Sefania 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Sefania 1:1-18

11:1 2Fal 22:1; 2Tim 3:16; 2Pet 1:21; 1Nya 3:14Neno la Bwana lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda:

Onyo La Maangamizi Yanayokuja

21:2 Mwa 6:7Bwana asema,

“Nitafagia kila kitu

kutoka kwenye uso wa dunia.”

31:3 Yer 4:25; 50:3; Hos 4:3; Eze 14:17“Nitafagilia mbali watu na wanyama;

nitafagilia mbali ndege wa angani

na samaki wa baharini.

Wafanyao maovu watapata tu kokoto,

nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,”

asema Bwana.

Dhidi Ya Yuda

41:4 Yer 6:12; 15:6; Mik 5:13; Sef 2:11; Hos 10:5“Nitaiadhibu Yuda

na wote wakaao Yerusalemu.

Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali

kila mabaki ya Baali,

majina ya wapagani na makuhani

waabuduo sanamu:

51:5 Yer 5:7; 8:2; 1Fal 11:33; Law 18:21wale ambao husujudu juu ya mapaa

kuabudu jeshi la vitu vya angani,

wale ambao husujudu na kuapa kwa Bwana

na ambao pia huapa kwa Malkamu,

61:6 Yer 2:13; Isa 9:13; Hos 7:7wale wanaoacha kumfuata Bwana,

wala hawamtafuti Bwana

wala kutaka shauri lake.

71:7 Isa 13:6; 41:1; Eze 7:19; Yoe 3:14; Amo 5:18-20; Yer 46:10Nyamazeni mbele za Bwana Mwenyezi,

kwa maana siku ya Bwana iko karibu.

Bwana ameandaa dhabihu,

amewaweka wakfu wale aliowaalika.

81:8 Isa 24:21; Yer 39:6Katika siku ya dhabihu ya Bwana

nitawaadhibu wakuu

na wana wa mfalme

na wale wote wanaovaa

nguo za kigeni.

91:9 1Sam 5:5; Amo 3:10Katika siku hiyo nitaadhibu wote ambao

hukwepa kukanyaga kizingiti,

ambao hujaza hekalu la miungu yao

kwa dhuluma na udanganyifu.”

101:10 Isa 22:5; Neh 3:13; 2Nya 33:14; Amo 5:16Bwana asema, “Katika siku hiyo

kilio kitapanda juu kutoka lango la Samaki,

maombolezo kutoka mtaa wa pili,

na mshindo mkubwa kutoka vilimani.

111:11 Yak 5:1; Hos 9:6; Ufu 18:11, 12Ombolezeni, ninyi mnaoishi katika eneo la sokoni;

wafanyabiashara wenu wote wameangamizwa,

wote ambao wanafanya biashara ya fedha

wataangamizwa.

121:12 Amo 6:1; Ay 21:15; Za 10:11-13; Yer 48:11; Eze 8:12; 2Fal 21:16; Ay 22:13Wakati huo nitasaka mji wa Yerusalemu kwa taa,

na kuwaadhibu wale ambao

wanakaa katika hali ya kuridhika,

ambao ni kama divai

iliyobaki kwenye machicha,

ambao hudhani, ‘Bwana hatafanya lolote,

jema au baya.’

131:13 2Fal 24:13; Yer 15:13; Mik 6:15; Kum 28:30-39; Mao 5:2; Amo 5:11Utajiri wao utatekwa nyara,

nyumba zao zitabomolewa.

Watajenga nyumba,

lakini hawataishi ndani yake;

watapanda mizabibu

lakini hawatakunywa divai yake.

Siku Kubwa Ya Bwana

141:14 Yer 30:7; Ufu 6:17; Yoe 1:15; 2:1; Mal 4:5; Eze 7:7; Dan 7:13“Siku kubwa ya Bwana iko karibu:

iko karibu na inakuja haraka.

Sikilizeni! Kilio katika siku ya Bwana

kitakuwa kichungu,

hata shujaa atapiga kelele.

151:15 1Sam 2:9; Mk 13:24-25; Yoe 2:2Siku ile ni siku ya ghadhabu,

siku ya fadhaa na dhiki,

siku ya uharibifu na ukiwa,

siku ya giza na utusitusi,

siku ya mawingu na giza nene,

161:16 Yer 4:19; 8:16; Hos 5:8; Amo 3:6; Kum 28:52; Isa 2:15siku ya tarumbeta na mlio wa vita

dhidi ya miji yenye ngome

na dhidi ya minara mirefu.

171:17 Kum 28:52; Isa 59:10; Yer 9:22; Za 79:3; 83:10Nitawaletea watu dhiki,

nao watatembea kama vipofu,

kwa sababu wametenda dhambi

dhidi ya Bwana.

Damu yao itamwagwa kama vumbi

na matumbo yao kama taka.

181:18 Ay 20:20; 40:11; Eze 7:11; 7:19; Kum 29:20; Sef 3:8; Mwa 6:7Fedha yao wala dhahabu yao

hazitaweza kuwaokoa

katika siku hiyo ya ghadhabu ya Bwana.

Katika moto wa wivu wake

dunia yote itateketezwa,

kwa maana ataleta mwisho

wa wote wanaoishi katika dunia ghafula.”