Waebrania 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 13:1-25

Huduma Inayompendeza Mungu

113:1 Rum 12:10; 1The 4:9; 1Pet 1:22; 2:17; 3:8; 4:8; 2Pet 1:7; 1Yn 3:11; 4:7Endeleeni kupendana kama ndugu. 213:2 Mt 25:35; Rum 12:13; 1Tim 3:2; 1Pet 4:9; Mwa 18:3; 19:2Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua. 313:3 Mt 25:36; Kol 4:18; Ebr 10:34; Rum 12:15; 1Kor 12:26; 1Pet 3:8Wakumbukeni wale waliofungwa gerezani kana kwamba ninyi mmefungwa pamoja nao. Pia wakumbukeni wale wanaotendewa vibaya, kana kwamba ni ninyi wenyewe mnateswa.

413:4 Mal 2:15; 1Kor 7:38; 1Tim 4:3; Kum 22:22; 1Kor 6:9; Efe 5:5; Ufu 22:15Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote. 513:5 1Tim 3:3; Flp 4:11; Kum 31:6, 8; Yos 1:5; Mwa 28:15; Mt 6:25, 34; 1Nya 28:20; Za 37:25Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,

“Kamwe sitakuacha,

wala sitakupungukia.”

613:6 Za 27:1; 56:4; 118:6Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,

“Bwana ni msaada wangu; sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?”

713:7 Ebr 13:17, 24; 1Kor 16:16; Ebr 4:12; 6:12Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao. 813:8 Yn 8:58; Ebr 1:12; Za 102:27; Ufu 1:4Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele.

913:9 Efe 4:14; Kol 2:7; 2:16; Ebr 9:10; Rum 14:17; 1Yn 4:1; 1Tim 4:3Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria. 1013:10 1Kor 9:13; 10:18Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema hawana haki ya kula vile vitu vilivyowekwa juu yake.

1113:11 Law 16:15; Kut 29:14; Law 4:12; 9:11; 16:27; Hes 19:3Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. 1213:12 Yn 19:17, 18; Mdo 7:58; Efe 5:26; Rum 3:25Vivyo hivyo, Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe. 1313:13 Lk 9:23; Ebr 11:26; 1Pet 4:14Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. 1413:14 Mik 2:10; Flp 3:20Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao.

1513:15 1Pet 2:5; Isa 57:19; Hos 14:2; Efe 5:20; Law 7:12; Za 50:14, 23; 107:22; 116:17; Hos 14:2Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake. 1613:16 Rum 12:13; Flp 4:18; 1Kor 9:12; Ebr 6:10Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.

1713:17 Isa 62:6; Mdo 20:28; Ebr 13:7, 24; Flp 2:29; 1The 5:12; 1Tim 5:17; Eze 3:17; 33:2, 7; Mdo 20:26Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

1813:18 1The 5:25; Mdo 23:1Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia. 19Ninawasihi zaidi mniombee ili nipate kurudishwa kwenu upesi.

Maombi Ya Kuwatakia Baraka

20Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, 21awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen.

Maneno Ya Mwisho Na Salamu

2213:22 1Pet 5:12; Yak 1:21Ndugu zangu, nawasihi mchukuliane na maneno yangu ya maonyo, kwa kuwa nimewaandikia waraka mfupi tu.

2313:23 1The 3:2; Mdo 16:1; 1Tim 6:12Nataka ninyi mjue kwamba ndugu yetu Timotheo amefunguliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja pamoja naye kuwaona.

2413:24 Ebr 13:7, 17; Mdo 18:2Wasalimuni viongozi wenu wote na watakatifu wote. Wale wa kutoka Italia wanawasalimu.

2513:25 Tit 3:15; Kol 4:18Neema iwe nanyi nyote. Amen.