Ufunuo 3 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 3:1-22

Kwa Kanisa Lililoko Sardi

13:1 Ufu 1:4; 1:16; 2:2; 1Tim 5:6“Kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika:

“Haya ndiyo maneno ya aliye na zile Roho saba3:1 Roho saba za Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa. 23:2 Eze 34:4Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyosalia na yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu. 33:3 Ufu 2:5; 2Pet 3:10Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na ukatubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala hutajua saa nitakayokuja kwako.

43:4 Yud 23; Ufu 6:11“Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili. 53:5 Ufu 20:12; Mt 10:32Yeye ashindaye atavikwa vazi jeupe kama wao. Sitafuta jina lake kutoka kitabu cha uzima, bali nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele za malaika wake. 63:6 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.

Kwa Kanisa Lililoko Filadelfia

73:7 Yn 5:20; Isa 22:22; Mt 16:19“Kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 83:8 Mdo 14:27; Ufu 2:13Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno langu wala hukulikana Jina langu. 93:9 Ufu 2:9; Isa 49:23; 43:4Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, nitawafanya waje wapige magoti miguuni pako, na wakiri ya kwamba nimekupenda. 103:10 2Pet 2:9; Ufu 2:10; 11:10; 17:8Kwa kuwa umeshika amri yangu ya kuvumilia katika saburi, nitakulinda katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote, ili kuwajaribu wote wakaao duniani.

113:11 Ufu 2:25; Mt 16:27; Ufu 2:25; 1Kor 9:25“Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. 123:12 Gal 2:9; Ufu 14:1; 22:4; 21:2-10Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji mkubwa wa Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya. 133:13 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.

Kwa Kanisa Lililoko Laodikia

143:14 Kol 1:16-18“Kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu. 153:15 Rum 12:11Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa moja au lingine. 16Hivyo kwa kuwa u vuguvugu, si baridi wala moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. 173:17 Hos 12:8; 1Kor 4:8Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu chochote.’ Lakini hutambui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi. 183:18 Ufu 16:15Nakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, ili upate kuwa tajiri, na mavazi meupe ili uyavae upate kuficha aibu ya uchi wako, na mafuta ya kupaka macho yako ili upate kuona.

193:19 Kum 8:5; 1Kor 11:32; Ufu 2:5“Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu. 203:20 Mt 24:33; Lk 12:36; Yn 14:23Tazama! Nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu yeyote akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami.

213:21 Mt 19:28; Ufu 5:5“Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 223:22 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.”

New International Version

Revelation 3:1-22

To the Church in Sardis

1“To the angel3:1 Or messenger; also in verses 7 and 14 of the church in Sardis write:

These are the words of him who holds the seven spirits3:1 That is, the sevenfold Spirit of God and the seven stars. I know your deeds; you have a reputation of being alive, but you are dead. 2Wake up! Strengthen what remains and is about to die, for I have found your deeds unfinished in the sight of my God. 3Remember, therefore, what you have received and heard; hold it fast, and repent. But if you do not wake up, I will come like a thief, and you will not know at what time I will come to you.

4Yet you have a few people in Sardis who have not soiled their clothes. They will walk with me, dressed in white, for they are worthy. 5The one who is victorious will, like them, be dressed in white. I will never blot out the name of that person from the book of life, but will acknowledge that name before my Father and his angels. 6Whoever has ears, let them hear what the Spirit says to the churches.

To the Church in Philadelphia

7“To the angel of the church in Philadelphia write:

These are the words of him who is holy and true, who holds the key of David. What he opens no one can shut, and what he shuts no one can open. 8I know your deeds. See, I have placed before you an open door that no one can shut. I know that you have little strength, yet you have kept my word and have not denied my name. 9I will make those who are of the synagogue of Satan, who claim to be Jews though they are not, but are liars—I will make them come and fall down at your feet and acknowledge that I have loved you. 10Since you have kept my command to endure patiently, I will also keep you from the hour of trial that is going to come on the whole world to test the inhabitants of the earth.

11I am coming soon. Hold on to what you have, so that no one will take your crown. 12The one who is victorious I will make a pillar in the temple of my God. Never again will they leave it. I will write on them the name of my God and the name of the city of my God, the new Jerusalem, which is coming down out of heaven from my God; and I will also write on them my new name. 13Whoever has ears, let them hear what the Spirit says to the churches.

To the Church in Laodicea

14“To the angel of the church in Laodicea write:

These are the words of the Amen, the faithful and true witness, the ruler of God’s creation. 15I know your deeds, that you are neither cold nor hot. I wish you were either one or the other! 16So, because you are lukewarm—neither hot nor cold—I am about to spit you out of my mouth. 17You say, ‘I am rich; I have acquired wealth and do not need a thing.’ But you do not realize that you are wretched, pitiful, poor, blind and naked. 18I counsel you to buy from me gold refined in the fire, so you can become rich; and white clothes to wear, so you can cover your shameful nakedness; and salve to put on your eyes, so you can see.

19Those whom I love I rebuke and discipline. So be earnest and repent. 20Here I am! I stand at the door and knock. If anyone hears my voice and opens the door, I will come in and eat with that person, and they with me.

21To the one who is victorious, I will give the right to sit with me on my throne, just as I was victorious and sat down with my Father on his throne. 22Whoever has ears, let them hear what the Spirit says to the churches.”