Waamuzi 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 3:1-31

Mataifa Yaliyobaki Katika Ile Nchi

13:1 Kut 15:25Haya ndiyo mataifa Bwana aliyoyaacha ili kuwajaribu Waisraeli wote ambao hawakujua vita vyovyote vya Kanaani 2(alifanya hivi ili tu kuwafundisha wazao wa Waisraeli ambao hawakuwa wamejua vita hapo awali): 33:3 Yos 13:2; Mwa 10:14; 10:17; Kut 3:8; Kum 3:8; Hes 13:21wafalme watano wa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni, Wahivi waishio katika milima ya Lebanoni kuanzia Mlima wa Baal-Hermoni hadi Lebo-Hamathi. 43:4 Kut 12:25Waliachwa ili kuwajaribu Waisraeli kuona kama wangetii amri za Bwana, alizokuwa amewapa baba zao kwa mkono wa Mose.

53:5 Za 106:36; Yos 3:10; 11:3; Ezr 9:1Waisraeli wakaishi miongoni mwa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 63:6 Ezr 10:18; Neh 13:23; Mal 2:11; Kut 34:16; Kum 7:3-4, 16Wakawaoa binti zao, nao wakawatoa binti zao waolewe na wana wa hayo mataifa, na kuitumikia miungu yao.

Othnieli

73:7 Kum 4:9; 32:18; Amu 8:34; Za 78:11; 106:7; Yer 23:27; Amu 2:11-13; 1Fal 16:33; 2Nya 34:7; Isa 17:8Waisraeli wakafanya maovu machoni pa Bwana, wakamsahau Bwana Mungu wao na kutumikia Mabaali na Maashera. 83:8 Amu 2:14; Za 44:12; Isa 50:1; 52:3; Mwa 24:10Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli, hivyo akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-Rishathaimu mfalme wa Aramu-Naharaimu3:8 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. ambaye Israeli walikuwa chini yake wakimtumikia kwa muda wa miaka minane. 93:9 Amu 6:6-7; 10:10; 1Sam 12:10; Za 106:44; 107:13; Kum 28:29; Neh 9:27Waisraeli walipomlilia Bwana, yeye akawainulia mwokozi, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, ambaye aliwaokoa. 103:10 Hes 11:25; Amu 6:34; 11:29; 13:25; 14:6; 15:14; 1Sam 11:6; 16:13; 1Fal 18:46; 1Nya 12:18; 2Nya 24:20; Isa 11:2; Mwa 10:22Roho wa Bwana akaja juu yake, hivyo akawa mwamuzi wa Israeli, akaenda vitani. Bwana akamtia Kushan-Rishathaimu mfalme wa Aramu mikononi mwa Othnieli, naye akamshinda. 113:11 Yos 14:15; Amu 5:31; 8:28; Kut 16:35; 15:17Hivyo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arobaini, mpaka Othnieli mwana wa Kenazi alipofariki.

Ehudi

123:12 Amu 2:11; 1Sam 12:9Waisraeli wakafanya maovu mbele za Bwana tena, kwa kuwa walifanya maovu hayo Bwana akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu dhidi ya Israeli. 133:13 Mwa 19:38; Amu 10:11; Mwa 14:7; Amu 1:16Egloni akawataka Waamoni na Waamaleki waungane naye, akaja kuishambulia Israeli, nao wakatwaa Mji wa Mitende3:13 Yaani Yeriko. 143:14 Yer 48:1Waisraeli wakawa chini ya Egloni mfalme wa Moabu kwa muda wa miaka kumi na minane.

153:15 Amu 1:4; 20:16; 1Nya 12:2; 2Sam 8:2-6; 1Fal 4:21; 2Fal 17:3; Es 10:1; Za 68:29; 72:10; 89:22; Mhu 2:8; Isa 60:5; Hos 10:6; Za 107:13Waisraeli wakamlilia tena Bwana, naye akawapa mwokozi: Ehudi, mtu wa shoto, mwana wa Gera, Mbenyamini. Waisraeli wakatuma kwa Egloni mfalme wa Moabu ushuru kwa mkono wa Ehudi. 16Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja,3:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume. 173:17 Ay 15:27; Za 73:4Akamkabidhi ushuru Egloni mfalme wa Moabu, ambaye alikuwa mtu mnene sana. 18Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru aliwaruhusu waende zao. 19Yeye mwenyewe akafuatana nao hadi kwenye sanamu ya kuchora kwenye mawe karibu na Gilgali, ndipo yeye akarudi, akafika kwa Egloni na kusema, “Ee Mfalme, ninao ujumbe wa siri kwa ajili yako.”

Mfalme akasema, “Nyamazeni kimya!” Nao wale waliomhudumia wote wakamwacha, wakatoka nje.

203:20 Amo 3:15; Neh 8:5Ndipo Ehudi akamsogelea alipokuwa ameketi peke yake kwenye chumba cha juu cha jumba lake la kifalme la majira ya kiangazi, na kusema, “Ninao ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yako.” Mfalme alipokuwa anainuka kutoka kwenye kiti chake, 213:21 2Sam 2:16; 3:27; 20:10Ehudi akaunyoosha mkono wake wa kushoto na kuufuta ule upanga aliokuwa ameufunga kwenye paja lake la kulia, akamdunga Mfalme Egloni tumboni mwake. 22Hata mpini nao ukazama tumboni pamoja na upanga wenyewe, nao upanga ukatokea mgongoni mwake. Ehudi hakuuchomoa huo upanga, nayo mafuta yakashikamana juu ya upanga. 23Ehudi akatoka nje barazani; akamfungia milango ya chumba cha juu na kuifunga kwa funguo.

243:24 1Sam 24:3Baada ya kuondoka, watumishi wakaja na kukuta milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka amejipumzisha kwenye chumba cha ndani cha nyumba yake ya majira ya kiangazi.” 253:25 2Fal 2:17; 8:11Wakangoja hata wakawa na fadhaa, basi wakati hakufungua milango ya chumba, wakachukua funguo na kuifungua. Tazama wakaona bwana wao amelala sakafuni, amekufa.

26Walipokuwa wangali wanangoja, Ehudi akatoroka, akapita hapo kwenye sanamu ya kuchora kwenye mawe na kukimbilia Seira. 273:27 Law 25:9; Amu 6:34; 7:18; 2Sam 2:28; Isa 18:3; Yer 42:14Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza.

283:28 Mwa 19:37; Yos 2:24; Amu 1:2; Hes 13:29; Yos 2:9Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa Bwana amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakateremka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakuacha mtu yeyote kuvuka. 29Wakati huo wakawaua Wamoabu watu waume wapatao 10,000 ambao wote walikuwa wenye nguvu na mashujaa; hakuna mtu yeyote aliyetoroka. 303:30 Mwa 36:35Siku ile Moabu wakashindwa na Israeli, nayo nchi ikawa na amani kwa miaka themanini.

Shamgari

313:31 Amu 5:6; Yos 23:10; 13:2; Amu 10:11; 13:1; 1Sam 5:1; 31:1; 2Sam 8:1; Yer 25:30; 47:1Baada ya Ehudi akaja Shamgari mwana wa Anathi, aliyewapiga Wafilisti 600 kwa fimbo iliyochongoka ya kuongozea ngʼombe. Naye pia akawaokoa Waisraeli.