Ruthu 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ruthu 1:1-22

Naomi Na Ruthu

11:1 Amu 2:16-18; Mwa 12:10; 35:19; 36:35; 47:4; 2Fal 6:25; Hag 1:11; Za 105:16; Kum 28:38; 1Fal 18:2; Mik 5:2Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu. 21:2 Rut 2:1; 4:3; Amu 3:30; 1Sam 16:18; Mwa 35:16-19Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu, wakaishi huko.

3Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili. 41:4 1Fal 11:1; Mt 1:5; Rut 4:13; Ezr 9:2; Neh 13:23Nao wakaoa wanawake Wamoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na wa pili aliitwa Ruthu. Baada ya kama miaka kumi, 51:5 Rut 2:11Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.

61:6 Mwa 11:31; 36:35; 38:16; 50:24; Kut 4:31; Yer 29:10; Sef 2:7; Za 80:14; Zek 10:3; Lk 1:68; 7:16; Mwa 28:20; 48:15; Mit 30:8; Isa 55:10; Mt 6:11; Za 132:15Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba Bwana amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiandaa kurudi nyumbani. 7Yeye na wakweze wawili wakaondoka pale walipokuwa wakiishi na kushika njia kurudi nchi ya Yuda.

81:8 Mwa 38:11; 19:19; Yos 24:25; 2Tim 1:16Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. Bwana na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi. 91:9 Rut 3:1; Mwa 27:27, 38; 29:11; Hes 25:6Bwana na amjalie kila mmoja wenu maisha mema nyumbani kwa mume mwingine.”

Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti kubwa, 10wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe nyumbani kwa watu wako.”

111:11 Mwa 38:11; Kum 25:5Lakini Naomi akasema, “Rudini nyumbani, binti zangu. Kwa nini mnifuate? Je, mimi nitaweza tena kuwa na wana wengine ambao wataweza kuwaoa ninyi? 12Rudini nyumbani, binti zangu; mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa bado kuna tumaini kwangu, hata kama ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa wana, 131:13 Mwa 38:11; Kut 1:14; 15:23; 1Sam 30:6; Ay 19:21; Za 32:4; 38:2; Amu 2:15; 4:5je, mngesubiri mpaka wakue? Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La, hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko ninyi, kwa sababu mkono wa Bwana umekuwa kinyume nami!”

141:14 Rut 2:11; 3:1; Mik 7:6; Mit 17:17; 18:24; Yn 6:66-69; Ebr 10:39; Mwa 31:28; Kum 10:20Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake, akaenda zake, lakini Ruthu akaambatana naye.

151:15 Kum 25:7; Yos 24:14; Amu 11:24Naomi akamwambia, “Tazama, mwenzako anarejea kwa watu wake na kwa miungu yake. Rudi pamoja naye.”

161:16 2Fal 2:2; Yos 24:15; Mwa 24:58; Za 45:10; Rut 2:11-12Lakini Ruthu akajibu, “Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 171:17 1Sam 3:17; 14:44; 20:13; 25:22; 1Fal 2:23; 19:2; 20:10; 2Sam 3:9; 19:13; 2Fal 6:31; 15:21Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. Bwana na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo.” 181:18 Mdo 21:14Naomi alipotambua kwamba Ruthu amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena.

191:19 Amu 17:7; Isa 23:7; Mt 21:10; Mao 2:15Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?”

201:20 Mwa 15:1; 17:1; Za 91:1; Kut 6:3; Ay 6:4Akawaambia, “Msiniite tena Naomi,1:20 Naomi maana yake Wa Kupendeza, Wa Kufurahisha. niiteni Mara,1:20 Mara maana yake Chungu. kwa sababu Mwenyezi1:20 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. amenitendea mambo machungu sana. 211:21 Ay 1:21; 30:11; Za 88:7; Isa 53:4Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Bwana amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Bwana amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”

221:22 Rut 2:2-6, 21; 4:5, 10; Kut 9:31; Mwa 11:31; Law 19:9; 2Sam 21:9Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthu Mmoabu mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu mwanzoni mwa kuvuna shayiri.