Waefeso 6 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Waefeso 6:1-24

Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi

16:1 Kol 3:20; Mt 6:20Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. 26:2 Kut 20:12; Kum 5:16; 27:16; Yer 35:18; Eze 22:7; Mal 1:6; Mt 15:4; Mk 7:10“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 36:3 Kut 20; 12; Kum 5:16“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”

46:4 Kol 3:21; Mit 13:24; 22:6Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

Mafundisho Kuhusu Watumwa Na Mabwana

56:5 Tit 2:9; Kol 3:22; Efe 5:22Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo. 66:6 Rum 6:22; Kol 3:22, 23Watiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 76:7 Kol 3:23Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu. 86:8 Kol 3:24Mkijua kwamba Bwana atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.

96:9 Ay 31:13, 14Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

Silaha Za Mungu

106:10 Hag 2:4; Efe 1:19Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 116:11 Rum 13:12Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 126:12 Efe 1:21; Rum 8:38; Efe 1:3Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 136:13 Efe 6:11; 2Kor 6:7; 10:4, 11; Efe 5:16Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 146:14 Isa 1:5; Za 132:9Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 156:15 Isa 52:7; Rum 10:15nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 166:16 1Yn 5:4; Mt 5:37Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 176:17 Isa 59:17; Ebr 4:12Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. 186:18 Lk 18:1; Mt 26:41; Flp 4:6Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

196:19 1The 5:25; Mdo 4:29; 2Kor 3:12Niombeeni na mimi pia, ili kila nifunguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri, 206:20 2Kor 5:20; Mdo 21:23ambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni ili nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo.

Salamu Za Mwisho

216:21 Mdo 20:4Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa. 226:22 Kol 4:7-9Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali yetu, na awatie moyo.

236:23 Gal 6:16; 1Pet 5:14Amani iwe kwa ndugu, na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. 246:24 Tit 2:7; 1Pet 1:8Neema iwe na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo wa dhati. Amen.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以弗所书 6:1-24

父慈子孝

1你们做儿女的,要按主的旨意听从父母,这是理所当然的。 2因为第一条带着应许的诫命就是:“要孝敬父母, 3使你在世上蒙福、长寿。”6:3 申命记5:16 4你们做父亲的,不要激怒儿女,要照主的教导和警戒养育他们。

主仆之间

5你们做奴仆的,要战战兢兢、诚诚实实、怀着敬畏的心服从你们世上的主人,就像服从基督一样。 6不要只做讨好人的表面工夫,要像基督的奴仆一样从心里遵行上帝的旨意。 7要甘心乐意地工作,像是在事奉主,不是在服侍人。 8要知道:不管是奴仆还是自由人,每个人所做的善事都会得到主的奖赏。 9你们做主人的也一样,要善待奴仆,不可威吓他们。要知道你们主仆同有一位在天上的主人,祂不偏待人。

上帝所赐的军装

10最后,你们要靠着主和祂的大能大力做刚强的人, 11要穿戴上帝所赐的全副军装,以便能够抵挡魔鬼的阴谋。 12因为我们争战的对象不是这世上的血肉之躯,而是在这黑暗世界执政的、掌权的、管辖的和天上属灵的邪恶势力。 13因此,你们要用上帝所赐的全副军装装备自己,好在邪恶的时代抵挡仇敌,到争战结束后仍然昂首挺立。 14务要站稳,用真理当作带子束腰,以公义当作护心镜遮胸, 15把和平的福音当鞋穿在脚上准备行动。 16此外,还要拿起信心的盾牌,好灭尽恶者一切的火箭。 17要戴上救恩的头盔,紧握圣灵的宝剑——上帝的话。 18要靠着圣灵随时多方祷告和祈求,警醒不怠地为众圣徒祷告。 19也请你们为我祷告,求上帝赐我口才,让我勇敢地把福音的奥秘讲解明白。 20我为传福音成了带锁链的使者。请你们为我祷告,使我能尽忠职守,放胆传福音。

问候

21推基古会把我的近况全部告诉你们,好让你们也了解我的处境。他是主内亲爱的弟兄和忠心的仆人。 22我特意派他去你们那里,好让你们知道我们的近况,并且心受鼓舞。

23愿父上帝和主耶稣基督赐给各位弟兄姊妹平安、爱心和信心! 24愿所有忠贞地爱我们主耶稣基督的人都蒙恩典!