Waamuzi 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 6:1-40

Gideoni

16:1 Amu 2:11; Mwa 25:2; Hes 25:15-18Waisraeli wakafanya tena yaliyo maovu mbele za Bwana, naye kwa miaka saba Bwana akawatia mikononi mwa Wamidiani. 26:2 1Sam 13:6; Isa 5:30; 8:21; 26:16; 27:3; 2:19; Yer 48:28; 49:8; Ay 24:8; Yer 41:9; Ebr 11:38Mkono wa Midiani ukawa na nguvu dhidi ya Israeli na kwa ajili ya Wamidiani, Waisraeli wakajitengenezea mahali pa kujificha milimani, kwenye mapango na ngome. 36:3 Hes 13:29; Mwa 25:6; Isa 11:14; Yer 49:28Kila wakati Waisraeli walipopanda mazao mashambani, Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki walivamia nchi yao. 46:4 Law 26:16; Kum 28:30, 51; Isa 10:6; 42:22; Mwa 10:19Wakapiga kambi katika mashamba yao na kuharibu mazao ya nchi yote hadi kufikia Gaza, wala hawakuacha kiumbe chochote kilicho hai kwa Waisraeli, iwe kondoo au ngʼombe au punda. 56:5 Kum 28:42; Amu 8:10; Isa 21:7; 60:6; Yer 49:28Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia zao; wakavamia nchi ili kuiharibu. 6Waisraeli wakafanywa kuwa maskini sana na Wamidiani, hata Israeli wakamlilia Bwana kuomba msaada.

76:7 Amu 3:9Waisraeli walipomlilia Bwana kwa sababu ya Wamidiani, 86:8 Kum 18:15; 1Fal 20:13, 22; 2Fal 17:13, 23; Neh 9:29; Yer 25:5; Ay 36:10; Eze 18:30-31; Amu 2; 1Bwana akawapelekea nabii, ambaye aliwaambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Niliwapandisha mtoke Misri, toka nchi ya utumwa. 96:9 Neh 10:9; Za 136:24; 44:2Nikawanyakua kutoka mikononi mwa Wamisri na kutoka mikononi mwa watesi wenu wote. Nikawafukuza watoke mbele yenu nami nikawapa ninyi nchi yao. 106:10 Kut 20:5; Yos 24:15; Yer 10:2Nikawaambia, ‘Mimi ndimi Bwana Mungu wenu; msiiabudu miungu ya Waamori, ambayo mnakaa katika nchi yao!’ Lakini ninyi hamkuitii sauti yangu.”

116:11 Mwa 16:7; Yos 18:23; Amu 7:14; 8:13, 29; Hes 26:30; Amu 7:1; 8; 1; Ebr 11:32; Rut 2:17; 3:2; 1Sam 23:1; Neh 13:15; Isa 16:10; 63:3; Mao 1:15; Yoe 3:13Malaika wa Bwana akaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi, Mwabiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione. 126:12 Yos 1:5; Rut 2:4; 1Sam 10:7; Za 129:8; Amu 11:1; Lk 1:11, 28Malaika wa Bwana alipomtokea Gideoni, akamwambia, “Bwana yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.”

136:13 Yos 3:5; 2Sam 7:22; Za 44; 1; 78:3; Kum 31:17; 2Nya 15; 2Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Bwana hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”

146:14 Ebr 11:34; Amu 10:1; 1Fal 14:27Bwana akamgeukia na kusema “Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kutoka mikononi mwa Wamidiani. Je, si mimi ninayekutuma wewe?”

156:15 Isa 60:22; 1Sam 9:20-21Gideoni akauliza, “Ee Bwana wangu, nitawezaje kuwaokoa Israeli? Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.”

166:16 Kut 3:12; Hes 14:43; Yos 1:5Bwana akamjibu, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.”

176:17 Mwa 24:14; Kut 3; 12; 4:8Gideoni akajibu, “Kama basi nimepata kibali machoni pako, nipe ishara kuonyesha kweli kwamba ni wewe unayesema nami. 18Tafadhali ninakuomba usiondoke hapa mpaka nitakaporudi na kukuletea sadaka yangu na kuiweka mbele yako.”

Naye Bwana akamwambia, “Nitangoja mpaka utakaporudi.”

196:19 Mwa 18:7-8; Law 19:36; Amu 13:15Gideoni akaingia ndani ya nyumba yake na kuandaa mwana-mbuzi pamoja na kuoka mikate isiyotiwa chachu kutokana na efa moja6:19 Efa moja ni sawa na lita 22. ya unga. Akaweka nyama kwenye kikapu na mchuzi kwenye chungu, akamletea huyo malaika hapo nje chini ya mti wa mwaloni na kumpa.

