Ufunuo 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 1:1-20

Utangulizi Na Salamu

11:1 Ufu 22:16; Dan 2:28, 29; Yn 12:49; 17:8, 19; Ufu 22:6Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo ni lazima yatukie hivi karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika wake kwa Yohana mtumishi wake, 21:2 1Kor 1:6; Ufu 6:9; Ebr 4:12; Ufu 12:17; 19:10ambaye anashuhudia kuhusu kila kitu alichokiona, yaani, Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. 31:3 Lk 11:28; Ufu 22:7; Rum 13:11Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.

Salamu Kwa Makanisa Saba

41:4 Isa 11:2; Rum 1:7; Ufu 4:8; 11:17; 3:1; 4:5; 5:6Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia:

Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, na kutoka kwa wale roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi, 51:5 Isa 55:4; Kol 1:18; Ufu 17:14na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni yule shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, mtawala wa wafalme wa dunia.

Kwake yeye anayetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka dhambi zetu kwa damu yake, 61:6 1Pet 2:5; Rum 11:36akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.

71:7 Dan 7:13; Zek 12:10Tazama! Anakuja na mawingu,

na kila jicho litamwona,

hata wale waliomchoma;

na makabila yote duniani

yataomboleza kwa sababu yake.

Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.

81:8 Ufu 22:6; 4:8; 21:6; 22:13; 15:3; Kut 3:14; Isa 41:4; Ufu 21:6“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”

Maono Ya Kristo

91:9 Mdo 14:22; 2Tim 2:12Mimi, Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Yesu na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu. 101:10 Ufu 17:3; 3:1Katika siku ya Bwana, nilikuwa katika Roho na nikasikia sauti kubwa kama ya baragumu nyuma yangu 111:11 Ufu 2:8; 22:13; Mdo 18:19; Kol 2:1; Mdo 16:14ikisema, “Andika kwenye kitabu haya yote unayoyaona, kisha uyapeleke kwa makanisa saba, yaani: Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.”

121:12 Zek 1:2; Ufu 3:1Ndipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Nami nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu, 131:13 Eze 1:26; Ufu 14:14; Dan 10:5; Ufu 15:6na katikati ya vile vinara vya taa, alikuwamo mtu kama Mwana wa Adamu, akiwa amevaa joho refu, na mkanda wa dhahabu ukiwa umefungwa kifuani mwake. 141:14 Dan 7:9; Ufu 19:12Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji, nayo macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. 151:15 Eze 1:7; 43:2; Ufu 2:18; 19:6Nyayo zake zilikuwa kama shaba inayongʼaa, katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mugurumo ya maji mengi. 161:16 Ufu 3:1; Isa 1:20; Ebr 4:12Katika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua likingʼaa kwa nguvu zake zote.

171:17 Eze 1:28; Dan 8:17, 18; Isa 48:12; Ufu 22:13Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akauweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema: “Usiogope, Mimi ndiye wa Kwanza na wa Mwisho. 181:18 Rum 6:9; Kum 32:40; Ufu 9:1Mimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu.1:18 Kuzimu linalotokana na neno Hades la Kiyunani au Sheol kwa Kiebrania; maana yake ni mahali pa mateso kwa watu waliopotea.

191:19 Ufu 1:11; Hab 2:2“Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyopo na yale yatakayotukia baada ya haya. 201:20 Zek 4:2; Mt 5:14, 15Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, navyo vile vinara saba ni hayo makanisa saba.