Waebrania 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waebrania 6:1-20

Hatari Ya Kuanguka

16:1 Flp 3:12, 13, 14; Ebr 5:12; 9:14Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tukisonga mbele ili tufikie utimilifu, sio kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, 26:2 Yn 3:25; Mdo 6:6; 2:24; 17:18, 22mafundisho kuhusu aina za ubatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. 36:3 Mdo 18:21; 1Kor 4:19Mungu akitujalia tutafanya hivyo.

46:4 Ebr 10:22; Efe 2:8; Gal 3:2; Mt 12:31, 32; 2Pet 2:20, 21; 1Yn 5:16; Yn 4:10; 6:32Kwa kuwa ni vigumu kwa wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu, 56:5 Ebr 2:5; 4:12; Za 34:8ambao wameonja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, 66:6 2Pet 2:21; 1Yn 5:16; Mt 4:3; Ebr 10:29kisha wakianguka, kuwarejesha tena katika toba. Kwa kuwa wanamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili na kumdhalilisha hadharani, nayo ikawa hasara kwao.

76:7 Za 65:10; Mwa 1:11, 12Ardhi ile ipokeayo mvua inyeshayo juu yake mara kwa mara hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao kwa ajili yao yalimwa, nayo nchi hiyo hupokea baraka kutoka kwa Mungu. 86:8 Mwa 3:17, 18; Isa 5:6; 27:4Lakini ardhi ikizaa miiba na mibaruti, haina thamani na iko hatarini ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuchomwa moto.

96:9 1Kor 10:14Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu. 106:10 Mt 10:40, 42; 1The 1:3Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia. 116:11 Ebr 3:6, 14; Kol 2:2; Flp 1:6Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, 126:12 Ebr 13:7; 10:36; 2The 1:4; Yak 1:3; Ufu 13:10; 14:12ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi.

Uhakika Wa Ahadi Ya Mungu

136:13 Mwa 22:16, 17; Lk 1:73; Za 105:9Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, 146:14 Mwa 22:17akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 156:15 Mwa 21:5Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.

166:16 Kut 22:10Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote. 176:17 Ebr 6:18; Za 110:4; Rum 4:16; Ebr 11:9; Rum 11:29Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo. 186:18 Hes 23:19; Tit 1:2; Ebr 3:6Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti. 196:19 Law 16:2; Ebr 9:2, 3, 7Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho iliyo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika sehemu takatifu iliyopo nyuma ya pazia, 206:20 Ebr 4:14; 2:17; 5:6mahali ambapo Yesu mtangulizi wetu aliingia kwa niaba yetu. Yeye amekuwa Kuhani Mkuu milele, kwa mfano wa Melkizedeki.