Waamuzi 12 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 12:1-15

Yefta Na Efraimu

112:1 Yos 13:27; Amu 11:1; 8:1Watu wa Efraimu wakaita majeshi yao, wakavuka kwenda Zafoni, wakamwambia Yefta, “Kwa nini mmekwenda kupigana na Waamoni bila kutuita ili twende pamoja nawe? Basi tutaichoma moto nyumba yako, pamoja nawe ukiwa ndani yake.”

2Yefta akajibu, “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa na Waamoni, hata ingawa niliwaita hamkuniokoa katika mkono wao. 312:3 Amu 9:17; Kum 20:7; 1Sam 19:5; Ay 13:14Nilipoona kuwa hamkunipa msaada nikauhatarisha uhai wangu na nikavuka kupigana na Waamoni. Naye Bwana akanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?”

412:4 1Fal 17:1; Mwa 46:20; Isa 9:21; 19:2Ndipo Yefta akakusanya watu wa Gileadi pamoja na kupigana na Efraimu. Wagileadi wakawashinda Efraimu, kwa kuwa Waefraimu walisema, “Ninyi Wagileadi ni watoro mliotoroka toka Efraimu na Manase.” 512:5 Yos 2:5-7; Amu 3:28Wagileadi wakaviteka vivuko vya Yordani dhidi ya hao Waefraimu, kisha ilikuwa yeyote yule aliyenusurika katika Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao watu wa Gileadi walimuuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Kama alijibu “Hapana,” 6walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’ ” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo.

7Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Basi Yefta akafa, akazikwa katika mmojawapo wa miji ya Gileadi.

Ibzani, Eloni Na Abdoni

812:8 Mwa 35:19Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. 9Alikuwa na wana thelathini na binti thelathini. Akawaoza binti zake kwa watu wengine nje ya ukoo wake, na kuwatwalia wanawe wanawake thelathini toka nje ya ukoo wake. Ibzani akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka saba. 10Ibzani akafa, akazikwa huko Bethlehemu.

11Baada yake Eloni, Mzabuloni, akawa mwamuzi wa Israeli, naye akawaamua kwa muda wa miaka kumi. 1212:12 Yos 10:12Kisha Eloni akafa, akazikwa katika Aiyaloni, katika nchi ya Zabuloni.

1312:13 2Sam 23:30; 1Nya 11:31; 27:14Baada yake, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi wa Israeli. 1412:14 Amu 8:30; 5:10; 10:4Naye akazaa wana arobaini na wana wa wanawe thelathini waliopanda punda sabini. Akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka minane. 1512:15 Amu 5:14Ndipo Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, naye akazikwa huko Pirathoni katika Efraimu, katika nchi ya vilima ya Waamaleki.