Ufunuo 14 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 14:1-20

Mwana-Kondoo Na Wale 144,000

114:1 Ufu 5:6; Za 2:6; Ufu 7:4; 3:12Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao. 214:2 Ufu 1:15; 5:8-9; Eze 1:24; 43:2Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kwa kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao. 314:3 Ufu 5:9; 4:6; 4:4; 14:1Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wanne wenye uhai na wale wazee. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. 414:4 2Kor 11:2; Ufu 3:4; Yak 1:18Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni bikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 514:5 Yn 1:47; Efe 5:27Vinywani mwao hapakuonekana uongo, wala hawakuwa na hatia yoyote.

Malaika Watatu

614:6 Ufu 8:13; 19:17; 3:10; 13:7Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. 714:7 Za 34:9; Ufu 15:4; 11:13; 8:10Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”

814:8 Isa 21:9; Ufu 17:2-4; 18:3Malaika wa pili akafuata akisema, “Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu, ule uliyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.”

914:9 Ufu 13:14Malaika wa tatu akawafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, “Kama mtu yeyote anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso au kwenye mkono wake, 1014:10 Isa 51:17; Yer 25:15; 51:7yeye pia atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. 1114:11 Isa 34:10; Ufu 19:3Nao moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa yeyote anayepokea chapa ya jina lake.” 1214:12 Ufu 13:10; 1Kor 15:18; 1The 4:16; 1Kor 15:18; 1The 4:16Hapa ndipo penye wito wa subira na uvumilivu wa watakatifu; wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu katika uaminifu kwa Yesu.

1314:13 1Kor 15:18; 1The 4:16; Ufu 2:7; 22:17Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wafu wafao katika Bwana tangu sasa.”

“Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”

Kuvuna Mavuno Ya Dunia

1414:14 Dan 7:13; Ufu 1:13; 6:2Nikatazama, hapo mbele yangu palikuwa na wingu jeupe, na aliyekuwa ameketi juu ya hilo wingu alikuwa “kama Mwana wa Adamu” mwenye taji ya dhahabu kichwani mwake na mundu mkali mkononi mwake. 1514:15 Yoe 3:13; Mk 4:29; Yer 51:33Kisha malaika mwingine akaja kutoka hekaluni naye akamwita kwa sauti kubwa yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akasema, “Chukua mundu wako ukavune kwa kuwa wakati wa mavuno umewadia, kwa maana mavuno ya dunia yamekomaa.” 16Hivyo yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akauzungusha mundu wake duniani, nayo dunia ikavunwa.

1714:17 Ufu 14:15Malaika mwingine akatoka katika hekalu lililoko mbinguni, naye pia alikuwa na mundu mkali. 1814:18 Ufu 6:9; 8:5; 16:7; 14:15Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.” 1914:19 Ufu 19:15Hivyo yule malaika akauzungusha mundu wake duniani na kukusanya zabibu za dunia na kuzitupa kwenye shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu. 2014:20 Yoe 3:13; Ebr 13:12; Ufu 11:8Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasi,14:20 Kimo cha hatamu za farasi ni kama mita moja na nusu. kwa umbali wa maili 200.14:20 Maili 200 ni sawa na kilomita 320.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

启示录 14:1-20

天上的新歌

1我又观看,见羔羊站在锡安山上,与祂在一起的有十四万四千人,他们额上都有祂和祂父的名字。 2我听见有声音从天上传来,像江海澎湃,像雷霆轰鸣,又像琴师弹奏竖琴的声音。 3他们在宝座前,在四个活物和众长老面前唱一首新歌。除了从地上被赎出来的十四万四千人以外,没有人能学得会这歌。 4这些人从未沾染过妇女,都是童身。无论羔羊往哪里去,他们都紧随其后。他们是从世人中被赎出来的,作为初熟的果实献给上帝和羔羊。 5他们从未说谎,纯洁无瑕。

三位天使的信息

6我看见另一位天使在空中飞翔,要将永远的福音传给地上的各国家、各部落、各语言族群、各民族。 7他大声说:“要敬畏上帝,归荣耀给祂,因为祂审判的时候到了。要敬拜造天地、海洋和一切水源的上帝。”

8接着又一位天使说:“巴比伦大城倒塌了!倒塌了!她曾使万民喝她淫乱的烈酒。”14:8 以赛亚书21:9

9之后,第三位天使高喊:“一切敬拜怪兽和兽像、在手或额上接受兽印的, 10都要喝上帝烈怒调制的酒,就是祂怒杯里毫无掺杂的烈酒。他们要在圣天使和羔羊面前,在火和硫磺中受煎熬。 11他们受煎熬所冒的烟不断上腾,永无休止。那些拜兽、兽像和接受了兽名印记的人昼夜不得安宁。” 12因此,持守上帝命令和耶稣真道的圣徒需要坚忍。

13我听见天上有声音说:“你将下面的话写下来,从今以后,那些为主而死的人有福了!”

圣灵说:“是的!他们将得享安息,不再劳苦。他们工作的成果必随着他们。”

地上的收割

14我又观看,见有一朵白云,上面坐着的好像是人子,14:14 但以理书7:13祂头戴金冠,手拿锋利的镰刀。 15有一位天使从殿中出来,扬声向坐在云上的那位说:“挥动你的镰刀收割吧!地上的庄稼已经熟透了,可以收割了。” 16于是,坐在云上的那位便向大地挥动镰刀,把地上的庄稼都收割了。

17另一位天使手里也拿着锋利的镰刀从天上的殿中出来。 18又有一位掌管火的天使从祭坛那里出来,对手拿镰刀的天使高喊:“挥动你锋利的镰刀,收取地上葡萄树的果实吧!它们已经熟透了。” 19于是,那天使挥动镰刀,收取了地上的葡萄,抛到上帝烈怒的大榨酒池中。 20葡萄在城外的榨酒池中被踩踏,血从榨酒池中涌出,高至马的嚼环,流了三百公里14:20 “三百公里”希腊文是“一千六百司他町”。远。