Tito 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Tito 3:1-15

Kutenda Mema

13:1 Rum 13:1; 2Tim 2:21Wakumbushe watu kuwanyenyekea watawala na kuwatii wenye mamlaka, wawe tayari kutenda kila lililo jema. 23:2 Efe 4:31; 2Tim 2:24Wasimnenee mtu yeyote mabaya, wasiwe wagomvi, bali wawe wapole, wakionyesha unyenyekevu kwa watu wote.

33:3 Efe 2:2, 5, 8; 1Kor 6:11Maana sisi wenyewe wakati fulani tulikuwa wajinga, wasiotii, tukiwa watumwa wa tamaa mbaya na anasa za kila aina. Tuliishi katika uovu na wivu, tukichukiwa na kuchukiana sisi kwa sisi. 43:4 Efe 2:7; Tit 2:11; Mit 8:31; 1Tim 2:3Lakini wema na upendo wa Mungu Mwokozi wetu ulipofunuliwa, 53:5 Efe 2:9; Rum 12:2; 3:20; 9:11; Gal 2:16; 2Tim 1:9; Yn 3:3, 5alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 63:6 Rum 5:5; Eze 36:25; Yoe 2:28; Yn 1:16; Mdo 2:33; 10:45ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu, 73:7 Rum 3:24; 8:24; Tit 1:2ili kwamba, tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kuwa warithi tukiwa na tumaini la uzima wa milele. 83:8 1Tim 1:15; Tit 2:14Hili ni neno la kuaminiwa. Nami nataka uyasisitize mambo haya, ili wale ambao wamemwamini Mungu wapate kuwa waangalifu kujitoa kwa ajili ya kutenda mema wakati wote. Mambo haya ni mazuri tena ya manufaa kwa kila mtu.

93:9 1Tim 1:14; 2Tim 2:14Lakini jiepushe na maswali ya kipuzi, mambo ya koo, mabishano na ugomvi kuhusu sheria, kwa sababu hayana faida, tena ni ubatili. 103:10 Rum 16:17; 2Kor 13:2; Mt 18:17; 2The 3:6, 14; 2Tim 3:5; Yn 10Mtu anayesababisha mafarakano, mwonye mara ya kwanza, kisha mwonye mara ya pili. Baada ya hapo, usihusike naye tena. 113:11 Mdo 13:46; 1Tim 6:4, 5Kwa kuwa unajua kwamba mtu kama huyo amepotoka na tena ni mwenye dhambi. Yeye amejihukumu mwenyewe.

Maneno Ya Mwisho Na Kumtamkia Baraka

123:12 Mdo 20:4; 2Tim 4:9, 21Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi. 133:13 Mdo 18:24Fanya kila uwezalo uwasafirishe Zena yule mwanasheria na Apolo na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji katika safari yao. 14Watu wetu hawana budi kujifunza kutenda mema, ili waweze kuyakimu mahitaji ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.

153:15 1Tim 1:2; Kol 4:18Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu wale wanaotupenda katika imani.

Neema iwe nanyi nyote. Amen.