Rum 15:16Lakini hata kama nikimiminwa kama sadaka ya kinywaji kwenye dhabihu na huduma itokayo katika imani yenu, mimi ninafurahi na kushangilia pamoja nanyi nyote. 182:18 Flp 3:1; 4:4Vivyo hivyo, ninyi nanyi imewapasa kufurahi na kushangilia pamoja nami.

Paulo Amsifu Timotheo

192:19 Mdo 16:1; Flp 2:23Natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate kufarijika moyo nitakapopata habari zenu. 202:20 1Kor 16:10Sina mtu mwingine kama yeye, ambaye ataangalia hali yenu kwa halisi. 212:21 1Kor 10:24; 13:5Kwa maana kila mmoja anajishughulisha zaidi na mambo yake mwenyewe wala si yale ya Yesu Kristo. 222:22 1Kor 4:17; 1Tim 1:2Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana ametumika pamoja nami kwa kazi ya Injili, kama vile mwana kwa baba yake. 232:23 Flp 2:19Kwa hiyo, ninatumaini kumtuma kwenu upesi mara nitakapojua mambo yangu yatakavyokuwa. 242:24 Flp 1:25Nami mwenyewe ninatumaini katika Bwana kwamba nitakuja kwenu hivi karibuni.

Paulo Amsifu Epafrodito

252:25 Flp 1:1Lakini nadhani ni muhimu kumtuma tena kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mtendakazi pamoja nami, aliye askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma ili ashughulike na mahitaji yangu. 262:26 Flp 1:8Kwa maana amekuwa akiwaonea sana shauku ninyi nyote, akiwa na wasiwasi kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa. 27Kweli alikuwa mgonjwa, tena karibu ya kufa. Lakini Mungu alimhurumia, wala si yeye tu, bali hata na mimi alinihurumia, nisipatwe na huzuni juu ya huzuni. 282:28 Flp 2:25Kwa hiyo mimi ninafanya bidii kumtuma kwenu ili mtakapomwona kwa mara nyingine, mpate kufurahi, nami wasiwasi wangu upungue. 292:29 1Kor 16:18; 1Tim 5:17Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana kwa furaha kubwa, nanyi wapeni heshima watu kama hawa, 302:30 1Kor 16:17kwa sababu alikaribia kufa kwa ajili ya kazi ya Kristo, akihatarisha maisha yake ili aweze kunihudumia vile ninyi hamkuweza.