Obadia 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Obadia 1:1-21

11:1 Mwa 25:14; Isa 1:1; 21:11; Yoe 3:19; Mal 1:3; Eze 25:12-14; Yer 6:4-5; 49:7-22; Isa 11:14; 18:2; 34:11Maono ya Obadia.

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi kuhusu Edomu:

Tumesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:

Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,

“Inukeni, twendeni tukapigane vita dhidi yake.”

2“Angalieni, nitawafanya wadogo miongoni mwa mataifa,

mtadharauliwa kabisa.

31:3 Isa 14:13; 16:6; 2Fal 14:7; 2Nya 25:11-12; Ufu 18:7Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,

wewe unayeishi katika majabali ya miamba

na kufanya makao yako juu,

wewe unayejiambia mwenyewe,

‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’

41:4 Isa 10:14; 14:13; 14:14, 15; Ay 20:6; Amo 9:2; Yer 49:16; Hab 2:9Ingawa unapaa juu kama tai

na kufanya kiota chako kati ya nyota,

nitakushusha chini kutoka huko,”

asema Bwana.

51:5 Isa 24:13; Kum 4:27; 24:21“Ikiwa wevi wangekuja kwako,

ikiwa wanyangʼanyi wangekujia usiku:

Lo! Tazama ni maafa kiasi gani yangekuwa yanakungojea:

je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?

Kama wachuma zabibu wangekuja kwako,

je, wasingebakiza zabibu chache?

6Lakini tazama jinsi Esau atakavyotekwa,

jinsi hazina zake zilizofichwa zitatekwa nyara!

71:7 Yer 30:14; Za 41:9Wote ulioungana nao watakufukuza hadi mpakani,

rafiki zako watakudanganya na kukushinda,

wale wanaokula mkate wako watakutegea mtego,

lakini hutaweza kuugundua.

81:8 Ay 5:12; Isa 29:14“Katika siku hiyo,” asema Bwana,

“je, sitaangamiza watu wenye hekima wa Edomu,

watu wenye ufahamu katika milima ya Esau?

91:9 Mwa 36:11, 34; Amo 2:16; Za 76:5; Yer 49:22; Nah 3:13Ee Temani, mashujaa wako watatiwa hofu,

kila mmoja katika milima ya Esau

ataangushwa chini kwa kuchinjwa.

101:10 Yoe 3:19; Amo 1:11-12; Za 137:7; Mwa 47:21; Eze 35:5, 15; Mal 1:4; Eze 25:12-14; 35:9Kwa sababu ya jeuri uliyofanya dhidi ya ndugu yako Yakobo,

aibu itakufunika;

utaangamizwa milele.

111:11 Ay 6:27; Nah 3:10; Eze 24:6Siku ile ulisimama mbali ukiangalia

wakati wageni walipojichukulia utajiri wake

na watu wa nchi nyingine walipoingia malango yake

wakipiga kura kwa ajili ya Yerusalemu,

ulikuwa kama mmoja wao.

121:12 Eze 25:6; 35:15; Mit 17:5; 24:17; Mik 4:11; Ay 31:29Usingemdharau ndugu yako

katika siku ya msiba wake,

wala kufurahia juu ya watu wa Yuda

katika siku ya maangamizi yao,

wala kujigamba sana

katika siku ya taabu yao.

131:13 Eze 35:5Usingeingia katika malango ya watu wangu

katika siku ya maafa yao,

wala kuwadharau katika janga lao

katika siku ya maafa yao,

wala kunyangʼanya mali zao

katika siku ya maafa yao.

14Usingengoja kwenye njia panda

na kuwaua wakimbizi wao,

wala kuwatoa watu wake waliosalia

katika siku ya shida yao.

151:15 Yer 46:10; 50:29; Hab 2:8; Amu 1:7; Za 137:8; Eze 35:15; Yoe 2:31; 3:7-8; Eze 30:3; Amo 5:8“Siku ya Bwana iko karibu

kwa mataifa yote.

Kama ulivyofanya, nawe utafanyiwa vivyo hivyo,

matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako.

161:16 Yer 25:15; 49:12; Mao 4:21-22; Isa 51:17; Kut 15:17; Eze 25:12-14Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu,

vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo,

watakunywa na kunywa,

nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo.

171:17 Za 69:35; 74:2; Isa 14:1-2; Amo 9:11-15; Zek 8:12Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwepo

na wale watakaookoka;

nao utakuwa mtakatifu,

nayo nyumba ya Yakobo

itamiliki urithi wake.

181:18 Zek 12:6; Yer 49:10; Isa 1:31Nyumba ya Yakobo itakuwa moto,

na nyumba ya Yosefu itakuwa mwali wa moto;

nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu,

nao wataiwasha moto na kuiteketeza.

Hakutakuwa na watakaosalimika

kutoka nyumba ya Esau.”

Bwana amesema.

191:19 Isa 11:14; Sef 2:7; Yer 31:5; Hes 1:36Watu kutoka nchi ya Negebu

wataikalia milima ya Esau,

na watu kutoka miteremko ya vilima

watamiliki nchi ya Wafilisti.

Watayakalia mashamba ya Efraimu na Samaria,

naye Benyamini atamiliki Gileadi.

201:20 Lk 4:26; Yer 33:13; 1Fal 17:9-10Kundi la Waisraeli walioko uhamishoni Kanaani

watarudi na kumiliki nchi mpaka Sarepta.

Walioko uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu

watamiliki miji ya Negebu.

211:21 Dan 2:24, 44; Ufu 11:15; Zek 14:9; Isa 19:20; Amu 3:9; Za 22:28; 47:9Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayuni

kutawala milima ya Esau.

Nao ufalme utakuwa wa Bwana.