Waamuzi 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 4:1-24

Debora

14:1 Amu 3:15; 2:11; 2:19Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni pa Bwana. 24:2 Kum 32:30; Yos 11:1; 1Sam 12:9; Za 83:9Hivyo Bwana akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu4:2 Haroshethi-Hagoyimu ina maana Haroshethi ya Mataifa. 34:3 Yos 17:16; Amu 10:12; Za 106:42; Amu 1:19Kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma yapatayo 900, naye alikuwa amewatesa Waisraeli kwa ukatili kwa muda wa miaka ishirini, Waisraeli wakamlilia Bwana wakaomba msaada.

44:4 Amu 5:1, 7, 12; Kut 15:20Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye alikuwa anaamua Israeli wakati ule. 54:5 1Sam 14:2; 22; 6; Yos 18:25; 12:5-9; Mwa 35:8Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue. 64:6 Amu 5:12-15; 1Sam 12:11; Ebr 11:32; Yos 12:22; Mwa 30:8; Amu 5:18; 6:35; Yos 19:22Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “Bwana, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume 10,000 toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori. 74:7 Yos 11:1; Amu 5:12; 1Fal 18:40; Za 83:9; Amu 1:2Nitamshawishi Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, pamoja na magari yake na jeshi lake, hadi Mto Kishoni na kumtia mikononi mwako.’ ”

8Baraka akamwambia, “Ukienda pamoja nami nitakwenda, lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.”

94:9 Yos 12:22; Amu 2:14Debora akamwambia, “Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Bwana atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi, 104:10 2Nya 36:23; Ezr 1:2; Isa 41:2; 42:6; 45:3; 46:11; 48:15mahali ambapo Baraka aliwaita Zabuloni na Naftali. Watu 10,000 wakamfuata Baraka, na Debora pia akaenda pamoja naye.

114:11 Mwa 15:19; Hes 10:29; Yos 24:26; Amu 9:6; Yos 19:33Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni wengine, yaani, wazao wa Hobabu, mkwewe Mose, naye akapiga hema lake karibu na ule mti mkubwa wa mwaloni ulioko Saananimu, karibu na Kedeshi.

124:12 Yos 19:22Sisera alipoambiwa kuwa Baraka mwana wa Abinoamu alikuwa amepanda Mlima Tabori, 134:13 Yos 17:16; Amu 4:7; 5:19Sisera akakusanya pamoja magari yake yote 600 ya chuma na watu wote waliokuwa pamoja naye, kuanzia Haroshethi-Hagoyimu mpaka Mto wa Kishoni.

144:14 Amu 1:2; Kum 9:3; 1Sam 8:20; 2Sam 5:24; Za 68:7Ndipo Debora akamwambia Baraka, “Nenda! Hii ndiyo siku ambayo Bwana amemtia Sisera mikononi mwako. Je, Bwana hakukutangulia mbele yako?” Hivyo Baraka akashuka kutoka Mlima Tabori, akifuatwa na watu 10,000. 154:15 Kut 14:24; Za 18:14; Kut 14:28; Za 83:9-10Bwana akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, pamoja na jeshi lake lote kwa upanga mbele ya Baraka, naye Sisera akaliacha gari lake na kukimbia kwa miguu. 164:16 Kut 14:28; Za 83:9-10Lakini Baraka akafuata magari pamoja na jeshi mpaka Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.

174:17 Amu 5:6, 24; Mwa 15:19; Yos 11; 1Sisera, hata hivyo, akakimbia kwa miguu mpaka kwenye hema la Yaeli, mkewe Heberi, Mkeni, kwa sababu palikuwa na uhusiano wa kirafiki kati ya Yabini mfalme wa Hazori na ukoo wa Heberi, Mkeni.

18Yaeli akaenda kumlaki Sisera na kumwambia, “Karibu, bwana wangu, karibu ingia ndani kabisa. Usiogope.” Basi Sisera akaingia ndani ya hema ya Yaeli, naye akamfunika kwa blanketi nene.

194:19 Mwa 18:8; Amu 5:25Akamwambia, “Nina kiu, tafadhali nipe maji ya kunywa.” Ndipo akafungua kiriba cha maziwa na kumpa akanywa, kisha akamfunika.

20Naye Sisera akamwambia, “Simama mlangoni pa hema na mtu yeyote akija na kukuuliza, ‘Je, kuna mtu yeyote hapa?’ sema, ‘Hapana.’ ”

214:21 Mwa 2:21; 15:12; 1Sam 26:12; Isa 29:10; Yon 1:5; Amu 5:26Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi, akiwa amechoka. Akakigongomea kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa.

224:22 Amu 5:27Baraka akakaribia akimfuatia Sisera, Yaeli akatoka kumlaki. Akamwambia, “Njoo, nitakuonyesha mtu unayemtafuta.” Hivyo wakaingia ndani ya hema wakiwa wamefuatana na tazama Sisera alikuwa amelala humo, akiwa amekufa, na hicho kigingi cha hema kikiwa kimegongomewa kupitia paji la uso wake.

234:23 Neh 9:24; Za 18:47; 44:2; 47:3; 144:2; Yos 11; 1Basi siku ile Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani, mbele ya Israeli. 244:24 Za 83:9; 106:43Nao mkono wa Waisraeli ukaendelea kuwa na nguvu zaidi na zaidi dhidi ya Yabini, mfalme wa Kanaani, mpaka wakamwangamiza.