Waamuzi 10 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 10:1-18

Tola

110:1 Amu 8:31; Mwa 30:18; 46:13; Amu 6:14; Yos 15:48; Amu 2:16Baada ya Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyeishi huko Shamiri, katika nchi ya vilima ya Efraimu, akainuka kuokoa Israeli. 2Akaamua Israeli kwa miaka ishirini na mitatu. Ndipo akafa, naye akazikwa huko Shamiri.

Yairi

310:3 Hes 32:41Baada yake akafuatiwa na Yairi, Mgileadi, ambaye aliamua Israeli kwa miaka ishirini na miwili. 410:4 Mwa 49:11; 1Fal 1:33; Hes 32:41Alikuwa na wana thelathini waliopanda punda thelathini. Nao walikuwa na miji thelathini iliyoko Gileadi, inayoitwa Hawoth-Yairi mpaka leo. 510:5 Hes 32:41Yairi akafa, naye akazikwa huko Kamoni.

Yefta

610:6 Amu 2:11, 13; Eze 27:16; Mwa 10:15; 19:38; Hes 21:29; Mwa 26:1; Amu 2:12; Kum 32:15Wana wa Israeli wakatenda tena maovu machoni pa Bwana. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni na miungu ya Wafilisti. Kwa kuwa Waisraeli walimwacha Bwana wala hawakuendelea kumtumikia, 710:7 Kum 31:17; 32:30hivyo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni, 810:8 Yos 12:2ambao waliwaonea na kuwatesa mwaka ule. Kwa miaka kumi na minane wakawatesa Waisraeli wote upande wa mashariki ya Mto Yordani katika Gileadi, nchi ya Waamori. 910:9 Amu 1:22; 11:4Waamoni nao wakavuka Yordani ili kupigana na Yuda, Benyamini na nyumba ya Efraimu, nayo nyumba ya Israeli ikawa katika taabu kubwa. 1010:10 Amu 3:9; Kut 9:27; Za 32:5; Yer 3:25; 8:14; 14:20; 2:27Ndipo Waisraeli wakamlilia Bwana wakasema, “Tumetenda dhambi dhidi yako, kumwacha Mungu wetu na kutumikia Mabaali.”

1110:11 Kut 14:30; Mwa 14:7; Amu 3:13, 31Bwana akawaambia, “Wakati Wamisri, Waamori, Waamoni, Wafilisti, 1210:12 Mwa 14:7; Yos 15:55; Amu 4:3; Za 106:42Wasidoni, Waamaleki na Wamaoni walipowaonea na ninyi mkanililia na kuomba msaada, je, sikuwaokoa kutoka mikononi mwao? 1310:13 Kum 32:15; Yer 11:10; 13:10Lakini ninyi mmeniacha mimi na kutumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena. 1410:14 Isa 44:17; 57:13; Kum 32:37; Yer 2:28; 11:12; Hab 2:18Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!”

1510:15 1Sam 3:18; 2Sam 10:12; 15:26; Ay 1:21; Isa 39:8Lakini Waisraeli wakamwambia Bwana, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.” 1610:16 Yos 24:23; Yer 18:8; Isa 63:9; Kum 32:36; Za 106:44-45Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni katikati yao nao wakamtumikia Bwana. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli.

1710:17 Mwa 31:49; Amu 11:29Ndipo Waamoni wakaitwa vitani na kupiga kambi huko Gileadi, Waisraeli wakakusanyika na kupiga kambi huko Mispa. 1810:18 Amu 11:8-9Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana wao kwa wao, “Yeyote yule atakayeanzisha mashambulizi dhidi ya Waamoni atakuwa kiongozi wa wote wakaao Gileadi.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

士师记 10:1-18

士师陀拉和雅珥

1亚比米勒死后,以萨迦陀拉拯救了以色列人。他住在以法莲山区的沙密,祖父是朵多,父亲是普瓦2陀拉以色列的士师二十三年,死后葬在沙密

3之后,基列雅珥以色列的士师二十二年。 4他有三十个儿子,每人骑一头驴。他们在基列拥有三十座城,那些城到现在还叫“雅珥之城”。 5雅珥死后,葬在加们

以色列人因犯罪而受罚

6后来,以色列人又做耶和华视为恶的事,祭拜巴力亚斯她录,又拜亚兰西顿摩押亚扪非利士的神明。他们背弃耶和华,不再事奉祂。 7耶和华向他们发怒,把他们交在非利士人和亚扪人手中。 8那年,非利士人和亚扪人击垮了以色列人,压迫基列地区、约旦河东亚摩利境内的以色列人达十八年。 9亚扪人还渡过约旦河攻击犹大便雅悯以法莲支派,使以色列人苦不堪言。 10于是,他们呼求耶和华说:“我们背弃我们的上帝去祭拜巴力,我们得罪了你。” 11耶和华对他们说:“你们受埃及人、亚摩利人、亚扪人、非利士人、 12西顿人、亚玛力人和马云人的压迫,就呼求我,我岂没有拯救你们吗? 13但你们竟背弃我,去事奉其他神明,所以我不再救你们。 14你们去呼求自己选择的神明吧!你们有难,让他们救你们吧!” 15他们对耶和华说:“我们犯了罪,任你处置我们,只求你今天拯救我们。” 16以色列人除掉了他们的外邦神像,转而事奉耶和华。耶和华不忍再看以色列人受苦。

17当时,亚扪人整装备战,在基列安营;以色列人也集合起来,在米斯巴安营。 18基列的首领们彼此商议说:“谁先攻打亚扪人,谁就做所有基列人的首领。”