Waamuzi 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 14:1-20

Ndoa Ya Samsoni

114:1 Amu 13:24; Mwa 38:12Samsoni akateremkia Timna, akamwona mwanamke wa Kifilisti. 214:2 Mwa 21:21; 34:4Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipe ili awe mke wangu.”

314:3 Mwa 24:4; 34:14; 1Sam 14:6; Kut 34:16; Kum 7:3Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda kujitwalia mwanamke kutoka kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa?”

Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza.” 414:4 Kum 2:30; Yos 11:20; Amu 13:1; 15:11(Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa Bwana, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.) 5Samsoni akateremkia Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia. 614:6 Amu 3:10; 1Sam 17:35; Amu 13:25Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono yake bila silaha yoyote kama vile mtu ampasuavyo mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake aliyoyafanya. 7Basi akateremka na kuongea na yule mwanamke, naye akampendeza Samsoni.

8Baada ya muda aliporudi ili akamwoe, akatazama kando ili kuutazama mzoga wa yule simba, na tazama, kulikuwa na kundi la nyuki ndani ya ule mzoga wa simba na kulikuwa na asali; 9akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba.

1014:10 Mwa 29:2Basi baba yake akateremka kumwona huyo mwanamke. Samsoni akafanya karamu huko, kama ilivyokuwa desturi ya vijana. 11Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye.

1214:12 Hes 12:8; Eze 17:2; 20:49; 24:3; Hos 12:10; Mwa 29:27; 45:22Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini. 13Lakini msipoweza kufumbua, ndipo ninyi mtanipa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.”

Wakamwambia, “Tuambie hicho kitendawili, hebu na tukisikie.”

14Akawaambia,

“Ndani ya mlaji,

kulitoka kitu cha kuliwa,

ndani ya mwenye nguvu,

kulitoka kitu kitamu.”

Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.

1514:15 Amu 16:5; Mhu 7:26; Law 20:14-16; Amu 15:6Siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atueleze hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyangʼanya kile tulicho nacho?”

1614:16 Amu 16:15Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.”

Samsoni akamwambia, “Wala sijamweleza baba yangu wala mama yangu, kwa nini nikufumbulie?” 1714:17 Es 1:5Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ile ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye akawaeleza watu wake kile kitendawili.

18Siku ya saba kabla ya jua kutua, watu wa mji wakamwambia Samsoni,

“Ni nini kitamu kama asali?

Ni nini chenye nguvu kama simba?”

Samsoni akawaambia,

“Kama hamkulima na mtamba wangu,

hamngeweza kufumbua

kitendawili changu.”

1914:19 Amu 3:10; 2Nya 24:20; Yos 13:3; Isa 11:2; 1Sam 11:6Ndipo Roho wa Bwana akamjia Samsoni kwa nguvu. Akateremka mpaka Ashkeloni, akawaua watu waume thelathini miongoni mwa watu wa mji, akatwaa mali zao na nguo zao, akawapa watu wale waliofumbua kile kitendawili. Akiwa na hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake. 2014:20 Amu 15:2, 6; Yn 3:29Lakini huyo mke wa Samsoni akakabidhiwa kwa rafiki yake Samsoni ambaye alikuwa rafiki yake msaidizi siku ya arusi.