Waamuzi 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 5:1-31

Wimbo Wa Debora

15:1 Amu 4:4, 6; Kut 15:1; Za 32:7Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:

25:2 2Nya 17:16; Za 110:3“Wakuu katika Israeli wanapoongoza,

wakati watu wanapojitoa

kwa hiari yao wenyewe:

mhimidini Bwana!

35:3 Kut 15:1; Za 27; 6“Sikieni hili, enyi wafalme!

Sikilizeni, enyi watawala!

Nitamwimbia Bwana, nitaimba;

kwa wimbo nitamhimidi Bwana,

Mungu wa Israeli.

45:4 Kut 13:21; Hes 24:18; Kut 33:2; 2Sam 22:8; Za 18:7; 77:18; 82:5; Isa 2:19-21; 64:3; Yer 10; 10; 50:46; 51:29; Yoe 3:16; Nah 1:5; Hab 3:6; Za 68:8; 77:17“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri,

ulipopita katika mashamba ya Edomu,

nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,

naam, mawingu yakamwaga maji.

55:5 Kut 19:18; Za 29:6; 46:3; 77:18; 114:4; Isa 64:3Milima ilitetemeka mbele za Bwana,

hata ule wa Sinai,

mbele za Bwana,

Mungu wa Israeli.

65:6 Amu 3:31; 4:17; Law 26:22; Isa 33:8; Za 125:5; Isa 59:8“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,

katika siku za Yaeli,

barabara kuu hazikuwa na watu;

wasafiri walipita njia za kando.

75:7 Amu 4:4Mashujaa walikoma katika Israeli,

walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka,

nilipoinuka kama mama katika Israeli.

85:8 Kum 32:17; Amu 2:13; Yos 2:5; Hes 25:7Walipochagua miungu migeni,

vita vilikuja katika malango ya mji,

hapakuonekana ngao wala mkuki

miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.

9Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli,

pamoja na wale wanaojitoa wenyewe

kwa hiari yao miongoni mwa watu.

Mhimidini Bwana!

105:10 Mwa 49:11; Amu 12:14; 10:4“Nanyi mpandao punda weupe,

mkiketi juu ya matandiko ya thamani,

nanyi mtembeao barabarani,

fikirini 115:11 1Sam 12:7; Dan 9:16; Mik 6:5juu ya sauti za waimbaji

mahali pa kunyweshea maji.

Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana,

matendo ya haki ya mashujaa wake

katika Israeli.

“Ndipo watu wa Bwana

walipoteremka malangoni pa mji.

125:12 Za 44:23; 57:8; Isa 51:9, 17; Amu 4:4-6; Za 68:18; Efe 4:8‘Amka, amka! Debora!

Amka, amka, uimbe!

Ee Baraka! Inuka,

chukua mateka wako uliowateka,

ee mwana wa Abinoamu.’

13“Ndipo mabaki ya watu

wakashuka dhidi ya wenye nguvu,

watu wa Bwana,

wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.

145:14 Mwa 41:52; Amu 1:29; 3:13; Hes 34:21; Mwa 50:23Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;

Benyamini akiwa miongoni

mwa watu waliokufuata.

Kutoka Makiri wakashuka viongozi,

na kutoka Zabuloni wale washikao

fimbo ya jemadari.

155:15 Mwa 50:18; Amu 4:4-6Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;

naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,

wakija nyuma yake kwa mbio

wakielekea bondeni.

Katika jamaa za Reubeni,

palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

165:16 Mwa 49:11; Hes 32; 1Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo

kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi?

Kwa jamaa za Reubeni,

palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

175:17 Yos 12:2; 17:7; 19:29Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani.

Naye Dani, kwa nini alikaa

kwenye merikebu siku nyingi?

Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,

akikaa kwenye ghuba zake ndogo.

185:18 Mwa 30:20; 30:8; Za 68:27; Amu 9:6Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao,

vilevile nao watu wa Naftali.

195:19 Yos 11:5; Amu 4; 13; Ufu 16:16; Yos 12:21; Amu 1:27“Wafalme walikuja na kufanya vita;

wafalme wa Kanaani walipigana

huko Taanaki karibu na maji ya Megido,

lakini hawakuchukua fedha wala nyara.

205:20 Yos 10:11Kutoka mbinguni nyota zilipigana,

nyota kutoka njia zake

zilipigana na Sisera.

215:21 Amu 4:7; Yos 1:6Mto wa Kishoni uliwasomba,

ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.

Songa mbele, ee nafsi yangu,

kwa ujasiri!

225:22 Yer 8:16Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo:

farasi wake wenye nguvu

huenda mbio kwa kurukaruka.

23Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe.

Walaaniwe watu wake kwa uchungu,

kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana,

kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’

245:24 Lk 1:42; Amu 4:17; Mwa 15:19“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote,

mkewe Heberi, Mkeni,

abarikiwe kuliko wanawake wote

waishio kwenye mahema.

255:25 Mwa 18:8; Amu 4:19Aliomba maji, naye akampa maziwa;

kwenye bakuli la heshima

akamletea maziwa mgando.

26Akanyoosha mkono wake

akashika kigingi cha hema,

mkono wake wa kuume

ukashika nyundo ya fundi.

Akampiga Sisera kwa nyundo,

akamponda kichwa chake,

akamvunjavunja na kumtoboa

paji lake la uso.

27Aliinama miguuni pa Yaeli,

akaanguka; akalala hapo.

Pale alipoinama miguuni pake,

alianguka;

pale alipoinamia, ndipo alipoanguka,

akiwa amekufa.

285:28 Yos 2:15; Mit 7:6“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia;

nyuma ya dirisha alilia, akasema,

‘Mbona gari lake linachelewa kufika?

Mbona vishindo vya magari yake

vimechelewa?’

29Wanawake wenye busara

kuliko wengine wote wakamjibu;

naam, husema moyoni mwake,

305:30 Kut 15:9; 1Sam 30:24; Za 68:12; 45:14; Eze 16:10; 2Sam 1:24‘Je, hawapati na kugawanya nyara:

msichana mmoja au wawili kwa kila mtu,

mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara,

mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa,

mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu:

yote haya yakiwa nyara?’

315:31 Hes 10:35; 2Sam 23:4; Ay 37:21; Za 19:4; 89:36; Isa 18:4; 2Sam 18:32; Amu 3:11“Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana!

Bali wote wakupendao na wawe kama jua

lichomozavyo kwa nguvu zake.”

Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.