Waefeso 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waefeso 4:1-32

Umoja Katika Mwili Wa Kristo

14:1 Efe 3:1; Kol 1:10; 1The 2:12Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa. 24:2 Kol 3:12, 13; Efe 1:4Kwa unyenyekevu wote na upole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo. 34:3 Kol 3:14; Rum 15:5Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 44:4 1Kor 12:13Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. 54:5 1Kor 8:6; 2Kor 11:4; Yud 3; Gal 3:27, 28; Ebr 6:6Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 64:6 Rum 11:36; 1Kor 12:6; Mal 2:10; 1Kor 8:6; 12:6; Rum 11:36Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.

74:7 1Kor 12:7, 11; Rum 12:3Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo. 84:8 Kol 2:15; Za 68:18Kwa hiyo husema:

“Alipopaa juu zaidi, 4:8 Juu zaidi hapa ina maana mbingu za mbingu.

aliteka mateka,

akawapa wanadamu vipawa.”

94:9 Yn 3:13; 6:33, 62(Asemapo “alipaa juu,” maana yake nini isipokuwa ni kusema pia kwamba Kristo alishuka pande za chini sana za dunia?4:9 Pande za chini sana za dunia hapa maana yake Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu. 104:10 Mdo 1:9, 11; 1Tim 3:16; Ebr 4:14; 7:26; 9:24; Mdo 2:13; Mit 30:1-4; Efe 1:23Yeye aliyeshuka ndiye alipaa juu zaidi kupita mbingu zote, ili apate kuujaza ulimwengu wote.) 114:11 2Pet 3:2; Mdo 21:8Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, 124:12 1Kor 12:27; 1Pet 2:5; 2Tim 3:17kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa 134:13 Kol 1:28mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Kristo.

144:14 1Kor 14:20; Yn 1:6; Efe 6:11Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu. 154:15 Efe 1:22Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani, Kristo. 164:16 Kol 2:19Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikamanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake.

Maisha Ya Zamani Na Maisha Mapya

174:17 Rum 1:21Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 184:18 Rum 1:21; Efe 2:12; 2Kor 3:14Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 194:19 1Tim 4:2; Rum 1:24; Kol 3:5Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

20Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo. 214:21 Efe 1:13Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 224:22 1Pet 2:1; Rum 6:6Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, 234:23 Kol 3:10ili mfanywe upya roho na nia zenu, 244:24 Rum 6:4; Efe 2:10mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

Kanuni Za Maisha Mapya

254:25 Law 19:11; Rum 12:15Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja. 264:26 Za 4:4; Yak 1:19, 20; Mt 5:22Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, 274:27 Yak 4:7; 1Pet 5:9wala msimpe ibilisi nafasi. 284:28 Mdo 20:35; 1The 4:11; Lk 3:11Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kifaacho kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji.

294:29 Kol 3:8; Mt 12:36; Efe 5:4; Kol 3:8; 4:6; 1The 5:11Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao. 304:30 1The 5:19; Rum 8:23Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 314:31 Kol 3:8; Tit 3:2; Yak 4:11; 1Pet 2:1; Tit 3:3Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. 324:32 Mt 6:14, 15Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.