206:20 Amu 13:19Malaika wa Mungu akamwambia, “Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uviweke juu ya mwamba huu na umimine huo mchuzi juu yake.” Gideoni akafanya hivyo. 216:21 Kut 4:2; Law 9:24Malaika wa Bwana akainyoosha fimbo iliyokuwa mkononi mwake, ncha yake ikagusa ile nyama na ile mikate isiyotiwa chachu, nao moto ukatoka kwenye mwamba ukateketeza ile nyama na ile mikate. Malaika wa Bwana akatoweka kutoka machoni pake. 226:22 Kum 13:16; Mwa 32:30; 11:32Gideoni alipotambua kuwa ni malaika wa Bwana, akapiga kelele kwa mshangao, akasema, “Ole wangu, Bwana Mwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!”

236:23 Dan 10:19; Mwa 16:13; Kum 5:26Lakini Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.”

246:24 Mwa 22:14; Yos 18:23Hivyo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom.6:24 Yehova-Shalom maana yake Bwana ni Amani. Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.

256:25 Kut 34:13; Amu 2:13; Kum 2:13; 7:5Usiku ule ule Bwana akamwambia, “Mchukue ngʼombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate Ashera iliyo karibu nayo. 266:26 Mwa 8:20Kisha mjengee Bwana Mungu wako, madhabahu halisi, kwa taratibu zake, juu ya huu mwamba. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.”

27Basi Gideoni akawachukua watumishi wake kumi na kufanya kama Bwana alivyomwambia. Lakini kwa kuwa aliwaogopa jamaa yake na watu wa mji, akafanya haya usiku badala ya mchana.

286:28 1Fal 16:32; 2Fal 21:3Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa na yule ngʼombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu yaliyojengwa upya!

29Wakaulizana, “Ni nani aliyetenda mambo haya?”

Walipochunguza kwa makini, wakaambiwa, “Ni Gideoni mwana wa Yoashi, ndiye alitenda hivi.”

30Watu wa mji wakamwambia Yoashi, “Mlete mwanao hapa. Ni lazima afe, kwa sababu amebomoa madhabahu ya Baali na kukatakata nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo.”

316:31 1Sam 24:15; Za 43:1; Yer 30:13Lakini Yoashi akauambia ule umati uliokuwa umezunguka ukiwa kinyume naye, “Je, ninyi mtamtetea Baali? Mnajaribu kumwokoa? Yeyote mwenye kumpigania atauawa kufikia kesho asubuhi! Kama Baali ni mungu kweli, anaweza kujitetea mwenyewe wakati mtu anapobomoa madhabahu yake.” 326:32 Amu 7:1; 8:29, 35; 9:1; 1Sam 12:11Basi siku ile wakamwita Gideoni “Yerub-Baali,” yaani, “Baali na ashindane naye,” kwa sababu alibomoa madhabahu yake.

336:33 Hes 13:29; Mwa 25:6; Yos 15:56; Eze 25:4; Hos 1:5Basi Wamidiani wote, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki wakaunganisha majeshi yao, wakavuka ngʼambo ya Yordani na kupiga kambi katika Bonde la Yezreeli. 346:34 Amu 3:10; Yos 6:20; Amu 3:27; Yos 17:2Ndipo Roho wa Bwana akamjia Gideoni, akapiga tarumbeta, akiwaita Waabiezeri ili wamfuate. 356:35 Yos 17:7; Amu 4:6; 7:23Akatuma wajumbe waende katika Manase yote, akiwataka wachukue silaha na pia katika Asheri, Zabuloni na Naftali, nao wakakwea ili kukutana nao.

36Gideoni akamwambia Mungu, “Kama utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu, kama ulivyoahidi: 376:37 Ay 31:20; Hes 18; 27; 2Sam 6:6; 24:16; Mwa 24; 14tazama, nitaweka ngozi ya kondoo kwenye kiwanja cha kupuria nafaka, na kama utakuwepo umande juu ya ngozi tu, nayo ardhi yote ikiwa kavu, ndipo nitakapojua kuwa utaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.” 38Hivyo ndivyo ilivyotokea. Gideoni akaamka asubuhi na mapema kesho yake, akaikamua ile ngozi, umande ukatoka, maji ya kujaa bakuli.

396:39 Mwa 18:32Kisha Gideoni akamwambia Bwana, “Usinikasirikie. Ninaomba nifanye ombi moja lingine. Niruhusu nifanye jaribio jingine moja kwa ngozi hii. Wakati huu uifanye ngozi hii kavu na ardhi yote ifunikwe na umande.” 406:40 Kut 4:3-7; Isa 28:7Usiku ule Mungu akafanya hivyo. Ngozi ile ilikuwa kavu, nayo ardhi yote ikafunikwa na umande.