Ufunuo 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 15:1-8

Malaika Saba Na Mapigo Saba

115:1 Ufu 12:1-3; 17:1; 21:9; Law 26:21Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni: malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika. 215:2 Ufu 4:6; 13:14Nikaona kile kilichoonekana kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Kando ya hiyo bahari, walikuwa wamesimama wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake pamoja na tarakimu ya jina lake. Mikononi mwao walikuwa wameshika vinubi walivyopewa na Mungu. 315:3 Kut 15:1; Kum 32:4; Za 111:2; 145:17Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema:

Bwana Mungu Mwenyezi,

matendo yako ni makuu na ya ajabu.

Njia zako wewe ni za haki na za kweli,

Mfalme wa nyakati zote!

415:4 Yer 10:7; Isa 66:23Ni nani ambaye hatakuogopa wewe Bwana

na kulitukuza jina lako?

Kwa kuwa wewe peke yako ndiwe mtakatifu.

Mataifa yote yatakuja

na kuabudu mbele zako,

kwa kuwa matendo yako ya haki

yamedhihirishwa.”

515:5 Ufu 11:19; Hes 1:50Baada ya haya nikatazama, nalo hekalu, la hema la Ushuhuda, lilikuwa limefunguliwa mbinguni. 615:6 Ufu 14:15; 1:13Ndani ya lile hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani ingʼaayo na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao. 715:7 Ufu 4:6Ndipo mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, yeye aishiye milele na milele. 815:8 Isa 6:4; 1Fal 8:10-11; 2Nya 5:13-14Nalo lile hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna yeyote aliyeweza kuingia mle hekaluni mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.