Waebrania 9 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Waebrania 9:1-28

Ibada Katika Hema La Kidunia

19:1 Kut 25:8Basi agano lile la kwanza lilikuwa na kanuni zake za kuabudu na pia patakatifu pake pa kidunia. 29:2 Kut 26:1; 26:35; 40:4; 25:31; 25:23; Law 24:5Hema ilitengenezwa. Katika sehemu yake ya kwanza kulikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa wakfu; hii sehemu iliitwa Mahali Patakatifu. 39:3 Kut 26:31, 33; 40:3, 21; Ebr 6:19Nyuma ya pazia la pili, palikuwa na sehemu iliyoitwa Patakatifu pa Patakatifu, 49:4 Kut 30:1-5; 25:10-22; 16:32, 33; Hes 17:10; Kut 31:18; 32:15ambapo palikuwa na yale madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba, na lile Sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu. Sanduku hili lilikuwa na gudulia la dhahabu lenye mana, ile fimbo ya Aroni iliyochipuka, na vile vibao vya mawe vya Agano. 59:5 Kut 25:17-19; 25:20-22; 26:34Juu ya lile Sanduku kulikuwa na makerubi ya Utukufu yakitilia kivuli kile kifuniko ambacho ndicho kiti cha rehema. Lakini hatuwezi kueleza vitu hivi kwa undani sasa.

69:6 Hes 28:3Basi vitu hivi vilipokuwa vimepangwa, makuhani waliingia daima katika sehemu ya kwanza ya hema ili kufanya taratibu zao za ibada. 79:7 Law 16:11-19; Ebr 9:2, 3; Law 16:34Lakini ni kuhani mkuu peke yake aliyeingia ndani ya sehemu ya pili ya hema. Tena hii ilikuwa mara moja tu kwa mwaka, na hakuingia kamwe bila damu, ambayo alitoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda bila kukusudia. 89:8 Ebr 3:7; Yn 14:6; Ebr 10:19, 20Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa anaonyesha kwamba, maadamu ile hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia Patakatifu pa Patakafifu ilikuwa bado haijafunguliwa. 99:9 Ebr 10:1; 5:1; 8:3; 7:19Huu ulikuwa mfano kwa ajili ya wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizokuwa zikitolewa hazikuweza kusafisha dhamiri ya mtu anayeabudu. 109:10 Law 11:2-23; Hes 6:3; Kol 2:16; Law 11:25, 28, 40; Ebr 7:16Lakini hizi zilishughulika tu na vyakula na vinywaji, pamoja na taratibu mbalimbali za kunawa kwa nje, kanuni kwa ajili ya mwili zilizowekwa hadi wakati utimie wa matengenezo mapya.

Damu Ya Kristo

119:11 Ebr 2:17; 10:1; 9:24; 8:2; Yn 2:19Kristo alipokuja akiwa Kuhani Mkuu wa mambo mema ambayo tayari yameshawasili, alipitia kwenye hema iliyo kuu zaidi na bora zaidi, ambayo haikutengenezwa kwa mikono ya binadamu, hii ni kusema, ambayo si sehemu ya uumbaji huu. 129:12 Ebr 9:19; Law 16:6, 15; Ebr 10:4; 9:24, 26, 28; Rum 3:25Hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama; lakini aliingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele. 139:13 Ebr 10:4; Hes 19:9, 17, 18Damu ya mbuzi na ya mafahali, na majivu ya mitamba walivyonyunyiziwa wale waliokuwa najisi kwa taratibu za kiibada viliwatakasa, hata kuwaondolea uchafu wa nje. 149:14 1Pet 3:18; Efe 5:2; Za 51:2; 65:3; Yer 33:8; Zek 13:1; Tit 2:14; Mt 16:16Basi ni zaidi aje damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa, itatusafisha dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo mauti, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai!

159:15 Gal 3:20; Lk 22:20; Rum 8:28; 11:29; Ebr 6:15; 7:22; Mdo 20:32Kwa sababu hii Kristo ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.

16Kwa habari ya wosia,9:16 Wosia hapa kwa neno la Kiyunani ni agano. ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa, 179:17 Gal 3:15kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai. 189:18 Kut 24:6-8Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. 199:19 Kut 24:5, 6, 8; Law 16:14, 15, 18; 14:4, 6, 7, 49, 51, 52Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote. 209:20 Kut 24:8; Mt 26; 28Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 219:21 Kut 29:12, 36; Law 8:15, 19; 16:1, 15, 16, 18, 19Vivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada. 229:22 Law 17:11; Kut 29:21; Law 8:15Kwa kweli sheria hudai kwamba, karibu kila kitu kitakaswe kwa damu, wala pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.

