Nehemia 9 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Nehemia 9:1-38

Waisraeli Waungama Dhambi Zao

19:1 Law 26:40-45; Yos 7:6; 1Sam 4:12Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi ule ule, Waisraeli walikusanyika pamoja, wakifunga na kuvaa nguo za gunia na kujitia mavumbi vichwani mwao. 29:2 Ezr 6:21; Neh 13:3Wale wa uzao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Wakasimama mahali pao, na kuungama dhambi zao na uovu wa baba zao. 39:3 Neh 8:7Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria ya Bwana Mungu wao kwa muda wa robo siku, na wakatumia robo nyingine kwa kuungama dhambi na kumwabudu Bwana Mungu wao. 49:4 Ezr 10:23Walawi wafuatao walikuwa wamesimama kwenye ngazi: Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Hawa walimlilia Bwana Mungu wao kwa sauti kubwa. 59:5 Za 78:4; Kut 15:6-11; 1Nya 29:13Nao Walawi Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabnea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakasema: “Simameni mkamsifu Bwana Mungu wenu, yeye ambaye ni Mungu tangu milele hata milele.

“Libarikiwe jina lake tukufu, litukuzwe juu ya baraka zote na sifa. 69:6 Kum 6:4; Isa 37:16; Kut 8:19; Mk 12:29; Mdo 4:24Wewe peke yako ndiwe Bwana. Uliziumba mbingu, hata mbingu za mbingu na jeshi lote la mbinguni, dunia na vyote vilivyo ndani yake, na pia bahari na vyote vilivyomo ndani yake. Huvipa vitu vyote uhai, nalo jeshi la mbinguni linakuabudu wewe.

79:7 Mwa 11:28-31; 17:5“Wewe ni Bwana Mungu uliyemchagua Abramu na kumtoa kutoka Uru ya Wakaldayo, nawe ukamwita Abrahamu. 89:8 Ezr 9:1; Yos 23:14; 21:45; Mwa 15:6; Ezr 9:15Uliona kuwa moyo wake ni mwaminifu kwako, nawe ukafanya Agano naye kuwapa wazao wake nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi. Umetimiza ahadi yako kwa sababu wewe ni mwenye haki.

99:9 Kut 2:23-25; 14:10-30“Uliona mateso ya baba zetu huko Misri, ukasikia kilio chao huko Bahari ya Shamu. 109:10 Za 74:9; Kut 9:16; Yer 32:20; Dan 9:15Ulituma ishara za miujiza na maajabu dhidi ya Farao, dhidi ya maafisa wake wote na watu wote wa nchi yake, kwa kuwa ulifahamu jinsi Wamisri walivyowafanyia ufidhuli. Ukajifanyia jina linalodumu hadi leo. 119:11 Kut 14:21; 15:4-5; Za 78:13; Ebr 11:29Ukagawa bahari mbele yao, ili waweze kupita katikati yake penye nchi kavu, lakini uliwatupa Wamisri waliowafuatilia katika vilindi, kama jiwe kwenye maji mengi. 129:12 Kut 13:21; 15:13Mchana uliwaongoza kwa nguzo ya wingu, na usiku kwa nguzo ya moto kuwamulikia njia iliyowapasa kuiendea.

139:13 Kut 19:11, 19; Za 119:137; Kum 4:7-8; Rum 7:12“Ulishuka katika Mlima Sinai, ukanena nao kutoka mbinguni. Uliwapa masharti na sheria zile ambazo ni za kweli na haki, pia amri na maagizo mazuri. 149:14 Mwa 2:3; Kut 20:8-11Uliwafahamisha Sabato yako takatifu na ukawapa amri, maagizo na sheria kupitia mtumishi wako Mose. 159:15 Za 78:24-25; Yn 6:31; Kut 16:14-15; Hes 20:7-13Katika njaa yao uliwapa mkate kutoka mbinguni, na katika kiu yao uliwatolea maji kutoka kwenye mwamba. Uliwaambia waingie na kuimiliki nchi ambayo ulikuwa umeapa kuwapa kwa mkono ulioinuliwa.

