11:1 Rum 1:1; 1Tim 2:4Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na kuijua kweli iletayo utauwa: 21:2 2Tim 1:1; 1:9imani na ujuzi ulioko katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu, asiyesema uongo, aliahidi hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, 31:3 1Tim 1:6; 2Tim 1:10; 1Tim 1:11; Lk 1:47naye kwa wakati wake aliouweka alilidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu:
41:4 2Kor 2:13; 1Tim 1:2; Rum 1:7; 1:12; 2Kor 4:13; Gal 2:3Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote:
Neema iwe kwako na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Kazi Ya Tito Huko Krete
51:5 Mdo 27:7; 11:30Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 61:6 1Tim 3:2; 3:12; 4; 1The 3:13Mzee wa kanisa asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi. 71:7 1Tim 3:1; 1Kor 4:1; 1Tim 3:3, 8Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali. 81:8 1Tim 3:2; 2Tim 3:3Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake. 91:9 1Kor 16:13; 1Tim 1:10Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwaonya wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.
Walimu Wa Uongo
101:10 1Tim 1:6; Mdo 11:2Kwa maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, hasa wale wa kikundi cha tohara. 111:11 2Tim 3:6; Tit 3:6; Yn 10:12; 1Pet 5:2Hao ni lazima wanyamazishwe, kwa sababu wanaharibu watu wa nyumba nzima wakifundisha mambo yasiyowapasa kufundisha. Wanafanya hivyo kwa ajili ya kujipatia mapato ya udanganyifu. 121:12 Mdo 17:28; 2:11Hata mmojawapo wa manabii wao mwenyewe amesema, “Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi, wavivu.” 131:13 2Kor 13:10; Tit 2:2Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo, uwakemee kwa ukali wapate kuwa wazima katika imani, 141:14 1Tim 4:7; 1:4; Kol 2:22; 2Tim 4:4ili wasiendelee kuangalia hadithi za Kiyahudi au maagizo ya wale watu wanaoikataa kweli. 151:15 Rum 14:14, 23; Za 18:26; Mt 7:14-19; Mdo 10:9-16Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna chochote kilicho safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka. 161:16 1Yn 2; 4; Yer 5; 2; 12:2; Hos 8:2, 3Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.