Ufunuo 12 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 12:1-17

Mwanamke Na Joka

1Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ukiwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake. 212:2 Gal 4:19Alikuwa na mimba naye akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kuzaa. 312:3 Dan 7:7, 20; Ufu 13:1; 19:21Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: Likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. 412:4 Ufu 8:7; Dan 8:10; Mt 22:16Mkia wake ukakokota theluthi ya nyota zote angani na kuziangusha katika nchi. Ndipo lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kuzaa ili lipate kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. 512:5 Za 2:9; Ufu 19:15Yule mwanamke akazaa mtoto mwanaume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo yake ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti chake cha enzi. 612:6 Ufu 11:2Yule mwanamke akakimbilia jangwani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku 1,260.

Malaika Mikaeli Amshinda Yule Joka

7Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao. 8Lakini joka na malaika zake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi yao huko mbinguni. 912:9 Mwa 3:1-7; Mt 25:41; Ufu 20:3, 8, 10; Lk 10:18; Yn 12:31Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.

Ushindi Mbinguni Watangazwa

1012:10 Ufu 11:15; Zek 3:1Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema:

“Sasa wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja

na mamlaka ya Kristo wake.

Kwa kuwa ametupwa chini

mshtaki wa ndugu zetu,

anayewashtaki mbele za Mungu

usiku na mchana.

1112:11 Ufu 7:14; 6:9; Lk 14:26Nao wakamshinda

kwa damu ya Mwana-Kondoo

na kwa neno la ushuhuda wao.

Wala wao hawakuyapenda maisha yao

hata kufa.

1212:12 Isa 44:23; Ufu 18:20; 8:13; 10:6Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu

na wote wakaao humo!

Lakini ole wenu nchi na bahari,

kwa maana huyo ibilisi ameshuka kwenu,

akiwa amejaa ghadhabu,

kwa sababu anajua ya kuwa

muda wake ni mfupi!”

13Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanaume. 1412:14 Kut 19:4; Dan 7:25Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko jangwani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu,12:14 Maana yake ni miaka mitatu na nusu. ya wakati ambako yule joka hawezi kufika. 15Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. 16Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake. 1712:17 Ufu 11:7; Mwa 3:15; Ufu 14:12; 1:2Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.