Waebrania 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waebrania 4:1-16

Pumziko Aliloahidi Mungu

14:1 Ebr 12:15Kwa hiyo, kwa kuwa bado ahadi ya kuingia rahani iko wazi, tujihadhari ili hata mmoja wenu asije akaikosa. 24:2 1The 2:13Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia; lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. 34:3 Za 95:11; Kum 1:34, 35; Ebr 3:11Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha, kama vile Mungu alivyosema,

“Kwa hiyo nikaapa katika hasira yangu,

‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ”

Lakini kazi yake ilikamilika tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 44:4 Mwa 2:2, 3; Kut 20:11Kwa maana mahali fulani amezungumza kuhusu siku ya saba, akisema: “Katika siku ya saba Mungu alipumzika kutoka kazi zake zote.” 54:5 Za 95:11; Ebr 3:3Tena hapo juu asema, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.”

64:6 Ebr 5:1; 3:18Kwa hiyo inabaki kuwa wazi kwa wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii. 74:7 Za 95:7, 8; Ebr 3:7Kwa hiyo Mungu ameweka siku nyingine, akaiita Leo, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa:

“Leo, kama mkiisikia sauti yake,

msiifanye mioyo yenu migumu.”

84:8 Yos 22:4; Ebr 1:1Kwa maana kama Yoshua alikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine. 9Kwa hiyo basi, imebaki raha ya Sabato kwa ajili ya watu wa Mungu; 104:10 Law 23:3; Ufu 14:13; Ebr 5:4kwa kuwa kila mmoja aingiaye katika raha ya Mungu pia hupumzika kutoka kazi zake mwenyewe, kama vile Mungu alivyopumzika kutoka kazi zake. 114:11 Ebr 5:6; 3:18Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili kwamba asiwepo yeyote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii.

124:12 Mk 4:14; 5:1; 11:28; Yn 10:35; Mdo 12:24; 1The 2:13; Isa 55:11; Yer 23:29; Ufu 1:16; 1Kor 14:24, 25Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 134:13 Za 33:13-15; Mit 5:21; Yer 16:17; 23:24; Dan 2:22Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye kwake ni lazima tutatoa hesabu.

Yesu Kristo Kuhani Mkuu Kuliko Wote

144:14 Ebr 2:17; 6:20; 8:1; 9:2; Mt 4:3; Ebr 3:1Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Yesu Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu. 154:15 Ebr 2:17, 18; 2Kor 5:21; Isa 53:3; Lk 22:28; 1Pet 2:22; 1Yn 3:5; Ebr 7:26Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo: lakini yeye hakutenda dhambi. 164:16 Ebr 7:19; Efe 2:18; 3:12; Ebr 10:19Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.