239:23 Ebr 8:5Kwa hiyo, ilikuwa muhimu kwa nakala za vitu vile vya mbinguni vitakaswe kwa dhabihu hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi. 249:24 Ebr 6:20; 8:2; Rum 8:34; Ebr 7:25; 1Yn 2:1Kwa maana Kristo hakuingia kwenye patakatifu palipofanywa kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele za Mungu kwa ajili yetu. 259:25 Ebr 9:7; 10:19Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe. 269:26 Ebr 9:12; 7:27; 10:10; 1Pet 3:18; 1Kor 10:11; Gal 4:4; Efe 1:10Ingekuwa hivyo, ingempasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. 279:27 Mwa 3:19; Mhu 3:20; 2Kor 5:10; Ufu 20:12, 13Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu, 289:28 Rum 6:10; 1Pet 3:18; 2:24; 1Yn 3:5; Mt 26:28; Rum 5:15; Tit 2:13vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

希伯來書 9:1-28

舊約敬拜的禮儀

1第一個約有敬拜的禮儀和地上的聖幕。 2建成後的聖幕共分兩間,外面的一間稱為聖所,裡面擺設了燈臺、桌子和供餅。 3第二道幔子後面的那一間叫至聖所, 4裡面有金香壇和包金的約櫃。約櫃裡珍藏著盛嗎哪的金罐、亞倫那根發過芽的手杖和兩塊約版, 5約櫃上面有榮耀的基路伯天使,高展翅膀遮蓋著施恩座。關於這些事,現在不能一一細說。

6這些東西都齊備了,祭司們便經常進入聖所,舉行敬拜。 7可是,只有大祭司有資格每年一次獨自進入至聖所,而且每次都要端著血進去,為自己獻上,也為以色列人的無心之過獻上。 8聖靈藉此指明,只要第一個聖幕還在,進入至聖所的路就還沒有打開。 9這件事是一個象徵,告訴現今的世代:所獻的禮物和祭物都不能使敬拜的人良心純全, 10因為這些不過是關於飲食和各種潔淨禮儀的外在規條,等新秩序的時代一到,便不再有效了。

美好新約

11現在基督已經來到,作了美好新約的大祭司,祂進入了那更偉大、更全備、非人手建造、不屬於這個世界的聖幕。 12祂只進入至聖所一次便完成了永遠的救贖,用的不是山羊和牛犢的血,而是自己的血。 13如果把山羊血、公牛血和母牛犢的灰灑在污穢的人9·13 「污穢的人」指在猶太人的宗教禮儀上被視為不潔淨的人。身上,都可以使他們聖潔,身體得到潔淨, 14更何況基督藉著永恆的靈把自己毫無瑕疵地獻給上帝呢?祂的血豈不更能洗淨我們的良心,使我們脫離導致滅亡的行為,以便事奉永活的上帝嗎?

15因此,基督是新約的中保,祂的死亡救贖了那些蒙召的人在第一個約下面所犯的罪,好叫他們得到上帝應許的永恆基業。

16要執行任何遺囑9·16 希臘文的「遺囑」和「約」是同一個字。,必須證實立遺囑的人已經死亡, 17因為只有人死以後遺囑才能生效。只要立遺囑的人還健在,遺囑就不能生效。 18正因如此,連立第一個約也需要用血才能生效。 19摩西依照律法向以色列人頒佈所有誡命之後,便用紅色的羊毛和牛膝草蘸了牛犢和山羊的血以及水,灑在律法書和百姓身上, 20說:「這是上帝用來與你們立約的血。」9·20 出埃及記24·8 21他又照樣把血灑在聖幕和所有敬拜用的器具上。 22根據律法,幾乎所有的器具都要用血來潔淨,因為若不流血,罪就得不到赦免。

23既然仿照天上樣式造的器具需要用這些祭牲的血來潔淨,天上的原物當然要用更美的祭物來潔淨。 24因為基督並非進入了人手所造的聖所,那只是真聖所的縮影,祂是進到了天上,替我們來到上帝面前。 25祂在天上不必一次又一次地把自己獻上,好像那些大祭司年年都帶著牛羊的血進入至聖所。 26否則,自創世以來,祂不知道要受難多少次了。但如今在這世代的末期,祂只一次獻上自己,便除去了人的罪。 27按著定命,人人都有一死,死後還有審判。 28同樣,基督為了承擔世人的罪,也曾一次獻上自己。祂還要再來,不是來除罪,而是來拯救那些熱切等候祂的人。