Waebrania 1 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waebrania 1:1-14

Mwana Ni Mkuu Kuliko Malaika

11:1 Efe 3:1; 2Kor 1:1; Hes 12:6, 8; Yn 9:29; Ebr 2:3; 4:8; 12:25; Lk 1:70; Mdo 2:30Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, 21:2 Kum 4:30; Ebr 9:26; 1Pet 1:20; Ebr 1:5; Mt 3:17; Ebr 3:6; 5:8; 7:28; Za 2:8; Mt 28:18; Yn 1:3; Ebr 11:3lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. 31:3 Yn 1:14; 14:9; Kol 1:17; Tit 2:14; Ebr 7:27; Mk 16:19Mwana ni mngʼao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni. 41:4 Efe 1:21; Flp 2:9, 10; Ebr 8:6Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.

51:5 Za 2:7; Mt 3:17; 2Sam 7:14Kwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wowote Mungu alipata kumwambia,

“Wewe ni Mwanangu;

leo mimi nimekuzaa?”

Au tena,

“Mimi nitakuwa Baba yake,

naye atakuwa Mwanangu?”

61:6 Yn 3:16; Kol 1:18; Ebr 10:5; Kum 32:43; Za 97:7Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema,

“Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.”

71:7 Za 104:4Anenapo kuhusu malaika asema,

“Huwafanya malaika wake kuwa pepo,

watumishi wake kuwa miali ya moto.”

81:8 Lk 1:33; Za 45:6, 7Lakini kwa habari za Mwana asema,

“Kiti chako cha enzi, Ee Mungu,

kitadumu milele na milele,

nayo haki itakuwa fimbo ya utawala

ya ufalme wako.

91:9 Flp 2:9; Isa 61:1, 3; Za 45:6, 7; Mdo 4; 27; 10:38Umependa haki na kuchukia uovu;

kwa hiyo Mungu, Mungu wako,

amekuweka juu ya wenzako

kwa kukupaka mafuta ya furaha.”

101:10 Za 8:6; 102:25; Zek 12:1Pia asema,

“Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia,

nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.

111:11 Isa 34:4; 51:6; Ebr 12:27; Mt 24:35; 2Pet 3:7; 3:10; Ufu 21:1Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu;

zote zitachakaa kama vazi.

121:12 Ebr 13:8; Za 102:25, 27Utazikungʼutakungʼuta kama joho,

nazo zitachakaa kama vazi.

Lakini wewe hubadiliki,

nayo miaka yako haikomi kamwe.”

131:13 Ebr 1:3; Mk 16:19; Yos 10:24; Ebr 10:13; Za 110:1; Mt 22:44Je, ni kwa malaika yupi ambaye Mungu amepata kumwambia wakati wowote,

“Keti mkono wangu wa kuume,

hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako”?

141:14 Za 91:11; 103:20; Dan 7:10; Mt 25:34; Mk 10:17; Mdo 20:32; Rum 11:14; Ebr 2:3; 5:9; 9:28Je, malaika wote si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?

New International Version

Hebrews 1:1-14

God’s Final Word: His Son

1In the past God spoke to our ancestors through the prophets at many times and in various ways, 2but in these last days he has spoken to us by his Son, whom he appointed heir of all things, and through whom also he made the universe. 3The Son is the radiance of God’s glory and the exact representation of his being, sustaining all things by his powerful word. After he had provided purification for sins, he sat down at the right hand of the Majesty in heaven. 4So he became as much superior to the angels as the name he has inherited is superior to theirs.

The Son Superior to Angels

5For to which of the angels did God ever say,

“You are my Son;

today I have become your Father”1:5 Psalm 2:7?

Or again,

“I will be his Father,

and he will be my Son”1:5 2 Samuel 7:14; 1 Chron. 17:13?

6And again, when God brings his firstborn into the world, he says,

“Let all God’s angels worship him.”1:6 Deut. 32:43 (see Dead Sea Scrolls and Septuagint)

7In speaking of the angels he says,

“He makes his angels spirits,

and his servants flames of fire.”1:7 Psalm 104:4

8But about the Son he says,

“Your throne, O God, will last for ever and ever;

a scepter of justice will be the scepter of your kingdom.

9You have loved righteousness and hated wickedness;

therefore God, your God, has set you above your companions

by anointing you with the oil of joy.”1:9 Psalm 45:6,7

10He also says,

“In the beginning, Lord, you laid the foundations of the earth,

and the heavens are the work of your hands.

11They will perish, but you remain;

they will all wear out like a garment.

12You will roll them up like a robe;

like a garment they will be changed.

But you remain the same,

and your years will never end.”1:12 Psalm 102:25-27

13To which of the angels did God ever say,

“Sit at my right hand

until I make your enemies

a footstool for your feet”1:13 Psalm 110:1?

14Are not all angels ministering spirits sent to serve those who will inherit salvation?