169:16 Kum 1:26-33; 31:27-29; Yer 19:15“Lakini wao, baba zetu, wakawa na kiburi na shingo ngumu, nao hawakutii maagizo yako. 179:17 Kut 34:6; Amu 8:34; Kut 22:27; Hes 14:1-4; Eze 5:6Wakakataa kusikiliza na kushindwa kukumbuka miujiza uliyoifanya miongoni mwao. Wakawa na shingo ngumu, na katika uasi wao wakamchagua kiongozi ili warudi kwenye utumwa wao. Lakini wewe ni Mungu mwenye kusamehe, mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo. Kwa hiyo hukuwaacha, 189:18 Kut 32:4hata wakati walijitengenezea sanamu ya ndama ya kusubu na kusema, ‘Huyu ni mungu wenu, aliyewapandisha kutoka nchi ya Misri,’ au walipofanya makufuru makubwa.

199:19 Za 106:45; Kut 13:21, 22; Hes 14:14“Kwa sababu ya huruma zako kuu hukuwaacha jangwani. Wakati wa mchana ile nguzo ya wingu haikukoma kuwaongoza katika njia yao, wala nguzo ya moto haikuacha kuwamulikia usiku njia iliyowapasa kuiendea. 209:20 Hes 9:17; Hag 2:5; Kut 16:15; 17:6Uliwapa Roho wako mwema ili kuwafundisha. Hukuwanyima mana yako vinywani mwao, nawe ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao. 219:21 Kum 2:7; 8:4Kwa miaka arobaini uliwatunza jangwani. Hawakukosa chochote, na nguo zao hazikuchakaa wala miguu yao haikuvimba.

229:22 Hes 21:21, 33; Kum 2:26–3:11; Mwa 15:5“Uliwapa falme na mataifa, ukiwagawia hata mipaka ya mbali. Wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani. 239:23 Mwa 12:2; Law 26:9; Hes 10:36Uliwafanya wana wao kuwa wengi kama nyota za angani, nawe ukawaleta katika nchi ambayo uliwaambia baba zao kuingia na kuimiliki. 249:24 Yos 11:23; Amu 4:23; 2Nya 14:13Wana wao wakaingia na kuimiliki nchi. Uliwatiisha Wakanaani mbele yao, walioishi katika nchi, ukawatia Wakanaani mikononi mwao, pamoja na wafalme wao na watu wa nchi, wawafanyie kama wapendavyo. 259:25 Kum 6:10-12; Hes 13:27; Kum 8:8-11; Eze 20:6Wakateka miji yenye ngome na nchi yenye rutuba, wakamiliki nyumba zilizojazwa na vitu vizuri vya kila aina, visima vilivyochimbwa tayari, mashamba ya mizabibu, mashamba ya mizeituni na miti yenye matunda kwa wingi. Wakala, wakashiba nao wakanawiri sana, wakajifurahisha katika wema wako mwingi.

269:26 Mdo 7:52“Lakini hawakukutii nao wakaasi dhidi yako, wakatupa sheria zako nyuma yao. Wakawaua manabii wako, waliowaonya ili wakurudie, na wakafanya makufuru makubwa. 279:27 Hes 25:17; Za 51:1Hivyo ukawatia mikononi mwa adui zao, ambao waliwatesa. Lakini walipoteswa, wakakulilia wewe. Kutoka mbinguni uliwasikia, nawe kwa huruma zako kuu ukawapa waokozi, waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.

289:28 Kut 32:22; Amu 2:17; 2Sam 24:14; Za 22:4; 106:43; 136:24“Lakini mara walipokuwa na raha, wakafanya maovu tena machoni pako. Kisha ukawaacha mikononi mwa adui zao, nao wakawatawala. Walipokulilia tena, ukasikia kutoka mbinguni, na kwa huruma zako ukawaokoa kila mara.

