Waebrania 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waebrania 10:1-39

Dhabihu Ya Kristo Ni Mara Moja Tu

110:1 Kol 2:17; Ebr 8:5; 9:23; 9:11; 9:9; 9:14Sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. 210:2 Ebr 9:9Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. 310:3 Law 16:21; 16:34; Ebr 9:7Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, 410:4 Mik 6:6, 7; Ebr 9:13; 9:11kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

510:5 Ebr 1:6; 2:14; 1Pet 2:24; Za 40:6; 50:8; Isa 1:11; Yer 6:20; Amo 5:21, 22Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani, alisema:

“Dhabihu na sadaka hukuzitaka,

bali mwili uliniandalia;

6sadaka za kuteketezwa na za dhambi

hukupendezwa nazo.

710:7 Ezr 6:2; Yer 36:2; Za 40:6-8; Mt 26:39Ndipo niliposema, ‘Mimi hapa, nimekuja,

imeandikwa kunihusu katika kitabu:

Nimekuja kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu.’ ”

810:8 Ebr 10:5, 6; Mk 12:33Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe). 910:9 Ebr 10:7Kisha akasema “Mimi hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi yako.” Aondoa lile Agano la kwanza ili kuimarisha la pili. 1010:10 Ebr 10:14; Efe 5:26; Ebr 2:14; 7:27; 1Pet 2:24Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.

1110:11 Ebr 5:1; 10:1, 4; Hes 28:3; Ebr 7:27Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi. 1210:12 Ebr 5:1; Mk 16:19; Ebr 1:3; Kol 3:1Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu. 1310:13 Yos 10:24; Ebr 1:13; Za 110:1; Mdo 2:35; 1Kor 15:25Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake, 1410:14 Ebr 10:1; Efe 5:26kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.

1510:15 Ebr 3:7Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema:

1610:16 Yer 31:33; Ebr 8:10“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao

baada ya siku hizo, asema Bwana.

Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao,

na kuziandika katika nia zao.”

1710:17 Yer 31:34; Ebr 8:12Kisha aongeza kusema:

“Dhambi zao na kutokutii kwao

sitakumbuka tena.”

18Basi haya yakiisha kusamehewa, hakuna tena dhabihu yoyote inayotolewa kwa ajili ya dhambi.

Wito Wa Kuvumilia

1910:19 Efe 3:12; Law 16:2; Efe 2:18; Ebr 9:8, 12, 25Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, 2010:20 Ebr 9:8; 6:19; 9:3kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kwa ajili yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili wake, 2110:21 Ebr 2:17; 3:6basi kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu juu ya nyumba ya Mungu, 2210:22 Ebr 10:1; 7:19; 3:12; Yak 1:6; 1Yn 3:21; Eze 36:25; 2Kor 7:1; 1Pet 1:2; Mdo 22:16sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi. 2310:23 Ebr 3:6; 3; 1; 1Kor 1:9Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumbayumba, kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu. 2410:24 Tit 2:14Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema. 2510:25 Mdo 2:42; Ebr 3:13; 1Kor 3:13Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.

2610:26 Kut 21:14; Hes 15:30; Ebr 5:2; 6:4-8; 2Pet 2:20; 1Tim 2:4Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. 2710:27 Isa 26:11; 2The 1:7; Ebr 9:27; 12:29Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu. 2810:28 Kum 17:6, 7; Mt 18:16; Ebr 2:2; Yn 8:17Yeyote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu. 2910:29 Ebr 2:3; 12:25; 1Kor 11:29; Mt 12:32; Efe 4:30; Mt 4:3; Ufu 1:5; Ebr 6:6; Mt 26:28Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema? 3010:30 Kum 32:35; Rum 12:19; Kum 32:36; Za 135:14Kwa kuwa tunamjua yeye aliyesema, “Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.” Tena asema, “Bwana atawahukumu watu wake.” 3110:31 2Kor 5:11; Isa 19:16; Mt 16:16Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.

3210:32 Ebr 6:4; Flp 1:9, 30; Gal 3:4; 2Yn 8; Kol 2:1Kumbukeni siku zile za kwanza, ambazo mkiisha kutiwa nuru mlistahimili mashindano makali ya maumivu. 33Wakati mwingine mlitukanwa na kuteswa hadharani; wakati mwingine mlikuwa radhi kuungana na wale waliofanyiwa hivyo. 3410:34 Ebr 13:3; 11:16; 1Pet 1:4, 5Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyangʼanywa mali zenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.

3510:35 Efe 3:12; Mt 5:12; 10:32Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno. 3610:36 Rum 5:3; Ebr 5:11; 12:1; Yak 1:3, 4, 12; 2Pet 1:6; Ebr 6:15; 9:15Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi. 3710:37 Mt 11:3; Ufu 22:20; Lk 18:8; 2Pet 3:9; Hab 2:3, 4Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu,

“Yeye ajaye atakuja wala hatakawia.

3810:38 Rum 1:17; Gal 3:11; Hab 2:3, 4Lakini mwenye haki wangu

ataishi kwa imani.

Naye kama akisitasita,

sina furaha naye.”

3910:39 2Pet 2:20, 21; Mdo 16:30, 31; 1The 5:9; 2The 2:14Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaositasita na kuangamia, bali tuko miongoni mwa hao wenye imani na hivyo tunaokolewa.