Ruthu 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ruthu 3:1-18

Ruthu Na Boazi Kwenye Sakafu Ya Kupuria

13:1 Rut 1:9, 14, 19; 1Kor 7:36; 1Tim 5:8; Kum 4:40; Za 128:2; Yer 22:15, 16Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti yangu, je, nisingelikutafutia pumziko ambako utatunzika vyema? 23:2 Rut 2:1, 8; Law 2:14; Hes 18:27; Amu 6:11Je, Boazi, ambaye umekuwa pamoja na watumishi wake wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya kupuria. 33:3 2Sam 12:20; 14:2; 2Fal 5:10; Za 26:6; 51:2; Isa 1:16; 61:3; Yer 4:14; Eze 16:9; Mwa 41:14; Kut 32:6; Mhu 2:3; Yer 15:17Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale mpaka atakapomaliza kula na kunywa. 4Atakapokwenda kulala, angalia mahali atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake, ulale. Naye atakuambia utakalofanya.”

53:5 Efe 6:1; Kol 3:20Ruthu akajibu, “Lolote usemalo nitatenda.” 63:6 Hes 18:27Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya.

73:7 Amu 19:6; 1Sam 25:36; 2Sam 13:28; 1Fal 21:7; Es 1:10; Wim 7:2; 2Nya 31:6; Yer 50:26; Hag 2:16Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala. 8Usiku wa manane, kitu kilimshtua Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke amelala miguuni pake.

93:9 Eze 16:8; Rut 2:20Akauliza, “Wewe ni nani?”

Akajibu, “Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa.”

103:10 Amu 17:2; Yos 2:12Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na Bwana. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini. 113:11 Mit 12:4; 14:1; 31:10Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri. 123:12 Rut 2:20; 4:1Ingawa ni kweli kwamba mimi ndiye jamaa aliye karibu, bado kuna mtu mwingine wa jamaa aliye karibu zaidi wa kukomboa kuliko mimi. 133:13 Kum 25:5; Rut 4:5, 6; Mt 22:24; Amu 8:19; Yer 4:2; Ebr 6:16; Hes 14:21; Hos 4:15Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama Bwana aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.”

143:14 Hes 18:27; Rum 14:16; 2Kor 8:21; Rum 12:17; 14:16; 2Kor 8:21; 1The 5:22; 1Pet 2:12Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema pasipo mtu kuweza kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”

153:15 Isa 3:22Pia akamwambia, “Leta shela yako uliyoivaa, uitandaze.” Naye alipoitandaza, akamimina vipimo sita vya shayiri, akamtwika. Kisha Ruthu akarudi zake mjini.

16Basi Ruthu alipofika kwa mama mkwe wake Naomi, akamuuliza, “Je, binti yangu, ilikuwaje huko?”

Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi alichomfanyia. 17Akaendelea kusema, “Amenipa shayiri vipimo sita3:17 Vipimo sita vya shayiri ni sawa na kilo 15. akisema, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ ”

183:18 Za 37:3-5Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu, mpaka utakapojua kwamba hili jambo limekwendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia mpaka akamilishe jambo hili leo.”