299:29 Za 5:5; Kum 4:29; Isa 2:11; Kum 30:16; Yer 25:3-7; Zek 7:11-12“Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza. 309:30 Isa 63:10; 1Fal 17:13-18; 2Nya 36:16Kwa miaka mingi ulikuwa mvumilivu kwao. Kwa njia ya Roho wako ukawaonya kupitia manabii wako. Hata hivyo hawakujali, basi ukawatia mikononi mwa mataifa jirani. 319:31 Yer 5:10; 4:27; Isa 48:9Lakini kwa rehema zako kuu hukuwakomesha wala kuwaacha, kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na rehema.

329:32 2Fal 17:3; 1Fal 8:23; Ay 9:19“Basi sasa, Ee Mungu wetu, uliye mkuu, mwenye nguvu na Mungu wa kuogofya, mwenye kushika agano lake la upendo, usiache taabu hizi zote zionekane kuwa kitu kidogo mbele za macho yako, taabu hizi zilizotupata, juu ya wafalme wetu na viongozi, juu ya makuhani wetu na manabii, juu ya baba zetu na watu wako wote, tangu siku za wafalme wa Ashuru hadi leo. 339:33 Mwa 18:25; Dan 9:14Katika hayo yote yaliyotupata, umekuwa mwenye haki, na umetenda kwa uaminifu, wakati sisi tumetenda mabaya. 349:34 2Fal 23:11; Yer 44:17Wafalme wetu, viongozi wetu, makuhani wetu na baba zetu hawakufuata sheria yako. Hawakuzingatia amri zako wala maonyo uliyowapa. 359:35 Isa 63:7; Kum 28:45-48Hata walipokuwa wangali katika ufalme wao, wakiufurahia wema wako mkuu katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa, hawakukutumikia wala kugeuka kutoka njia zao mbaya.

369:36 Kum 28:48; Ezr 9:9“Lakini tazama, sisi ni watumwa leo, watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu ili wapate kula matunda yake na vitu vingine vizuri inayozalisha. 379:37 Kum 28:33; Mao 5:5Kwa sababu ya dhambi zetu, mavuno yake mengi huenda kwa wafalme uliowaweka watutawale. Wanatawala juu ya miili yetu na mifugo yetu kama wapendavyo. Tuko katika dhiki kuu.

Mapatano Ya Watu

389:38 2Nya 23:16; Isa 44:5“Kwa sababu ya haya yote, tunajifunga katika mapatano, na kuyaandika, nao viongozi wetu, Walawi wetu na makuhani wetu wanatia mihuri yao.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

尼希米记 9:1-38

以色列人认罪祷告

1这月二十四日,以色列人聚集禁食。他们身披麻衣,头撒尘土。 2以色列人与其他外族人隔离,站着承认自己的罪恶和祖先的过犯。 3他们站在自己的地方,宣读他们上帝耶和华的律法书,长达三个小时9:3 “三个小时”希伯来文是“一天的四分之一”。。他们又用了三个小时认罪,敬拜他们的上帝耶和华。 4利未耶书亚巴尼甲篾示巴尼布尼示利比巴尼基拿尼站在台阶上,大声呼求他们的上帝耶和华。 5利未耶书亚甲篾巴尼哈沙尼示利比荷第雅示巴尼毗他希雅说:“起来称颂你们的上帝耶和华,直到永永远远。耶和华啊,你荣耀的圣名当受称颂!愿你的名被尊崇,超过一切称颂和赞美!

6“你,唯有你是耶和华!你创造了天、天上的天和天上的万象、地和地上的一切、海和海中的一切,你赐给万物生命。众天军都敬拜你。 7你是耶和华上帝,你拣选了亚伯兰,带他离开迦勒底吾珥,又给他改名为亚伯拉罕8你知道他对你忠心,就与他立约,把迦南人、人、亚摩利人、比利洗人、耶布斯人及革迦撒人的土地赐给他的后代。你实现了你的应许,因为你是公义的。

