Sefania 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Sefania 2:1-15

12:1 2Nya 20:4; Yoe 1:14; 2:16; Yer 3:3; 6:15Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja,

enyi taifa lisilo na aibu,

22:2 Isa 17:13; Hos 13:3; 2Fal 23:26; Yer 4:4; 10:25; Eze 7:19; Mao 4:11kabla ya wakati ulioamriwa haujafika

na siku ile inayopeperusha kama makapi,

kabla hasira kali ya Bwana haijaja juu yenu,

kabla siku ya ghadhabu ya Bwana

haijaja juu yenu.

32:3 Amo 5:6; Yoe 2:4; Isa 1:17; Za 45:4; 57:1; 76:9Mtafuteni Bwana, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi,

ninyi ambao hufanya lile analoamuru.

Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu;

labda mtahifadhiwa

siku ya hasira ya Bwana.

Dhidi Ya Ufilisti

42:4 Mwa 10:19; Amo 1:6-8; Zek 9:5-7; Yer 6:4; 47:5Gaza utaachwa

na Ashkeloni utaachwa magofu.

Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu

na Ekroni utangʼolewa.

52:5 1Sam 30:14; Law 26:31; Eze 25:16; Yos 13:3; Isa 14:30Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari,

enyi Wakerethi;

neno la Bwana liko dhidi yenu,

ee Kanaani, nchi ya Wafilisti.

“Mimi nitawaangamiza,

na hakuna atakayebaki.”

62:6 Isa 5:17; 17:2Nchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi Wakerethi,

patakuwa mahali pa wachungaji

na mazizi ya kondoo.

72:7 Isa 11:11; Hag 1:12; Mik 5:7; 4:10; Kut 4:31; Lk 1:68; Mwa 45:7; Kum 30:3; Za 126:4; Yer 23:3; 32:44; Hos 6:11; Eze 39:25; Yoe 3:1; Amo 1:6-8Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda,

hapo watapata malisho.

Wakati wa jioni watajilaza chini

katika nyumba za Ashkeloni.

Bwana Mungu wao atawatunza,

naye atawarudishia wafungwa wao.

Dhidi Ya Moabu Na Amoni

82:8 Mwa 19:37; Yer 48:27; 49:1; Eze 25:3, 8; 21:28; Mao 3:61; Isa 16:6“Nimeyasikia matukano ya Moabu

nazo dhihaka za Waamoni,

ambao waliwatukana watu wangu

na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.

92:9 Kum 23:6; 29:23; Isa 11:14; Yer 48:1-47; 49:1-6; Eze 25:1-11; 2Fal 19:31; Amo 1:13; 2:1-3Hakika, kama niishivyo,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,

Mungu wa Israeli,

“hakika Moabu itakuwa kama Sodoma,

Waamoni kama Gomora:

mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,

nchi ya ukiwa milele.

Mabaki ya watu wangu watawateka nyara;

mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”

102:10 Ay 40:12; Isa 16:6; Yer 48:27; Za 9:6Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao,

kwa kutukana na kudhihaki

watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote.

112:11 Mwa 49:10; 10:5; Za 2:8; 22:27; Isa 2:2, 3; Mal 1:11; Yn 4:21; 1Tim 2:8; Yoe 2:11; 1Nya 19:1; Eze 25:6-7; Isa 12:4; Za 86:9; Sef 3:9Bwana atakuwa wa kuhofisha kwao

atakapoangamiza miungu yote ya nchi.

Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,

kila moja katika nchi yake.

Dhidi Ya Kushi

122:12 Mwa 10:6; Isa 18:1; 20:4; Yer 46:10“Ninyi pia, ee Wakushi,

mtauawa kwa upanga wangu.”

Dhidi Ya Ashuru

132:13 Mwa 10:5-11; Zek 10:11; Mik 5:6Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini

na kuangamiza Waashuru,

akiiacha Ninawi ukiwa

na pakame kama jangwa.

142:14 Isa 5:17; 13:21; 14:23; Ufu 18:2; Za 102:6Makundi ya kondoo na ngʼombe yatajilaza pale,

viumbe vya kila aina.

Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba

wataishi juu ya nguzo zake.

Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani,

kifusi kitakuwa milangoni,

boriti za mierezi zitaachwa wazi.

152:15 Isa 32:9; 47:8; Eze 27:36; 28:2; Ufu 18:7; Yer 49:33; Nah 3:19Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha

wakijisikia salama.

Ulisema moyoni mwako,

“Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.”

Jinsi gani umekuwa gofu,

mahali pa kulala wanyama pori!

Wote wanaopita kando yake wanauzomea

na kutikisa mkono kwa dharau.