Waebrania 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waebrania 8:1-13

Kuhani Mkuu Wa Agano Jipya

18:1 Ebr 2:17; Mk 16:19; Ebr 4:14; Efe 1:20; Kol 3:1Basi jambo tunalotaka kulisema ni hili: Tunaye Kuhani Mkuu ambaye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Aliye Mkuu mbinguni, 28:2 Ebr 9:11, 24; 9:8, 12, 24yeye ahudumuye katika patakatifu, hema la kweli lililowekwa na Bwana, wala si na mwanadamu.

38:3 Ebr 2:17; 5:1; 9:9, 14; Efe 5:2Kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe sadaka na dhabihu. Vivyo hivyo, ilikuwa jambo muhimu kwa huyu Kuhani naye awe na kitu cha kutoa. 48:4 Ebr 5:1; 9:9Kama angekuwa duniani, hangekuwa kuhani, kwa sababu tayari wapo watu watoao sadaka kama ilivyoelekezwa na sheria. 58:5 Ebr 9:23; 10:1; 11:7; 12:25; Kol 2:17; Kut 25:40Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Mose alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano ulioonyeshwa kule mlimani.” 68:6 Ebr 8:8, 13; Lk 22:20; Gal 3:20; 2Kor 3:6, 8, 9Lakini huduma aliyopewa Yesu ni bora zaidi kuliko yao, kama vile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani, nalo limewekwa misingi wa ahadi zilizo bora zaidi.

78:7 Ebr 7:11, 18; 10:1Kwa maana kama hapakuwa na kasoro katika lile agano la kwanza, pasingekuwa na haja ya kutafuta nafasi kwa ajili ya jingine. 88:8 Yer 31:31, 32, 33, 34; Ebr 10:16, 17Lakini Mungu aliona kosa kwa watu, naye akasema:

“Siku zinakuja, asema Bwana,

nitakapofanya agano jipya

na nyumba ya Israeli

na nyumba ya Yuda.

98:9 Kut 19:5-6; 20:1-17Agano langu halitakuwa kama lile

nililofanya na baba zao

nilipowashika mkono

kuwaongoza watoke nchi ya Misri,

kwa sababu hawakuendelea kuwa waaminifu katika agano langu,

nami nikawaacha,

asema Bwana.

108:10 Rum 11:27; 2Kor 3:3; Ebr 10:16; Eze 11:20; Zek 8:8Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli

baada ya siku zile, asema Bwana.

Nitaziweka sheria zangu katika nia zao

na kuziandika mioyoni mwao.

Nitakuwa Mungu wao,

nao watakuwa watu wangu.

118:11 Isa 54:13; Yn 6:45Mtu hatamfundisha tena jirani yake,

wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana,’

kwa sababu wote watanijua mimi,

tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana.

128:12 Ebr 10:17; Yer 31:31-34Kwa sababu nitasamehe uovu wao,

wala sitazikumbuka dhambi zao tena!”

138:13 Ebr 8:6, 8; Lk 22:20; 2Kor 5:17; Rum 10:4Kwa kuliita agano hili “jipya,” Mungu amefanya lile agano la kwanza kuwa kuukuu; nacho kitu kinachoanza kuchakaa na kuwa kikuukuu kiko karibu kutoweka.