9“你看见我们祖先在埃及所受的苦,又听见他们在红海边的呼求, 10就行神迹奇事对付法老及其所有的臣仆和国民,因为你知道他们对以色列人行事狂傲。你使自己威名远扬直到今日。 11你在我们祖先面前把海水分开,使他们在海中走干地过去;你把追赶他们的人扔进深海,好像把石头扔进大水中。 12白天,你用云柱带领他们;夜间,你用火柱照亮他们当走的路。 13你降临在西奈山,从天上与他们说话,赐给他们公正的典章、信实的律法、美好的律例和诫命。 14你使他们知道你的神圣安息日,借你仆人摩西赐给他们诫命、律例和法度。 15他们饿了,你赐下天粮给他们吃;他们渴了,你使磐石流出水给他们喝。你吩咐他们去占领你起誓要赐给他们的土地。 16但我们的祖先行事狂傲,顽固不化,不肯听从你的诫命。 17他们拒绝听从,忘记了你为他们所行的奇事,顽固不化,自立首领要回埃及做奴隶。但你是乐意饶恕,有恩典,好怜悯,不轻易发怒,充满慈爱的上帝,你没有离弃他们。 18纵使他们为自己铸造了一头牛犊,声称那是带他们出埃及的上帝,大大亵渎了你, 19你还是对他们大施怜悯,没有在旷野离弃他们。白天,云柱没有离开他们,仍然引导他们前行;夜间,火柱仍然照亮他们当走的路。 20你差遣你良善的灵去教导他们,没有停止赐他们吗哪吃,也没有停止赐他们水喝。 21在旷野的四十年间,你供养他们,使他们一无所缺,他们的衣服没有穿破,脚也没有走肿。

22“你将列国列邦赐给他们,为他们划分疆界,他们占领了希实本西宏巴珊的土地。 23你使他们的子孙多如天上的星星,你带领他们进入你应许他们祖先的土地。 24他们的子孙进去占领了那地方,你在他们面前制服了住在那里的迦南人,把迦南诸王和那地方的人交在他们手里,任由他们处置。 25他们夺取坚固的城池、肥沃的土地、装满美物的房屋、挖好的水井、葡萄园、橄榄园以及各样果树。他们吃得饱足,身体发胖,享受你的厚恩。

26“然而,他们不顺从你,背叛你,把你的律法抛在背后,又杀掉劝诫他们归向你的众先知,大大亵渎了你。 27于是你把他们交在欺压他们的仇敌手中。他们在患难中向你呼求,你就从天上垂听,怀着丰盛的怜悯赐给他们拯救者,把他们从仇敌手中拯救出来。 28可是,他们得享平安后,又在你面前作恶,于是你离弃他们,把他们交在敌人手中,使敌人统治他们。他们回转向你呼求,你就从天上垂听,你一次次地怀着怜悯拯救他们。 29你警告他们,要使他们转向你的律法,但他们行事狂傲,不听从你的诫命,干犯你的典章。遵行这典章的人必因此而活。但他们背弃你,顽固不化,不肯听从。 30你多年来容忍他们,差遣你的灵借着你的众先知警告他们,但他们依然不肯听从,于是你把他们交在列邦手中。 31然而,你大施怜悯,没有完全毁灭他们,也没有离弃他们,因为你是有恩典、好怜悯的上帝。

32“因此,我们的上帝啊,你是伟大、全能、可畏、守约、施慈爱的上帝,求你不要轻看我们的王、首领、祭司、先知、祖先和你的子民,从亚述诸王时代直到今天所受的苦难。 33在这临到我们的一切事上,你都是公义的,因为你行事信实,我们行事邪恶。 34我们的王、首领、祭司和祖先没有遵行你的律法,也没有留心听从你的诫命和你给他们的警告。 35他们即使在本国,在你赐给他们广阔肥沃的土地上得享你的厚恩,也不事奉你,不离开恶道。 36今天,我们沦为奴隶,在你赐给我们祖先的土地上,在你让我们祖先享用其出产和各样美物的土地上,我们沦为奴隶。 37因为我们的罪过,这地方的丰富出产都归给了那些你派来统管我们的王。他们随意统管我们和我们的牲畜。我们生活在极大的苦难中。

38“鉴于此,我们郑重立约,记载下来。我们的首领、利未人和祭司都在上面盖了印。”